Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,871
- 155,841
Jamaa yangu Mwinsheikh Mwinyihaji Omary amepata msichana wa Kichina anayemiliki duka la kuuza maua kariakoo.
Mchina wa Mwinsheikh hajui kabisa Kiingerza ila Kiswahili anajitahidi kidogo.
Kila siku wakitoka kwenye duka lao la maua wanaenda kwenye migahawa ya Kichina, huko huyo binti hujumuika na Wachina wenzake, wanaongea kichina mwazo mpaka mwisho huku wakimuacha jamaa yangu anatumbua macho kama amenusurika kupigwa na bomu la mbagala.
Jana jamaa akawa amaechoshwa na tabia hiyo sugu ya msichana wake, akamwambia demu wake kuwa anataka kumpeleka kwenye migahawa ya Kitanzania.
Tukakutana pale Kijiji cha Makumbusho, tukawa tunapiga zetu story. Binti wa Kichina akaona maji yamezidi unga akamwambia bwana ke "turudi kwa wachina wenzangu na mimi nikaongee"
Jamaa akamwambia ulivyojisikia wewe ndivyo ninavyojisikia mimi tukiwa na wachina wenzako"
Wito wangu kwenu wana mapenzi:-
Mwenzio akikukwaza mweleze, wala usiweke moyoni wala usipange kumrudishia kisasi.