Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Huu uzi mbona umeunganishwa na wa 2013 ina maana mleta mada mzushi sio
 
Bavicha bwana yaani kupiga miluzi ndio anahesabia kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi; bure kabisa.
Gharama kabisa ni ipi, pale tunaposema diwani fulani anataka kuhamia sisiemu kwa kuunga mkono juhudi za Pombe alafu haonekani au, kukimbia na Box la kupigia kura kisha linarudishwa na Askari.?
 
Kwa bahati mbaya unadhani unaongea na mtoto au mtu asiyeifahamu Arusha. Naifahamu Arusha ndani nje. Ngoja nikueleze vizuri kwani unaonekana kumezwa na propaganda mfu. Arusha inategemea utalii wa wazungu na hakuna siku utalii huo uliwahi kusimama kwani hautegemei fadhila za wanasiasa wa ccm au viongozi wa serekali. Kilichopungua ni mikutano ya kiserekali tena nayo ilifanyika hivyo kwa hila ili itumike kupiga propaganda. Alipoingia Magufuli mikutano mingi ameizuia tena ni kwa nchi nzima sio kwa Arusha tu. Utalii wa wazungu umeendelea kukua Arusha tena bila jitihada za wazi za serekali, nakuambia jambo ninalolifahamu sio unayoambiwa na makada wa ccm kwa koti la serekali. Nina ushahidi wa hotel kuongezeka kwa ajili ya biashara ya utalii wa wazungu, achia mbali huo utalii mwingine hewa unaouzungumza. Ama kama unaweza leta ushahidi kwamba wazungu waliacha kuja arusha kisa kuna maandamano.

Kuhusu maandamano, hapa ndio ninapokuambia siasa chafu zilipojikita, na kwa bahati nzuri wananchi wa Arusha wanajitambua. Maandamamano yaliyowahi kufanyika Arusha wakati Lema akiwa mbunge hayajawahi kuzidi mara 3 na tena yote yalikuwa na sababu za msingi. Na maandamano haya yaliongozwa na Dr. Slaa ambaye leo hii mnamsujudia huko ccm. Maandamano ya kwanza yalikuwa kuhusu uchaguzi wa meya ambao utaratibu ulikiukwa. Maandamano ya pili ni Lema alipotoka gerezani baada ya kufungwa kwa hila enzi za JK. Tena haya hayakuwa maandamano bali ni kumsindikiza mpendwawao kwenye ofisi za cdm baada ya kushinda kesi kwa rufaa. Ili uonyeshe kwamba wewe sio mnafiki taja hayo maandamano mengi ili tuyaone hapa.

Kuhusu maendeleo, Arusha ina maendeleo muda mrefu na kwa taarifa yako baadaya Dar na Mwanza, Arusha ni ya tatu kwa maendeleo na kuchangia upande wa kodi. Na kinachofanya Arusha iwe na maendeleo ni uwepo wa wafanyabiashara wengi ambao wala hawaangalii hizo siasa zenu za majitaka. Na ushahidi kwamba wananchi wa Arusha wanajielewa na wala hawahadaiki na hizo siasa zenu chafu ni kule kushangiliwa. Wewe unaongea kile unacholishwa na wa viongozi wa ccm kupitia nafasi zao za kiserekali. Arusha ina maendeleo ya kutosha, na kinachofanywa na hao makada wa ccm ni kulitamani jimbo la Arusha, hivo wanaleta siasa za majitaka, lakini wananchi wa Arusha wanaelewa hizo ghiliba. Kwa ghiliza za hivyo mpelekee ile mikoa yenye watu wenye uelewa mdogo wanaoaminishwa kwamba mbunge analeta maendeleo. Nikushauri acha kuendekeza siasa za majitaka wakati watu tuna uelewa wa kutosha.
Mkuu rekebisha, baada ya Dar kwa maendeleo inafuata Arusha, Mwanza hamna kitu
 
Wewe bado una siasa za ushabiki lakini una uelewa mdogo. Nikuambie kitu, maendeleo yanaletwa na serekali na sio mbunge. Watu wenye uelewa mdogo ndio huwa wanaambiwa mbunge ndio anayeleta maendeleo. Zamani tulikuwa tukiona barabara, au miundu mbinu ya maji nk tulikuwa tunaambiwa ni mbunge kaleta. Lakini tulipojitambua tukafahamu ukweli. Kama ni huo ujinga wa kusema kwamba mbunge kaleta maendeleo basi ngoja na mimi niwe mjinga kama wewe. Wakati Lema anaingia madarakani barabara za mji zilikuwa mbovu ile mbaya. Sasa hivi barabara nyingi za mji zimejengwa kwa kiwango cha lami. Miinduo mbinu mbalimbali imeboreshwa kwa sana. Shule zimeongezeka yakiwemo na madarasa kuongezeka kwenye shule kongwe. Mambo haya zamani tuliingopewa ni mbunge analeta. Kama ndio hayo basi Lema amefanya mambo makubwa ile mbaya. Nitakupa kazi za mbunge hapo chini ili kukutoa ujinga
  1. Muwakilishi wa wananchi wake bungeni
  2. Kuisimamia na kuishauri serekali
  3. Kutunga sheria
Hizo ndio kazi za mbunge. Na kama ni kipimo cha mbunge kufanya kazi za maendeleo yaliyo kwenye eneo lake. Basi Lema ukiachia majimbo ya Dar, na mawili ya nyamagana na Mwanza, Lema ndio mbunge bora. Usiwe mjinga kuuliza kazi za maendeleo alizofanya mbunge wakati sio jukumu lake. Na hapa ndio nakuona una uelewa mdogo wa kazi za mbunge na ndio maana unaauliza kama mtu wa kijijini. Kuna majimbo ambayo hayajawahi kuongozwa na mpinzani lakini wanamaisha duni kuliko unavyoweza kudhani.
Mkuu achana na huyo shoga, naona anawashwa washwa amekosa wa kumkuna
 
Wale vijana wa kikurya mliowatumia 2015 mmewatelekeza magerezani bila Msaada wowote na waliwasaidia kuongeza idadi ya wabunge, na madiwani wenu Kwa kuwatisha wanaccm Kwa mapanga ili wasiende kupiga kura.
Chadema mungu anawaona
We mwanamke, tatizo ni Lema kushangiliwa au una dukuduku lingine? Maana naona umejaa nyembe kweli kweli!
 
Picha ya waumini?, Kwahiyo hapo ilikuepo Arusha mjini yote?, nikwambie tu Lema ni Msanii aliefuzu ngazi zote, hawa washangiliaji aliwapanga na alitegemea mkuu wa nchi atamwita asalimie, akadunda.
Jana kwenye ufunguzi wa nyumba za askari alikacha Kwa sababu hakuwa kapanga watu wa kumpigia vigergere aonekane bado wamo kumbe Kwisha habari yake
Umeulizwa ukitaka kupima virusi vya UKIMWI unakausha damu yote unapeleka na ndoo au unachukua tu sample? Huoni hata aibu mkuu?

Haya, huko kanisani kanunua watu wamshangilie, je na hapa JF kanunua watu? Maana tangu mwanzoni mwa uzi nakuona wewe peke yako ndio umejaa nyembe.

Nakuangalia tu nakucheki nasema hiiiiiiiiiiiiii...!
 
Back
Top Bottom