Goal-LINE TECHNOLOGY,je inahitajika kwenye soka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Goal-LINE TECHNOLOGY,je inahitajika kwenye soka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bajabiri, Jul 5, 2012.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wadau,fifa wapo kwenye mchakato wa kuleta utaratibu mpya wa kukubali goli kwa teknolojia ili kuondoa utata kama mpira umetinga wavuni au lah,,,,na mfano ni wakati wa mashindano ya EURO ambapo terry aliokoa,,,,mpira ambao inasemekana ulitinga wavun,
  Je goal-line technology ni nzuri???maana kwakweli itaondoa utata,ila pia ile hali ya ubishi miongon mwa washabiki itaondoka,,,,,ila vilevile hii technology itaendana na hali yetu waafrika????
  tujadiliane wadau
   
 2. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Naungana na Rais wa UEFA Michael Platin ambaye anachelea kukubali goal technology. Kuna mambo mengi mno ambayo marefa wanashindwa kuyabaini kama binadamu likiwemo hilo la kama mpira umevuka mstari au la. Lakini kuna mambo mengine kama ni onside au offside, ameshika au, amekwatuliwa au n.k. Mpira wa miguu utagawanyika maana achilia mbali technology hiyo kuweza kutumika katika ligi ya tanzania, je huko Ulemo au Ikungwipina watafanyaje
   
 3. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Mpira utapoteza ladha, utakuwa kama gemu sasa. Walijaribu kumweka refa nyuma ya goli lakini hakuna unafuu, penati bado ni za magumashi na magoli yanakataliwa.
  Siungani na Platini katika majaribio yake ya kuua soka.
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  @Mpha
  ila ladha ya soka itashuka bhana,,,,,mpira raha yake ni ubishi
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ila ladha ya soka inaelekea wapi?????
   
 6. fmlyimo

  fmlyimo JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Mashabiki wa soka wana asili ya ubishi. Hata wakileta hiyo mitambo wataendelea kubisha tu, watasema imechakachuliwa. Wengine watasema mitambo ya kichina inapendelea timu fulani. Ubishi hautaisha ila utaongezeka. Mashabiki noma, huwa wanaobishana mpaka na redio au Tv.
   
 7. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe, controvesial za soka ndo zinaufanya uwe mchezo wenye ladha kuliko mwingine.
  FIFA wanaua sasa, na leo wamepitisha hiyo technology na marefa watano kwenye game. Chefuuu...
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  It's been long overdue.
   
 9. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu maneno yako aliwahi kuyasema Arsene Wenger zaidi ya miaka kumi iliyopita. Nakumbuka alisema 'Technology isiwepo katika mpira,kwa sababu itaondoa ubishi, na ubishi ukiondoka football itakufa"Iitapoteza mashamsham"
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Lakini pia teknolojia hii na uhalisia wa afrika vinaendana wadau?????maana kwa sasa kule ulaya marefa wanaweza kuwasiliana,,,,,wakiwa wanachezesha,sisi hap hatujafikia,kisha hata vile vibao vya kubadilishia wachezaji wanatumia vya electronic sisi bado,je ni kweli kwamba waafrika tutakua tunaenda sambamba na fifa au ni kujipotezea muda na soka letu,,,,let say uwanjja kama wa ILULU kule lindi je wanaweza kuitumia hii teknolojia????ikiwa hata taa za uwanjan hakuna????
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Fifa wamesha prove goal line technology, and this is what we have been waiting to be implemented
   
 12. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ladha ya soka itapotea. Ndo maana nimesema naungana na Platin ambaye anapinga mfumo. Yeye anaona bora utaratibu wa marefa 5 uimarishwe
   
Loading...