Ghasia aagiza Fataki huyu abanwe mbavu.................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ghasia aagiza Fataki huyu abanwe mbavu....................

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rutashubanyuma, Dec 27, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Ghasia aagiza anayeambukiza Ukimwi abanwe


  Na Martha Fataely, Moshi

  MWENYEKITI wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya taifa ya takwimu ameagizwa kumchukulia hatua za kisheria mtumishi mmoja ambaye anadaiwa kuwaambukiza Ukimwi kwa makusudi watumishi wa taasisi hiyo. Waziri wa Nchi, Ofisi ya
  Rais, Menejment ya Utumishi, Bi. Hawa Ghasia alitoa agizo hilo katika ufunguzi wa kikao cha tatu cha wafanyakazi wa ofisi ya takwimu ya taifa ikiwa ni baada ya kupata taarifa za mtumishi huyo. Kutokana na malalamiko ya watumishi wengi na ukweli wa mambo yenyewe, namuachia mwenyekiti wa baraza wenu alishughulikie haraka iwezekanavyo ili kunusuru nguvu kazi ya taifa isiendelee kuteketea na ili iwe fundisho kwa wengine,� alisema.

  Waziri Ghasia alisema amepokea malalamiko mengi juu ya tabia mbaya za mtumishi huyo ambaye inasemekana kutokana na uwezo wa kifedha alionao amekuwa akiwarubuni wasichana wafanye naye mapenzi huku akijua ni muathirika.
  Hii sio tabia ya kiungwana lakini kwa kuwa kuna sheria za nchi ambazo zinaelekeza cha kufanya kwa watu kama hawa, hakuna haja ya kumfumbia macho, kwani huu ni mchezo mbaya,� alisema.

  Alisema ni vyema kwa mwenyekiti huyo Dkt. Albina Chuwa kutomuonea haya mtumishi huyo kwa kuwa taifa litaendelea kupoteza nguvu kazi na wazazi wametumia fedha nyingi kuwaelimisha watoto wao.

  [​IMG]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Easier said than done.............ushahidi kuupata ndiyo noma inapoanzia...............................

  Inabidi uthibitishe ya kuwa hao waathirika kweli walipata vvu kutoka kwa mshukiwa wa fataki....................kuthibitisha ya kuwa ni kweli alitembea nao.......hapo unahitaji shahawa zake zikutwe kwenye uke zao....................na zipimwe zionekane zina vvu na watuhumu wao hawana vvu hivyo kuthibitisha mtuhumiwa wa fataki kweli ana nia ya kuwaambukiza wahusika...............

  kuthibitisha nia ya kuwaambukiza watuhumu nayo ni mtihani mwingine.............................inabidi uthibitishe ya kuwa anaijua hali yake ya kiafya.....kwa maana alishawahi kupimwa na kuonekana ana vvu.kama hajawahi kupimwa inamaanisha ya kuwa hajijui afya yake na hivyo hawezi kupatikana na hatia ya kuambukiza wengine kwa kukusudia................................

  Hivi haya Mheshimiwa Ghasia anayajua au ni mwepesi wa kusukumia majukumu mazito hao wengineo.....ambao wamemlalamikia.............
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwanini hajamtaja kama anamjua? liyumba si yuko jela au kuna mwingine?
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Wanajua athari za kisheria ambazo zinaweza kuwakumba ukizingatia wanafanyia kazi majungu ya mitaani na hayajathibitishwa na madaktari................waathirika hao utawakuta nao ni njiwa tu na hawashikiki sasa wanamtafuta wakumlaumu tu......................
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kuna haja ya kurudi na mambo ya mze punch hadi maofisini sasa

  huyo jamaa atajwe bana
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Yaweza kusaidia.........ingawaje tangia watu wamegundua mahakama na msamiati wa kuchafuliwa jina...................basi ipo kazi katika kuwashughulikia hapo.............
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ruta:

  Kiutaalamu hiyo ni easy kesi. Virus wa HIV wana DNA markers. Hivyo ni rahisi kutambua ni nani ameambukiza.
   
Loading...