Ghorofa limenifanya nikosane na marafiki pamoja na wakwe zangu

ImageUploadedByJamiiForums1425027959.538444.jpg
One day YES kama wakishua vile
 
Last edited by a moderator:
Hongera yako ila hii jeuri acha kabisa, inaonekana unakajeuri jeuri hivi na inaweza kuwa ndio sababu ya hayo yote.

"kimya cha mpumbavu ......, na kelele za mwenye busara......!" jifunze kuwa silence, japo sina uhakika sana nahisi

umepiga picha gorofa barabarani na kulileta huku.
 
Ukiwa katikati ya familia duni ni lazima wakushangae,
vinginevyo hayo majumba mbona ni mengi tu miaka hii.
 
hivi uki kaa kimya kwani inaubaya gani mbona hayo ni maisha tu ikifa unaviacha watu wanagombania fito na vagae so thanks God achana na kujionyesha
 
Mara oooh!najenga ghorofa kinyerezi baba askofu aje azindue leo segerea hii si kachumbali flava sasa
 
Kijana orofa moja tu slab moja! tu umekuja kutupigia kelele mpaka hatulali! dah maskini akiokota matako hulia mbwata mbwata! All in all nakupa big up vijana wengi wa kibongo kufika hapo ulipofikia ni ndoto, alafu umetupa taarifa kupitia mlango wa nyuma.
 
Ama kweli nimeamini watanzania hatupendi kuona mtu akipiga hatua moja kwenda nyingine, tofauti na wenzetu hawa ngozi nyeupe ambao wao kupigana tafu ni mambo ya kawaida sana katika life cycle yao.

Nimeamua kuweka picha ya ghorofa langu ambalo lipo katika hatua za mwisho mwisho za ujenzi ili muweze kupata picha kamili ya hiki ninachokwenda kukisema.

kama mnavyoona ujenzi ndio unaendelea japokuwa umenigharimu kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho ningeweza kununua hata semi za mchanga na mabasi ya mikoani.

Twende katika pointi baadhi ya marafiki na masheji zangu ambao nimewahi kuwapeleka katika site yangu naona kuna tofauti kubwa na hapo mwanzo.

Kwanza kabisa ukaribu umepungua hata vile vikao vya bia na kutoka pamoja kila siku za mwisho wa wiki naona kwishinea na nikijaribu kuwapigia na kuwauliza naona wanajiumauma wakikosa la kusema.

Nasubutu kusema kwamba wameingiwa na roho flani hivi ya wivu wa kimaendeleo,nikaona sio kesi nikamshirkisha na mke wangu kuhusu hili swala nae akasema mapokeo ni kama yangu.

Ni hayo tuu kwa leo nikaona kukaa kimya sio solution ni bora nikatoa dukuduku langu la moyo hata kama hao niliowasema kama wakipata nafasi ya kupitia huu uzi wajue kwamba nimewadharau kwa kiwango cha juu mnoo.

Usiku mwema wanajamvi wenzangu.

H aha ha ha ..naomba nichangie hivi kwanza....

  • Hili Ghorofa ni makazi yanaojengwa na serikali kwa ajili ya Makazi Ya RAS mkoa wa Iringa,,Jengo nalifahamu liko Gangilonga juu kutoka MSD kama unaoenda Ikulu Ndogo ya Iringa,,,,nitafuatilia na kutuma picha...nikishaakikisha.
  • Pili kama ni katika suala la maendeleo na marafiki uwaoni katika vikao vya bia....hiii labda kweli ni wivu wa maendeleo lakin mengi yanasababishwa na wausika wenyewe,,,unaakuta marafiki zako wanakubeba kila siku wanakupa offer tu ya beer nyama choma ww uchangii wanakuchulia poa alafu siku ya siku unawaonyesha maendeleo yako hata mimi nakukwepa faster....ufai wewe ni parasite mbaya, mfano ofisi moja walikuwa na mwenzao..yeye kila siku kuomba vocha, naomba niamishie 250, au 300 kwa staff wenzake, naomba offer ya chapat ya maandazi kwa chai...Lunch anavuta...na wenzake wanampa kirafiki,,heee siku ya baada ya mwaka duh kaingiza gari mpya......watu wote pale ofisn walifadhahika baada ya kufurai..hakuna aliekuwa anampa hata vocha......kwisheney...............
 
Ama kweli nimeamini watanzania hatupendi kuona mtu akipiga hatua moja kwenda nyingine, tofauti na wenzetu hawa ngozi nyeupe ambao wao kupigana tafu ni mambo ya kawaida sana katika life cycle yao.

Nimeamua kuweka picha ya ghorofa langu ambalo lipo katika hatua za mwisho mwisho za ujenzi ili muweze kupata picha kamili ya hiki ninachokwenda kukisema.

kama mnavyoona ujenzi ndio unaendelea japokuwa umenigharimu kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho ningeweza kununua hata semi za mchanga na mabasi ya mikoani.

Twende katika pointi baadhi ya marafiki na masheji zangu ambao nimewahi kuwapeleka katika site yangu naona kuna tofauti kubwa na hapo mwanzo.

Kwanza kabisa ukaribu umepungua hata vile vikao vya bia na kutoka pamoja kila siku za mwisho wa wiki naona kwishinea na nikijaribu kuwapigia na kuwauliza naona wanajiumauma wakikosa la kusema.

Nasubutu kusema kwamba wameingiwa na roho flani hivi ya wivu wa kimaendeleo,nikaona sio kesi nikamshirkisha na mke wangu kuhusu hili swala nae akasema mapokeo ni kama yangu.

Ni hayo tuu kwa leo nikaona kukaa kimya sio solution ni bora nikatoa dukuduku langu la moyo hata kama hao niliowasema kama wakipata nafasi ya kupitia huu uzi wajue kwamba nimewadharau kwa kiwango cha juu mnoo.

Usiku mwema wanajamvi wenzangu.

Kumbe mkuu ndo wamiliki hiki kitu cha Kinyerezi, Hongera asee
 
Naona heshima imepungua unaonaje ukiuza hiyo ghorofa ukajenge heshima bar? After all waoga wa maisha ndio wanahangaika na kujenga majumba makuuuubwa kama hilo ghorofa.
 
Back
Top Bottom