Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Godbless Lema: Mungu tunakushukuru, Arusha asanteni sana

Ee Mungu Mwenyezi,

Daima tutakutukuza na kudumisha sifa zako.

Tunaanza na wewe na tunamaliza na wewe.

Amina.
 
G.Lema asante hata kwa kukumbuka kutoa neno la shukrani,
siyo kawaida kwa mwanasiasa kurudi na neno la 'ASANTE'

.........Asante zangu zikufikie kwa kujitoa mhanga kwa ajili ya ukombozi wa Tanzania.

Asanteni sana wana Arusha wote kwa moyo wa ujasiri mlio nao, siyo rahisi
kwa mtu wa kawaida kupigwa bomu na bado ukazidi kuwa jasiri kama wana
Arusha.


Nilikuwa namshangaa sana Arushaone aliposema anasimamia wapiga kura
kweli nilimwambia 'take care yourself'. Lakini Mungu aliwapigania na zoezi
likaisha tena kwa mafanikio makubwa.

Natamani kuona Tanzania ikiwa chini ya chama cha CHADEMA, natamani kuiona tena
Tanzania inayoongozwa kwa haki.

walitishia watu sana juzi wale binadamu(natamani kuwatukana)nilipofika kwenye kituo cha kura kulikuwa na PT za kutosha na zimesheheni hao binadamu, mmoja aliruka toka juu ya hiyo PT hadi karibu yangu eti ananiuliza unaenda wapi? kadi yako ya kupiga kura iko wapi? nikamuuliza napiga hapa hapa uliponisimamia au napiga eneo husika? akaniambia mbona jeuri sana wewe, nikamuangaliaa nikaliacha hapo, narudi kwenye gari wameniziba kutoka, nikaingia kwenye gari nikakaa mpaka walipojisikia kunipa njia, mxsiii na kama sio yale matisho yao wangehesabu kura mbili mbili kila vituo, ovyooo zao.
 
Pamoja kamanda,ila bado tuna deni la kuwataja wahusika wa mlipuko pale soweto kwa majina. Ningependekeza tuombe mkutano wa kuwashukuru wanaArusha na hapo tumalize kiu pomaja na mikakati ya kutimiza ahadi zetu ambazo ziko ndani ya uwezo wetu thanx naomba kuwasilisha
 
Pole sana Nyamayao
nyie na majasiri
kweli dar tusingedhubutu

Natamani dar tungesimama imara kama wana arusha au wana mbeya
kweli nchi ingebadilika.

Lakini naamini hata huku tutajifunza kutoka kwenu.

walitishia watu sana juzi wale binadamu(natamani kuwatukana)nilipofika kwenye kituo cha kura kulikuwa na PT za kutosha na zimesheheni hao binadamu, mmoja aliruka toka juu ya hiyo PT hadi karibu yangu eti ananiuliza unaenda wapi? kadi yako ya kupiga kura iko wapi? nikamuuliza napiga hapa hapa uliponisimamia au napiga eneo husika? akaniambia mbona jeuri sana wewe, nikamuangaliaa nikaliacha hapo, narudi kwenye gari wameniziba kutoka, nikaingia kwenye gari nikakaa mpaka walipojisikia kunipa njia, mxsiii na kama sio yale matisho yao wangehesabu kura mbili mbili kila vituo, ovyooo zao.
 
Last edited by a moderator:
Kwa niaba ya watu wa majengo tunakushukuru sana kamanda, hata sisi tulipigania sana kampeni zetu huku nakutoa elimu, pamoja tukashinda. Tulianza na mungu tukamaliza na mungu.
 
1002316_555828297812696_2004089766_n.jpg

tatizo siyo kung'ata ila umengatwa wapi.
 
Jinsi Mheshimiwa Lema alivyomaliza ujumbe wake umenichekesha sana!

" Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha
, Asanteni sana."
 
Nikiwa kama 'mwanaCCM' mwenye itikadi za TANU nawapa hongera sana CHADEMA kwa ushindi mkubwa lakini pia kwa namna walivyofanya kampeni zao kwa AMANI, HAKI na HEKIMA kubwa sana.

Pasipo kinyongo wala unafiki napenda kusema kuwa ni kweli kabisa CHADEMA kwa sasa ni chama kilichokomaa kisiasa.
 
Umekaribia kunitoa machozi ingawa na mimi nimpiganaji, nakushukuru kamanda! Tunahitaji wapiganaji style ya Lema kila mahali Tanzania. Napenda kuwatia moyo Arusha na kuwambia mmeziba njia zote za Mafisadi Arusha na Ccm hawana tena chao kilchobaki ni kupeleka moto huo kwa Ole Medeye ni kikwazo cha demokrasia hapo. Mungu akupe maisha marefu mno Kamanda Lema na makamanda wengine.
 
Asante sana mpiganaji wewe kweli ni jembe hapo Arusha na umeonyesha upendo kwa wapiga kura wako,

Ila bana hujaweka hata mstari mmoja wa kutushukuru na sie tuliokuwa tunapiga debe tukitokea huku Nyakahanga, Geita, Buseresere, Manyovu, Godegode, etc?

Mwisho nakuomba 2015 kaweke kambi kwa kajitu fulani kamo Bungeni ni kafupi hivi kanakuwaga na maneno ya nyodo sana kakikaa pale mbele ya Bunge na nafikiri kanatokea Mpwapwa hivi
 
Back
Top Bottom