Neno linasema heri anayesikia bila kuona na kuamini.Weka picha acha ukilaza wa kusikia sikia!
Kutitia sio kubonyea mkuu.Labda kata sikulaumu.Kutitia ni kuingia chini ardhini bila kubomoka!Yaani nzima nzima hiyooo inapotea ardhini.Nimeangalia ushahidi wa hili katika nyuzi zote sikuona.Mleta uzi alete kitu chenye akili.Mpaka sasa hakuna kinachoeleweka.
Mkuu, ujuavyo kuzama ni mpaka pawepo bahari, St. Kayumba inaonekana.acha uongo..linazama kwani kariakoo kuna bahari?
Asiporudi ndio utajua ni ukweli! Kwa nini usimtume njiwa?mmh.., ngoja nimtume mtu akaangalie kama kweli..
Bado kidogo, kunamtu anangojewa atoke ndio lianguke.Limeshaanguka tayari?
Kutitia maana yake ni kurudi udogoHapa kweli kuna haja ya watu kurudia somo la LUGHA YETU. Kwamba kutitia ni neno lisilo eleweka haiingii kwenye akili yangu ndogo.
Hata hivyo, nikubaliane na waliofananisha kutitia na kuzama, vinaendana kwani kuzama si lazima iwe majini.
Pia nitahadharishe kwamba jengo linaweza kutitia lote yaani pande zote za jengo zikaingia ardhini, au sehemu ya jengo ndiyo inaweza kutitia.
Iwapo jengo linatitia upande mmoja dalili zake ni nyufa zinazoongezeka, jengo kuegama (kulala) upande mmoja (au kuonekana limepinda) na kama litaendelea basi litaishia kuanguka/kuvunjika/kuporomoka.
Ieleweke kwamba majengo yote, barabara, madaraja na mabwawa yanayojengwa popote duniani huwa yanatitia na Wahandisi huwa wanaelewa kwamba, baada ya ujenzi, kiwango cha kutitia KINACHORUHUSIWA/KILICHO SALAMA kitakuwa ni kiasi gani. Katika hili mnaweza kukagua nyumba mnazoishi kama zina nyufa au ziliwahi kupata ufa/nyufa, na hata barabara na mabwawa huwa yana nyufa, ambazo ni dalili za kutitia.
Kudidimia ndio neno sawaKutitia maana yake ni kurudi udogo
ni wapi duniani umewahi kuona jengo limepotea ardhini?Kutitia ni....Yaani nzima nzima hiyooo inapotea ardhini.
ni wapi duniani umewahi kuona jengo limetitia lote?jengo linaweza kutitia lote
Mkuu kutititia ni kubonyea!
Naona kama Unakosea mwenyewe na kujisahihisha mwenyewe.Ulivyoongezea kwa kwenda chini umekaribia maana, manake ukisema tu kubonyea haileti maana, mfano gari inaweza kuwa imebinyea bila kutitia.
Kutitia inaendana na ardhi mkuu.
Naona kama Unakosea mwenyewe na kujisahihisha mwenyewe.
I like JF
Poa Poa Mkuu wangu.Siyo hivyo mkuu, sentensi ya kwanza nilim-quote kwa msahngao jamaa aliyesema kutitia ni kubonyea, baadaye akaongeza nyama kwamba ni kubonyea kwa kwenda chini ndo hiyo post ya pili ilipokuja, nikimaanisha sasa tunaanza kuelewana.
Ungefuatilia kidogo tu ungeelewa!
Mtanzania gani hajui maana ya kutitia, kutitia ni kitendo cha kitu kilichopo juu ya ardhi, kuzama ardhini kiasi yaani sio chote. Na hata ikitokea kimezama chote maelezo huwa kilititia na kuzama, ila kikizama kiasi huitwa kimetitia, nadhani nimeeleweka, ila napenda asome aliekuuliza maana ya kutitia. Kama mswahili atueleze kwao hiki kitendo wanakiitaje...mkuu kutititia mie sijui maana yake mi najua kutitia ndio kubonyea kwa kwenda chini
Kuchikichia ni kuiba kwa kuficha, haihusiani na kudidimia, kutitia, kuzama, kubonyea kwa kwenda chiniKutitia ni kitendo cha kuchikichia.
Acha uongo wewe kwa hiyo Nyoka akiingia mzima mzima shimoni utasema ametitiaKutitia sio kubonyea mkuu.Labda kata sikulaumu.Kutitia ni kuingia chini ardhini bila kubomoka!Yaani nzima nzima hiyooo inapotea ardhini.Nimeangalia ushahidi wa hili katika nyuzi zote sikuona.Mleta uzi alete kitu chenye akili.Mpaka sasa hakuna kinachoeleweka.
Kutitia ni "Kuzama mchangani huku likiwa wima"kutitia ndio inamaanisha nini?