GLASI ya BIBI...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mchezombaya alitembea kuelekea mahali fulani.Njiani akahisi kiu kali.Akaingia nyumba moja kuomba maji ya kunywa.Wenyeji wakamtuma mtoto mmoja wa miaka kumi hivi amhudumie.Jamaa akamwagiza mtoto maji.Punde mtoto akamletea maziwa.Akanywa.Akamwomba amwongeze maji au maziwa.

Mtoto akaleta tena maziwa.Baada ya kunywa tena,Mchezombaya akamuuliza mtoto:Kwanini nilipoomba maji ukaniletea maziwa? Mtoto akajibu: Humo kwenye maziwa alifia panya kwahiyo kia mtu hapa nyumbani aliyasusa kuyanywa.Mchezombaya akashtuka hadi glasi ikamponyoka na kuanguka chini.Ikapasuka vipandevipande.Mtoto akakimbilia walipo Ndugu zake wengine huku akisema: Mama,huyu mgeni ameivunja glasi ya bibi ya kutemea mate! Mchezombaya akazimia...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom