Nondo kwaajili ya ghorofa ya makazi

Limbu Nation

Member
Apr 18, 2024
15
5
Katika ujenzi hasa wa majengo marefu (maghorofa) matumizi ya nondo ni jambo lisilo epukika.

Baada ya kupata michoro kutoka kwa msanifu majengo (Archtect) michoro hiyo haina budi kupelekwa kwa structure Engineer ili iweze kufanyiwa hesabu.

Lengo la kufanya hesabu ni kujua ni nondo za aina gani zitafaa katika ujenzi huo na pia nondo hizo ziwekwe kwa namna gani na kwenye eneo gani. Na pia kujua ukubwa wa element za jengo (mfano unene wa slab, ukubwa wa nguzo, unene wa nguzo n.k) na pia kujua ni zege la aina gani litatumika (mfano, concrete class 15, 20, 25 au 30) na mambo mengine mengi.

Si ajabu kuona beam ikiwa na nondo za 16mm, 20mm na 25mm, au kuona element zikitumia zege la aina tofauti (mfano C20 na C25).

Hii hutuambia na kutupa picha kuwa aina ya nondo hutegemea sana matumizi ya jengo na uzito wa jengo husika.

Ila kwa kawaida imezoeleka kutumia nondo za 16mm au 20mm kwenye nguzo, 12mm au 10mm kwenye slab na 8mm kwenye ngazi.

NB: Kusema tu hili ni jengo/ghorofa kwaajili ya makazi haitoshi tu kuamua aina ya nondo, ni lazima kuuona mchoro, kuiona site na kujua aina ya udongo ambapo jengo hujengwa.

Mwisho, ni muhimu sana kutumia wataalam katika hatua zako zote za ujenzi ili kuokoa gharama na kuongeza kiwango cha ubora wa nyumba yako.

Niulize kuhusu ujenzi kupitia 0621003092 nami nitakusaida bure kabisa b’se im you’re fellow Tanzanian.
 
Mkuu, fanya ujitangaze kupitia EATV kwenye kipindi cha ujenzi. Wenye nia ya kujenga wanapenda sana kuona uhalisia wa kazi ukiwa site.
 
Back
Top Bottom