Godbless Lema ana ulinzi wa aina gani?

Godbless Lema ana ulinzi wa aina gani?

tupak

Member
Joined
Jun 22, 2012
Posts
32
Reaction score
5
Hofu ya maisha ya watanzania wenye upinzani wa wazi na watawala ni kubwa mno hasa baada ya Dr ulimboka kufanyiwa kitu cha ajabu. Moja ya watu wanaoipinga serikali waziwazi ni Godbles Lema, je huyu kiumbe analindwaje? Au kuna siku naye tutamsikia ametekwa na baadaye kuokotwa mabwe pande au ni hisia zangu tu?
 
Wote hao na akina Zitto wana ulinzi mkubwa sana
 
Hofu ya maisha ya watanzania wenye upinzani wa wazi na watawala ni kubwa mno hasa baada ya Dr ulimboka kufanyiwa kitu cha ajabu. Moja ya watu wanaoipinga serikali waziwazi ni Godbles Lema, je huyu kiumbe analindwaje? Au kuna siku naye tutamsikia ametekwa na baadaye kuokotwa mabwe pande au ni hisia zangu tu?

Mkuu.kwa hali ilivyo sasa yenyewe..si vigumu kusikia mkuu wa kaya amepelekwa "kingdom come" wakati akiwasili toka Rwanda..sembuse huyo Hemed msangi ambaye watu wanamtafutia pozi tu..ninachosema ni kuwa kama hawa vilaza wana hamu ya kuona watanzania si waoga,basi wafanye kitu kingine cha kipumbavu namna ile..kama ilivyo kwa ulimboka,watanzania wengi wanasubiri wanataka kuonyeshwa njia..tofauti tu ni kuwa njia watakayooneshwa baada ya mtu kama lema kuuawa itakuwa sio laini na ya amani sana..ila itawafikisha pahala pema zaidi watanzania.
 
Kufa ni lazima kwa kila mwanadam, ikiwa kufa kutatokana na vita dhidi ya uonevu wa wengine utakuwa umekufa kishujaa.
 
Hofu ya maisha ya watanzania wenye upinzani wa wazi na watawala ni kubwa mno hasa baada ya Dr ulimboka kufanyiwa kitu cha ajabu. Moja ya watu wanaoipinga serikali waziwazi ni Godbles Lema, je huyu kiumbe analindwaje? Au kuna siku naye tutamsikia ametekwa na baadaye kuokotwa mabwe pande au ni hisia zangu tu?

Watamdhuru vipi Lema wakati muda wote yupo na Wazee 24
 
Lema ana ulinzi mkubwa, kama vp akwaruzwe waone moto.
 
Kabla ya kulindwa na binadamu tayari alikwishayatoa maisha yake kwa ajili ya haki za wanyonge.Yule jamaa anaipenda sana Tanzania na watu wake.Hata Magamba wangekuwa na mtu mmoja kama Lema serikali isingeyumba kwa kiwango kama tunachoshuhudia.
 
Lema ni nani kwenye nchi hii hadi awindwe?
 
Wao wenyewe wanajua madhara kufanya chochote dhidi ya lema manake ni lazima tupigane nao hao magamba wote.
 
Sisi tuna Mungu, wao wana fedha.
Lema kwenye mikutano yake amekuwa akieleza hadi njia ya kufika nyumbani kwa wale wenye nia ya kumdhuru...lakini yuko salama salimini. Mtu atakayekuwa na ndoto za kumuua Lema hajazaliwa bado.
 
Dhambi kubwa kuliko zote ni woga, acha woga usipokufa leo, utakufa kesho usipokufa kesho utakufa siku 1 ambayo huijui kwa hiyo ni Heri vita inayotafuta haki na usawa duniani kuliko amani inayopumbaza na kuudhalilisha utu wa mwanadamu.
 
wajaribu ya mwakyembe, wote itabidi wahame nchi maisha yao yote pamoja na uzao wao.
 
Aache kuuliwa dr slaa au zitto kabwe ambao ndo majembe ya chadema...aje auliwe lema,kwa kipi alicho nacho sasa?yeye aendelee kudhurura tu na kubwabwaja maneno ovyo,hakuna mwenye shida nae wala!
 
Hofu ya maisha ya watanzania wenye upinzani wa wazi na watawala ni kubwa mno hasa baada ya Dr ulimboka kufanyiwa kitu cha ajabu. Moja ya watu wanaoipinga serikali waziwazi ni Godbles Lema, je huyu kiumbe analindwaje? Au kuna siku naye tutamsikia ametekwa na baadaye kuokotwa mabwe pande au ni hisia zangu tu?

ana ulinzi mkubwa sana kuliko unavyofikiria, fata kauli yake
TUNAANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU, JE NI NANI ALIYEMKUU ZAIDI YA MUNGU?
 
Lema ni nani kwenye nchi hii hadi awindwe?

Acha kutoa mapofu yote hii!

Lema ni yule Mkuu wako unayemhanya!
Unajifanya umepoteza kumbukumbu eeee! Pole sana!

MKAMANDA wana ulinzi masaa yote tangu alipotangaza vita serikali DHAIFU!
 
Back
Top Bottom