Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

naomba kujiunga na chama chenu jamani kwani huku niliko naona propaganda tu hakuna chochote
Ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa Mungu katika harakati zetu za kutafuta Uhuru wa kweli katika Taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika Siasa za Tanzania na wala sio Arusha peke yake , Nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema “ MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa Arusha na Tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa Mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika Siasa za Nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka Ndugu , Jamaa na Watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale Viwanja vya Soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya Watu wote wenye ni njema na amani ya Taifa hili .

Ushindi huu tumepewa na Mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , Wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya Mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari Mke wangu aliniambia “ Kila mahali Duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache Siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote Mungu hatawaponya Godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? kwanini ? nitamuomba Mungu damu za Watu waliokufa Mungu atalipa “ Usiogope Mume wangu , Mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona “ NEEMA LEMA .

Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani “ Only time will tell “ wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya “ Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa Huru na Haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa Chadema takribani wiki tano lakini CCM na viongozi wake waliendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili CCM watumie mtandao wao wa Mabalozi wa Nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na Polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa Mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku CCM wakiamini mtandao wao wa Mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake Mabalozi wa CCM walibeba na kukumbusha Watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , Watu walipigwa na Green Guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema “ TUNAKUSHUKURU MUNGU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .
Arusha Mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini MSIOGOPE

Tunakushukuru sana Mwenyezi Mungu na Watu wote Arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , Wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa Mungu.
Timu zote za Kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda Chama na Wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata Wapinzani wetu na Maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha , Asanteni sana .

Ni mimi Rafiki yenu .
Godbless J Lema ( MB)
 
Hakika Lema ni mwamba na juu yake litajengwa taifa jipya la Tanganyika

Mungu ibariki Tanganyika
Mungu tubariki Watanganyi na AFRIKA kwa ujumla
 
Lema na madiwani wako kazi yenu sasa ni kuhakikisha mnamng'oa meya wa magamba na kuweka meya wa watu ili muweze kupiga kazi mtuletee maendeleo tunayoyahitaji kwa kudhibiti mapato yote yanayokusanywa yatumike inavyopaswa.
 
Kamanda Mungu akurehemu sana kwa kazi nzuri na ngumu mnayoifanya. Mmefanya Arusha kuwa jiji la mfano mpaka kiasi cha wale magamba kuweweseka mpaka leo hakuna aliye tayari kuongelea uchaguzi wa Arusha. Hongereni sana na sisis tuko pamoja na nyie katika vita hii ya ukombozi wa fikra. Waliokuwa wanasema Chadema itakufa sasa wanaogopa hata vivuli vyao.

"IF GOD IS WITH US NO ONE CAN BE AGAINST US"

Jana niliandika thread kuhusu wasifu wa Lema ulivyochangia ushindi wa Arusha, kwa bahati mbaya iliondolewa na kuunganishwa nisikojua. Nakubaliana na awuyegani kuwa Lema ni mtu Adimu ndani ya Chadema. Ana hoja zenye ushiwishi mkubwa sana ambazo mbele ya safari zitachangia kuiangusha ccm nchi nzima. Mungu amlinde Lema na watoa kucha bila ganzi.

Jina la Lema siyo tu imetishia amani ya Mkuu wa Mkoa na ccm, bali hata kiti cha Kikwete kimeyumba kwa ujasiri wa kamanda Lema.
Lema ni zaidi ya wanavyomfahamu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Lema na madiwani wako kazi yenu sasa ni kuhakikisha mnamng'oa meya wa magamba na kuweka meya wa watu ili muweze kupiga kazi mtuletee maendeleo tunayoyahitaji kwa kudhibiti mapato yote yanayokusanywa yatumike inavyopaswa.

Meya aliyekalia kiti cha damu atang'olewa bila kupenda.
Huu ni mkakati wa haki na vita ya haki tutapigana

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Bora kabisa, uchaguzi urudiwe, hatujaridika na idida ya kura tulizopata!. Ratio ilikuwa iwe 1: 10. Tume harakisha uchaguzi urudiwe na ile kata nyingine ya sombetini tupate mpango mzima.

Afu Sugu kachukia kwanini ccm wamepata kura

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Watanzania tupo nyumayako na hayo ndo mageuzi yakweli; tumechoka na manyanyaso yao hakika bado kitambo kidogo respect to all Tanzanian together as one in the Name of jesus amen.
 
Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa NEEMA LEMA kwa kumpa support ya dhati kabisa MB. GODBLESS LEMA. Pili napenda kutoa shukrani za dhati kabisa MB. GODBLESS LEMA kwa kuwaongoza wanaARUSHA katika kipindi KIGUMU na HATARI sana katika maisha yake na maisha ya wanaARUSHA wote kwa ujumla na bila kusahau shukrani zangu za dhati kabisa kutoka ndani ya moyo wangu ziwaendee wanaARUSHA na CHADEMA. Asanteni.
 
aiseee thats great words....lema wewe ni kiongozi ni zaidi ya mwana siasa...asanten wana arusha
 
Mwendo Mdundo, kura za CCM Arusha zinazidi kuongezeka.
Wapiga kura Elfu sitini (60,000)
Wliojitokeza Elfu Tisa (9,000).
Hapo ratio hakuna, the turn -up is too low.
It means Elfu Hamsini plus waliojitokeza kupiga kura kwa CCM jumla CCM ina Mtaji wa Kura Elfu Hamsini zaidi.
Hao waliogopa Mabomu na vitisho.
Ikumbukwe: Makundi ya wazee,vijana wa kike na akina mama hawakujitokeza kwa wingi kwa kuogopa fujo na mabomu.
Waliopiga kura uchaguzi kata nne, wengi wao ni Wavuta Bangi,Wanywa Viroba na Majambazi waliokuwa wakitisha watu wasijitokeze kupiga kura.
2015 Kitaeleweka tu.
 
Ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa Mungu katika harakati zetu za kutafuta Uhuru wa kweli katika Taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika Siasa za Tanzania na wala sio Arusha peke yake , Nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema “ MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa Arusha na Tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa Mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika Siasa za Nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka Ndugu , Jamaa na Watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale Viwanja vya Soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya Watu wote wenye ni njema na amani ya Taifa hili .

Ushindi huu tumepewa na Mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , Wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya Mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari Mke wangu aliniambia “ Kila mahali Duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache Siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote Mungu hatawaponya Godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? kwanini ? nitamuomba Mungu damu za Watu waliokufa Mungu atalipa “ Usiogope Mume wangu , Mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona “ NEEMA LEMA .

Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani “ Only time will tell “ wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya “ Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa Huru na Haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa Chadema takribani wiki tano lakini CCM na viongozi wake waliendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili CCM watumie mtandao wao wa Mabalozi wa Nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na Polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa Mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku CCM wakiamini mtandao wao wa Mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake Mabalozi wa CCM walibeba na kukumbusha Watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , Watu walipigwa na Green Guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema “ TUNAKUSHUKURU MUNGU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .
Arusha Mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini MSIOGOPE

Tunakushukuru sana Mwenyezi Mungu na Watu wote Arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , Wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa Mungu.
Timu zote za Kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda Chama na Wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata Wapinzani wetu na Maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha , Asanteni sana .

Ni mimi Rafiki yenu .
Godbless J Lema ( MB)

Time will tell
 
Back
Top Bottom