Goba vs Kigamboni: Wapi ni pazuri zaidi?

Kigamboni pazuri kwa wanaofikiria miaka kadhaa mbele, itakuwa eneo Bora sana miaka ijayo, pia daraja litakapokuwa free, patavuta watu zaidi, ni sehemu ambayo imepangwa.

Changamoto yake ni ufinyu wa barabara za lami, pia usafiri wa umma(daladala, bado haujakaa vizuri, zinafunga kazi mapema halafu ghali
 
Goba kubwa, kuna mtaa unaitwa muungano, yupo jamaa amegawa shamba lake 30x30 unapata, pesa uwe nayo. Ni pm kwa maelezo zaidi. Kama huyajui maeneo hayo, neñda ka-sarvey kwanza. We uliza serikali ya mtaa wa muungano Goba ipo wapi. Nenda maeneo yale. Ukipenda sasa ni mp kwa maelezo zaidi. Umeme upo, mabomba ya maji Dawasco yapo mita chache kutoka site.
Tudokeze bei basi ya 30*30
 
I'm in love with Kigamboni, ukiwa kigamboni unaweza ku access mahali kokote kwa urahisi mno..Mfano ukivuka tu ferry unakutana na kituo kikuubwa kabisaa cha mwendokasi (Center)...
Pili, zile beaches Kigamboni daah,kigamboni kutamu balaa...
 
Msaada wa kimawazo

Hivi kati ya Goba na Kigamboni, wapi pazuri kujenga na kuishi.

Naomba ushauri wapi kuna maeneo mazuri.

1. Bei za viwanja
2. Huduma za kijamii
3. Usalama
4. Wapi ni potential
5. Na mengineyo

Utofauti upoje ndo nataka kujua, buget ya plot sio issue sana
..
Natanguliza shukrani
Unalinganisha Goba na kigamboni? Kigamboni hii isingekuwepo bahari ingekuwa ni sehemu ya mtaa wa posta
 
Mmmh hapo goba kukatiza makongo juu wee....kipande kirefu hataree mpaka uifikie survey ni umechoka na bado hapo hujakutana na jam

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Kama mtu unaishi goba tena ya uswazi halaf unafanya kazi/shughuli zako posta aisee ni kipengele ila let say unaishi mji mwema au kibugumo kigamboni then ofisi posta dah utaenjoy mpak basi
 
Bagamoyo Road ndo barabara ya kishua DSM nzima ( pande zote mbili ) , inafatia angalau morogoro road , kigamboni plus kilwa road uswahili mtupu , kigamboni inabebwa na makaz mapya sa hv Ila ni uswahili mtupu na vijana wamejaa kule full vibaka ...alaf ni aibu tuu kulinganisha Goba na kigamboni ... Goba huwez ishi kama shekeli za kuunga unga .... Kuna mama ntuilie wachache Sana Goba , kigamboni wapika uono wamejaa kule na inanuka shombo la samaki , although kuna upepo mwanana, kigamboni unapata msosi mboga Saba Kwa 1500 hatari Sana
 
Msaada wa kimawazo

Hivi kati ya Goba na Kigamboni, wapi pazuri kujenga na kuishi.

Naomba ushauri wapi kuna maeneo mazuri.

1. Bei za viwanja
2. Huduma za kijamii
3. Usalama
4. Wapi ni potential
5. Na mengineyo

Utofauti upoje ndo nataka kujua, buget ya plot sio issue sana
..
Natanguliza shukrani
Humu watu wengi ni wakazi wa Goba

Sisemi sana
 
Back
Top Bottom