Wanajamii, kwanza napenda kuyaweka haya kama kiangalizo kwa ccm wakati wana kauli mbiu maisha bora kwa kila mtanzania wakumbuke kwamba hawa watanzania si wajinga kama wanvyofikiri, wamechoka ahadi zisizotekelezeka takribani miaka hamsini, kila kukicha maisha yamezidi kuwa magumu badala ya petrol ishuke kuelekea yaliko mafuta ya taa, wao walipandisha mafuta ya taa yafuate petrol hii akili matope? Haya sukari inazalishwa hapa nchini lakini bei ni kubwa kuliko ile ya malawi,msumbiji na zambia alafu wanawakataza wafanyabiashara kuingiza sukari kwa wingi kwa kuwa wataua eti viwanda vyetu, hii ni kweli? Wataua vyetu au wataua biashara ya mafisadi walokumbatiwa na ccm? Waendelee kuwakumbatia maana majibu ya maumivu ya wananchi ni kuipiga ccm chini kifo cha mende, ccm haiwezi kuwafanya watanzania wapumbavu miaka yote, haiwezekani kamwe na kiama ndio sasa kwa ccm waandae jeneza la kujizika wenyewe.