Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,605
- 1,958
Sawa hongereni sana Chadema!
Nimeliona gazeti lako, sasa msije sema kura zimeibiwa.Kwa bahati mbaya unadhani unaongea na mtoto au mtu asiyeifahamu Arusha. Naifahamu Arusha ndani nje. Ngoja nikueleze vizuri kwani unaonekana kumezwa na propaganda mfu. Arusha inategemea utalii wa wazungu na hakuna siku utalii huo uliwahi kusimama kwani hautegemei fadhila za wanasiasa wa ccm au viongozi wa serekali. Kilichopungua ni mikutano ya kiserekali tena nayo ilifanyika hivyo kwa hila ili itumike kupiga propaganda. Alipoingia Magufuli mikutano mingi ameizuia tena ni kwa nchi nzima sio kwa Arusha tu. Utalii wa wazungu umeendelea kukua Arusha tena bila jitihada za wazi za serekali, nakuambia jambo ninalolifahamu sio unayoambiwa na makada wa ccm kwa koti la serekali. Nina ushahidi wa hotel kuongezeka kwa ajili ya biashara ya utalii wa wazungu, achia mbali huo utalii mwingine hewa unaouzungumza. Ama kama unaweza leta ushahidi kwamba wazungu waliacha kuja arusha kisa kuna maandamano.
Kuhusu maandamano, hapa ndio ninapokuambia siasa chafu zilipojikita, na kwa bahati nzuri wananchi wa Arusha wanajitambua. Maandamamano yaliyowahi kufanyika Arusha wakati Lema akiwa mbunge hayajawahi kuzidi mara 3 na tena yote yalikuwa na sababu za msingi. Na maandamano haya yaliongozwa na Dr. Slaa ambaye leo hii mnamsujudia huko ccm. Maandamano ya kwanza yalikuwa kuhusu uchaguzi wa meya ambao utaratibu ulikiukwa. Maandamano ya pili ni Lema alipotoka gerezani baada ya kufungwa kwa hila enzi za JK. Tena haya hayakuwa maandamano bali ni kumsindikiza mpendwawao kwenye ofisi za cdm baada ya kushinda kesi kwa rufaa. Ili uonyeshe kwamba wewe sio mnafiki taja hayo maandamano mengi ili tuyaone hapa.
Kuhusu maendeleo, Arusha ina maendeleo muda mrefu na kwa taarifa yako baadaya Dar na Mwanza, Arusha ni ya tatu kwa maendeleo na kuchangia upande wa kodi. Na kinachofanya Arusha iwe na maendeleo ni uwepo wa wafanyabiashara wengi ambao wala hawaangalii hizo siasa zenu za majitaka. Na ushahidi kwamba wananchi wa Arusha wanajielewa na wala hawahadaiki na hizo siasa zenu chafu ni kule kushangiliwa. Wewe unaongea kile unacholishwa na wa viongozi wa ccm kupitia nafasi zao za kiserekali. Arusha ina maendeleo ya kutosha, na kinachofanywa na hao makada wa ccm ni kulitamani jimbo la Arusha, hivo wanaleta siasa za majitaka, lakini wananchi wa Arusha wanaelewa hizo ghiliba. Kwa ghiliza za hivyo mpelekee ile mikoa yenye watu wenye uelewa mdogo wanaoaminishwa kwamba mbunge analeta maendeleo. Nikushauri acha kuendekeza siasa za majitaka wakati watu tuna uelewa wa kutosha.
Na akinuna lile komwe linazidi kuchomoza...Basi Sizonje atakuwa kanuna mpaka muda huu.
Bahati nzuri leo wapiga kura wake hao unaosema wamejitambua ndiyo waliomshangilia kwa sauti kuu!! Maana yake ni kuwa bado wanamkubali sana!!! Hao watakaomwangusha hiyo2020 labda ni wale misukule muliyo ichimbia lumumba! Lema is here to stay! Kunyweni sumu!tindo bado unaishi Kwa zama za kukariri, hebu Niambie in kipi wana Arusha wanaweza jivunia mafanikio japo mawili tu toka Kwa Mbunge Lema,
Nijuavyo mimi Lema kaidumaisha Arusha toka aanze ubunge, aliifanya Arusha kuwa ya maandamano na uporaji tu, si vinginevyo .
