Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Nampenda Lema, nawapenda makamanda wote wa Arusha!!!!!!!!!!! Poleni sana magamba, mliipenda sana arusha lakini ndo hivyo. 4 bila imewahusu. Kaeni mkijua kwamba huu ni mwanzo mapambano yanaendelea Tanzania nzima hakuna kulala mpaka kieleweke. Peoples Powerrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nampenda Lema, nawapenda makamanda wote wa Arusha!!!!!!!!!!! Poleni sana magamba, mliipenda sana arusha lakini ndo hivyo. 4 bila imewahusu. Kaeni mkijua kwamba huu ni mwanzo mapambano yanaendelea Tanzania nzima hakuna kulala mpaka kieleweke. Peoples Powerrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jana niliandika thread kuhusu wasifu wa Lema ulivyochangia ushindi wa Arusha, kwa bahati mbaya iliondolewa na kuunganishwa nisikojua. Nakubaliana na awuyegani kuwa Lema ni mtu Adimu ndani ya Chadema. Ana hoja zenye ushiwishi mkubwa sana ambazo mbele ya safari zitachangia kuiangusha ccm nchi nzima. Mungu amlinde Lema na watoa kucha bila ganzi.
 
Tunamshukuru sana MUNGU wetu anayetumia wana wake kutuelimisha na kutuunganisha. Ni maneno ya busara na yenye hekima alioyasema Lema ambayo kama binadamu tuna kila sababu ya kushukuru.

Mungu na azidi kukuongoza na kukupa hekima na busara zaidi Lema!
 
Hata hivyo taarifa za ukweli ni kwamba ccm wanampango wa kwenda mahakamani

Bora kabisa, uchaguzi urudiwe, hatujaridika na idida ya kura tulizopata!. Ratio ilikuwa iwe 1: 10. Tume harakisha uchaguzi urudiwe na ile kata nyingine ya sombetini tupate mpango mzima.
 
asante kiongozi jasiri kabisa katika historia ya jimbo hili, mungu akuongezee ujasiri na busara ili tulipeleke gurudumu salama, asante wa kushukuru
 
Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .
Nimefika kwenye section hii, moyo wangu wote umefunguka na kuiona haki ya kweli iliyomo ndani ya CD.- hakuna mtu anayeweza kuchezea nguvu ya umma, CDM ni mioyo ya watu wanyonge, CDM ni zile damu zilizokwisha kumwagia bila hatia, CDM ni roho za watu waliokatishwa maisha yao wakiwa wanapigania haki, CDM ni wale wote waliofunguliwa kesi za kila aina, CDM ni wote walioko magelezani wakitumikia vifungo mbali mbali -- CDM ni mkombozi wa nchi yetu - CDM ndiye baba wa taifa letu jipya tunalolipigania.
 
Wakati mbunge wa arusha mjini Mh. Godblee Lema akihutubia mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo kata nne za jijini Arusha alikuja na kauli mbiu mpya ya amani, kwamba mfuasi wa CHADEMA ukibughudhiwa/kusukumwa mara ya kwanza tulia, ukisukumwa mara ya pili tulia, ukisukumwa mara ya tatu tulia, lakini ukisukumwa mara ya nne basi sikiliza maelekezo ya MUNGU. Nilimsikia mara nyingi Mh; Lema akiisema hii kauli huku akimalizia na kusema kuwa ''CHADEMA hatutaki utawala wa damu''.

Kwa kweli kauli mbiu hii inalipa na ninamuomba mhe. Lema aendelee nayo ila ipewe coverage kubwa na iwe kauli ya chama Taifa kwa wafuasi wake popote pale walipo nchini hadi 2015 uchaguzi mkuu maana ''CHADEMA hatutaki utawala wa damu''.... Hongera Mhe. Godblee Lema, Arusha umetujengea ujasiri wa ajabu na siku zote Arusha tutasimama na wewe.
 
maelekezo ya mungu kujipiga mabomu kwenye mikutano yenu?
 
maelekezo ya mungu kujipiga mabomu kwenye mikutano yenu?

Kama Mungu amelekeza vile hakuna shida lakini ndo hivyo aibu yenu... Mtaua miili lakini roho zetu zitadumu na adhabu yenu haina mfanowe.
 
safi sana kamanda lema kwa kurudisha furaha ya chama kwa wananchi ,ambao kimsingi ndio wapiga kura wako na madiwani pia .tunajifunza kutoka kwako shukurani sana kwa maneno mazuri yenye hekima ndani yake .
 
hana busara hata kidogo huyooooo!unless uniambie ameandikiwa hii speech!

Jali content za si source. Naona content imekuumiza mpaka hutaki kuamini. Don't under estimate people.

God bless Godbless Lema, Godbless chadema!
 
Ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa Mungu katika harakati zetu za kutafuta Uhuru wa kweli katika Taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika Siasa za Tanzania na wala sio Arusha peke yake , Nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema “ MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa Arusha na Tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa Mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika Siasa za Nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka Ndugu , Jamaa na Watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale Viwanja vya Soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya Watu wote wenye ni njema na amani ya Taifa hili .

Ushindi huu tumepewa na Mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , Wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya Mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari Mke wangu aliniambia “ Kila mahali Duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache Siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote Mungu hatawaponya Godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? kwanini ? nitamuomba Mungu damu za Watu waliokufa Mungu atalipa “ Usiogope Mume wangu , Mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona “ NEEMA LEMA .

Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani “ Only time will tell “ wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya “ Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa Huru na Haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa Chadema takribani wiki tano lakini CCM na viongozi wake waliendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili CCM watumie mtandao wao wa Mabalozi wa Nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na Polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa Mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku CCM wakiamini mtandao wao wa Mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake Mabalozi wa CCM walibeba na kukumbusha Watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , Watu walipigwa na Green Guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema “ TUNAKUSHUKURU MUNGU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .
Arusha Mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini MSIOGOPE

Tunakushukuru sana Mwenyezi Mungu na Watu wote Arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , Wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa Mungu.
Timu zote za Kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda Chama na Wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata Wapinzani wetu na Maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha , Asanteni sana .

Ni mimi Rafiki yenu .
Godbless J Lema ( MB)
maneno yenye hekima kubwa kwa watu makini,umenikumbusha maneno aliyowai kusema mzee wetu Mtei kumwambia Kikwete kwamba ccm hawawezi kupata ushindi bila kuiba kura na ndio maana pale penye ulizi imara ccm imeshindwa.
 
Very inspirational statement for movement for change. We thank you Lema for your motivative thanks to Arusha voters, both chadema and non chadema members.
 
Jali content za si source. Naona content imekuumiza mpaka hutaki kuamini. Don't under estimate people.

God bless Godbless Lema, Godbless chadema!
always i overestimate him but naelewa upeo wake ni mdogo sana
 
Mwaka 2015 ni mwaka wa ushindi kwa CDM na vijana wote waliokuwa na miaka kuanzia 14 mwaka 2010 wataweza kupiga kura mwaka 2015 kama uandikishaji utafanyika 2014, sifikirii kama kwa shida walizonazo wataweza kuwapigia CCM. Na kwa mambo ya M-pesa na tigo pesa vijana watajiandikisha kupata vitambulisho la msingi ni kuwa na mkakati wa kuwaelimisha ili wafahamu adui wa maendeleo CCM. Kwa wapiga kura wa 2010 CDM imeweza kuleta upinzani kwenye chaguzi za marudio na pengine kushinda, baada ya kuandikisha kundi hilo la vijana CCM ni bye bye.
 
Back
Top Bottom