Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 17,739
- 11,979
Ndugu zangu Watanzania,
Waziri wa Fedha Mheshimiwa Daktari Mwingulu Lameck Nchemba Amewataka Waheshimiwa Wabunge pamoja na watanzania wote kujenga utamaduni wa kujadili sheria wakati wa mchakato wa Utungwaji wake na siyo wakati wa utekelezaji wake.
Ameyasema hayo kutokana na swali lililoulizwa na Mbunge wa Mbozi Mheshimiwa George Ranwell Mwenisongole aliyetaka kujuwa na kufahamu ni kwanini vyama vya ushirika vinalazimishwa na TRA kununua na kuwa na mashine ya EFD wakati havifanyi biashara na huuza mara moja tu kwa mwaka.
Akijibu swali hilo Mheshimiwa Dkt Mwigulu amesema kuwa Ukusanyaji wa kodi unafanyika kwa mujibu wa sheria namba 36(1) ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015. ambapo ni lazima mfanyabiashara anayesambaza bidhaa au kutoa huduma au kupokea malipo kutokana na malipo ya huduma aliyotoa anatakiwa kutoa risiti za kieletroniki.
Lakini pia amesema ya kuwa sheria inasema kuwa mfanyabiashara yeyote anayefanya mauzo ghafi ya millioni 11 na kuendelea kwa Mwaka anapaswa kuwa na mashine ya kielektroniki EFD. Ameendelea kusema ya kuwa lengo ni kuhamasisha utunzaji wa kumbukumbu ambapo EFD ni njia nzuri na rahisi yenye ufanisi mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu kwa mfanyabiashara.
Amesema pia kuwa haiwezekani mwalimu wa shule ya msingi atozwe kodi halafu aende aachwe tajiri.au mtu mwenye kipato cha chini cha mauzo chini ya Millioni 3 kwa mwaka atozwe na kulipishwa kodi halafu aende aachwe anayepokea malipo ya millioni Mia Moja.Amesema hii haiwezekani na siyo haki. Na kwamba mwezi ujao bunge litajadili pia masuala ya Kodi ,hivyo kama kuna sheria wabunge wanaona haifai basi ndio wakati wa kuijadili ili kuangalia kama itolewe au kufutwa au kufanyiwa marekebisho.
Mimi Mwashambwa Lucas ningependa kusema ya kuwa Waheshimiwa wabunge wetu wawe na utaratibu mzuri wa kujisomea,kutafiti,kuomba ushauri na kusikiliza wananchi wanasema nini wakati wanapokuwa wanajadili na kupitisha sheria fulani Bungeni itakayotumika kwa wanachi na Taifa kwa ujumla wake.
Nasema hili kwa kuwa imekuwa inasikitisha sana ,kuleta aibu , kufedhehesha,kuonyesha kukosa umakini na kutoelewa kwa undani kile wanachokipitisha ndani ya Bunge. kwa sababu ni kawaida unakuta sheria fulani inapita kwa kishindo na kwa kura zote za ndio, halafu baada ya muda wananchi wakianza kulalamika na kukosoa sheria husika mitaani unaona kuna wabunge wanaanza kushangaa kana kwamba ni kitu kigeni masikioni mwao na wala hawajawa kukisikia wala kushiriki katika mjadala wake wala kuunga mkono.
Jambo linaloonyesha aidha waheshimiwa wabunge wanakuwa wakati mwingine hawajapitia vifungu vyote na makabrasha yote yaliyo mezani pao kujuwa maana ya kile wanacho kipitisha na kukiunga mkono. Wakati mwingine mpaka unajiuliza inakuwaje mwananchi wa kawaida aone kwa haraka na ndani ya muda mfupi tatizo la sheria fulani ,halafu Mbunge anayekaa bungeni na kulipwa posho kwa ajili ya kazi hiyo ashindwe kuona tatizo hilo mpaka anapokuja kuona wananchi wakilalamika na kukosoa kwa nguvu na ndipo sasa naye Mbunge aanze kulaumu na kulalamika kana kwamba hakuwepo wakati wa utungaji na upitishwaji wake?
Tatizo nini nini? Shida inakuwa wapi? Kwanini hili linatokea kwa sheria inatungwa leo halafu kesho inakuwa inahitaji mabadiliko na marekebisho? Ni wapi panakosekana umakini? Ni nani hatekelezi wajibu wake? Je, waheshimiwa huwa wanapigia makofi na kuunga mkono mambo wasiyo yajua? Nini kifanyike hali hii isiwe inatokea? Kwa sababu tumeona jambo hili katika suala la kikokotoo ambapo wabunge wakiwa wakali kana kwamba siyo wao waiopitisha na wala hawajawahi kushiriki katika mjadala wa aina yoyote ile unaohusu kikokotoo.
Naweka kalamu yangu chini na kuishia hapa, sitaki kuwachosheni. Lakini tujiulize pia kwanini walipa kodi Tanzania ni wachache sana kuliko idadi ya watu wanaostahili kulipa kodi? Kwanini watanzania hawapendi kulipa kodi na hutafuta njia za kukwepa kulipa kodi kuliko kwenda kulipa kwa hiyari? Je ni kutokutambua umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya Taifa letu? Je, ni kutokujua kuwa nchi inaendeshwa kwa kodi na kila kitu tunachotaka kufanyiwa na serikali yetu kinatokana na kodi zetu, ambazo tunatakiwa tuone fahari kulipa badala ya kuwa wakwanza kutengeneza mifumo ya Ukwepaji kodi.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.