Arusha ya kabla Yake kua Mbunge ilikua smart Sana,ulikua mji wa kitalii haswa.
Kwa sasa Arusha inarudi kwenye mstari kutokana na kazi nzuri ya RC Mrisho Gambo, hili halina ubishi hata chembe.
Nakuhakikishia Lema anakazi ya ziada kurejea bungeni 2020,Wana Arusha wamekwisha msoma vizuri Sana, kawatumia ndivyo sivyo ma charii wa AR,sasa wamejitambua, narudia muda ni Mwalimu Subiri ufike
Muda ukifika utaongeaBahati nzuri leo wapiga kura wake hao unaosema wamejitambua ndiyo waliomshangilia kwa sauti kuu!! Maana yake ni kuwa bado wanamkubali sana!!! Hao watakaomwangusha hiyo2020 labda ni wale misukule muliyo ichimbia lumumba! Lema is here to stay! Kunyweni sumu!
Inaonekana Imekuuma sana hii mkuu...Kwani hii ya kushangiliwa Kwa Lema ina Tofauti gani na kujaza watu kwenye mkutano wa hadhara wakati wa kampeni kisha waliohudhuria kutokwenda kupiga kura ?
Muda ni Mwalimu, asubiri 2020,ataona matokeo halisi ya kushangiliwa
Ongezea na hii....... baada ya lema kushangiliwa gambo akabaki anachekacheka tu hajui afanye nini......... aipoteza hadi uelekeo mwisho wa siku hajui aongee nini........ .... maneno yakamwishia akabaki anambwelambwela tu mara atake kuisifia ccm.......... mara atake kutaja mabombedia mara atake kumsifia magufuli kwa kumteua askofu kagundua hajateuliwa na jpem,....... .. yani kidogo aanze kuzomewa maana ilifika wakati haeleweki anataka kuongea nini.......
Sifa za kijinga ni pamoja na kuzindua kiwanda kinachofanya kazi kwa zaidi ya miaka kumi,ni pamoja na mwenyekiti wa ccm kudai anapambana na ufujaji wa fedha za umma huku akitumia mabilioni kununua wapinzani njaa,ni pamoja na kujifanya mpenda haki huku akiwanyima wenzake haki!CHADEMA wanaongoza katika bara la Afrika kwa sifa za kijinga
Nimeliona gazeti lako, sasa msije sema kura zimeibiwa.
Mkuu tindo kila muda unavyozidi kwenda na watu pia hawagandi, wanabadilika, Fahamu hilo, wewe tindo si yule wa miaka mitano iliopita.
Hapo nyuma mlisema siku Mbowe akilazwa ndani patachimbika, cha ajabu kalala wiki na Hakuna respond yoyote, hata siku anadhaminiwa pale kisutu sikuona Shazi, Sana Sana ni ndugu na jamaa zake wa karibu, kachokwa, kumbuka miaka miwili iliopita ingekuaje?
Watu wamechoka na usanii, nimekwambia uniambie mambo mawili tu ya msingi wana Arusha wanayoweza jivunia Kwa Lema umeshindwa
Kwa sababu wanapendwa sana!! Unaposhangiliwa tu ghafla bila hata kuongea neno lolote la kuwafurahisha watu basi ni kuwa watu hao wanakupenda kutoka mioyoni mwao!!Magufuli ni lazima atafute attention ya hadhira kwa kumwaga povu jingiiiiii!! Huku akilazimika kuchomeka na utani wa hapa na pale jumlisha ahadi na michango kemkem bila kusahau kuchomeka ujenzi wa Reli na ununuzi wa bombadia!! Tofauti na hayo magufuli hawezi pigiwa hata makofi!!Ni kwann ivi viongoz wa chadema hua wanashangiliwa sana hata kwenye dhifa/hafla zisizo rasmi au wanazoonekana wamehudhuria kwa mazabe tu, ndo wanameki headline
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wengine nawacheki afu nasema hiiiiiiiiiii....
tindo Unajua maana ya uwakilishi?, ukichagua mwakilishi mzuri wa kukusemea kuna faida zake katika muktaza wa kupata Maendeleo, kadhalika mwakilishi asie makini hushindwa kuwakilisha matatizo ya wananchi wake Kwa serikali, pamoja na serikali kuwajibika kuleta Maendeleo, pia haja ya wawakilishi makini in muhimu, Lema hayupo makini katika kuwawakilisha Wana Arusha, yupo yupo tu, mbinu atumiayo in kuwanunulia macharii shin'gwaa tu na gampera,Wewe bado una siasa za ushabiki lakini una uelewa mdogo. Nikuambie kitu, maendeleo yanaletwa na serekali na sio mbunge. Watu wenye uelewa mdogo ndio huwa wanaambiwa mbunge ndio anayeleta maendeleo. Zamani tulikuwa tukiona barabara, au miundu mbinu ya maji nk tulikuwa tunaambiwa ni mbunge kaleta. Lakini tulipojitambua tukafahamu ukweli. Kama ni huo ujinga wa kusema kwamba mbunge kaleta maendeleo basi ngoja na mimi niwe mjinga kama wewe. Wakati Lema anaingia madarakani barabara za mji zilikuwa mbovu ile mbaya. Sasa hivi barabara nyingi za mji zimejengwa kwa kiwango cha lami. Miinduo mbinu mbalimbali imeboreshwa kwa sana. Shule zimeongezeka yakiwemo na madarasa kuongezeka kwenye shule kongwe. Mambo haya zamani tuliingopewa ni mbunge analeta. Kama ndio hayo basi Lema amefanya mambo makubwa ile mbaya. Nitakupa kazi za mbunge hapo chini ili kukutoa ujinga
Hizo ndio kazi za mbunge. Na kama ni kipimo cha mbunge kufanya kazi za maendeleo yaliyo kwenye eneo lake. Basi Lema ukiachia majimbo ya Dar, na mawili ya nyamagana na Mwanza, Lema ndio mbunge bora. Usiwe mjinga kuuliza kazi za maendeleo alizofanya mbunge wakati sio jukumu lake. Na hapa ndio nakuona una uelewa mdogo wa kazi za mbunge na ndio maana unaauliza kama mtu wa kijijini. Kuna majimbo ambayo hayajawahi kuongozwa na mpinzani lakini wanamaisha duni kuliko unavyoweza kudhani.
- Muwakilishi wa wananchi wake bungeni
- Kuisimamia na kuishauri serekali
- Kutunga sheria
Au mara nyngine hata kama anaenda kanisan kama ilivokua arusha bas kamati ya siasa ya mkoa inaorganize wanaccm waende kanisan wakakae viti vya mbele kama waumin tu ilimradi wakapige makofi mkuu akianza kuongeaKwa sababu wanapendwa sana!! Unaposhangiliwa tu ghafla bila hata kuongea neno lolote la kuwafurahisha watu basi ni kuwa watu hao wanakupenda kutoka mioyoni mwao!!Magufuli ni lazima atafute attention ya hadhira kwa kumwaga povu jingiiiiii!! Huku akilazimika kuchomeka na utani wa hapa na pale jumlisha ahadi na michango kemkem bila kusahau kuchomeka ujenzi wa Reli na ununuzi wa bombadia!! Tofauti na hayo magufuli hawezi pigiwa hata makofi!!
Mukipora kwa bunduki pia nitaongea!! Mukiiba kura kwa nguvu za polisi pia tutaongea! Maana hizo ndiyo njia pekee zinazowaweka madarakani hadi sasa! Tofauti na hizo mungeshakuwa historia zilipendwa!Muda ukifika utaongea
Wale vijana wa kikurya mliowatumia 2015 mmewatelekeza magerezani bila Msaada wowote na waliwasaidia kuongeza idadi ya wabunge, na madiwani wenu Kwa kuwatisha wanaccm Kwa mapanga ili wasiende kupiga kura.Mukipora kwa bunduki pia nitaongea!! Mukiiba kura kwa nguvu za polisi pia tutaongea! Maana hizo ndiyo njia pekee zinazowaweka madarakani hadi sasa! Tofauti na hizo mungeshakuwa historia zilipendwa!
Basi Sizonje atakuwa kanuna mpaka muda huu.