Gharama za Kuingiza gari TZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama za Kuingiza gari TZ

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kamarada, Feb 2, 2011.

 1. K

  Kamarada Senior Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  :bump: Salaam kwenu waungwana wote!

  Nafikiria kununua Ki-gari to JPN in Apr 2011,
  Plz naomba kufahamishwa gharama nitakazo paswa kuzilipa hadi linakuwa kwa barabara, bila gharama ya kununua na kusafirisha to Dsm Port! ie. gharama za bandari, VAT, TRA, nk.

  If ombi kama hili limewahi kujadiliwa, plz naombo muongozo wa kufika huko.

  Nawasilisha!
   
 2. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Swali halija kamilika, hako ka gari ni ka mwaka gani? Na kana CC Ukubwa gani?na umekanunua bei gani? Kana inspection ya JAAAI? (Kama hakana uende TBS Ubungo na $800)na umelipia pesa ngapi za kusafirisha yani freight to DSM/TANGA/ZNZ ukituma majibu haya utaweza kupata muelekeo wa watakavyo kukufisadi hapa TRA,TISCN NA TPA Usisahau kuna ku up lift na OTHERS CHARGE
   
 3. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwa kawaida ulipa gharama hizi

  Vat ni 18%
  CC ni 10%
  Uchakavu ( gari lililozidi miaka 10) ni 20%
  import duty ni 25%
  registration ni Tshs 308,000 (sijui kama zimepanda)
  za bandarini ni dola 10 kwa siku baada ya wiki 1 gari lilipofika (sijui kama zimeongezeka).

  SASA HIYO % NI ACCUMULATIVE YA KILA KODI KUTOKA KWA CIF


  e.g, jumla ya gharama zote za ununuzi wa gari kutoka Japan hadi Bandari ya DSM (au yoyote) ni $ 5000

  TRA wanaanza


  Import duty (20%) = $5000x20/100 = $1000

  CC (10%) = $500 +Vat($1000)=$6000, $6000x10/100 = $600

  Vat (18%) = $6000+ CC($600) = $6600, $6600x18/100= .....

  Nakuendelea, kwa hiyo ukiagiza gari kwa $ 5000 hakikisha una 75% ya kulipia kodi la siyo utoe mlungula na wajanja wa TRA
   
 4. K

  Kamarada Senior Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  JF ni Saikolopidia bana du :msela:, You've covered my need, nakushukuru sana ndg yangu.
  Nakwenda Kujinga sawaw sawa!!
   
 5. K

  Kamarada Senior Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kiongozi thanx kwa kuiona hiyo, nilitaka kupata Gen idea, nashukuru Mkuu "Trustme" kanipa idea niliyo kuwa naitaka :clap2:.
   
 6. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Unataka kununua gari kwenda Japan ama macho yangu?
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ha ha haaaa
   
 8. L

  Log Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
 9. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kuna vitu lazima uvi disclose ili tukusaidie kufanya calculations ambayo itakupa rough figure tu usitegemee ndio itakuwa gharama halisi as TRA wakiamua wana ku up lifts mathalan umenunua gari dola 1000 wanaweza kukataa na kuipa value yao hiyo value ndio base ya circulations zenyewe 5% import duty kuna VAT.

  Upande wa bandari lazima ujue vipimo vya gari unayoagiza na value as well wanacharge wharfage 6% ya custom value "hii baada ya ma uplifts yao na kupata release" kisha kuna handling ambayo ni 4 USD per CBM gari kama noah ina CBM 15 kwahiyo Handling charges ya Noah ni dola 60 bila VAT.
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ikiwa ni kutoka japan then hiyo post kabla ita apply ikiwa kwenda Japan itakuwa ngumu kujua as kila nchi ina sheria zake za forodha, je hilo gari linatoka chuo cha NYUMBU?
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  TRA wanawezaje kubadilisha gharama halizi nilizonunulia gari wakati kuna vithibitisho vya stakabadhi nilivyonunulia na kampuni nilikonunua?
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Trustme,
  Umesema uchakavu ni 20% kwa magari ambayo ni 10 years old and beyond. Je, hiyo 20% inatokana na bei ambayo mtu alinunua gari? Mathalan nina gari langu 15 years old, na nimekaa nalo kwa zaidi ya miaka kumi na nimeamua kurudi nalo Bongo. Nitahitajika kulipa 20 % ya value ipi?
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yaani gharama za kuingiza gari bongo ni zaidi ya gharama za kununua gari
   
 14. K

  Kakulwa Senior Member

  #14
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  duh hizi gharama wanaumiza sana aisee.Kuna gari nilitaka kuagiza kutoka Japan kwa US$3000,kwa mahesabu haya wallah mpaka linatembea inaeza fika US$ 10,000..duh kweli bongo ni noma
  Hivi wakuu kwa gharama hizi,kipi bora kati ya kuagiza mwenyewe au kuingia show rooms za bongo?
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ukiipata gari kwenye show rooms za b ongo kwa dola elfu saba nunua haraka.
   
 16. A

  Akiri JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Asante ndugu umetusaidia wengi. Huu ndio uzuri wa great thinker
   
 17. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2011
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Ukiingiza gari la zaidi ya miaka kumi utalipa kodi sawa na asilimia 93 ya CIF ya gari lako....wakati ukinunua gari lenye umri chini ya miaka kumi kama lina cc 1500 basi utalipa kodi asilimia 43 ya CIF na kama lina cc zaidi ya 1500 utalipa asilimia 65 ya CIF. Hii ni siplified version ya Trustme. Kwa zaidi ingia kwenye website ya TRA angalia kwenye Import duty...wametoa na jedwali kabisa
   
 18. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #18
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naomba nikusaidie kidogo,maneno mengi ya kiingereza hayana tafsiri ya moja kwa moja kuja kiswahili kama unavyodhani, mara nyingi yanategemea na namna na mazingira yanayotumika. Kwa mfano kwenye mpira, timu inapopata kona, lets say Totenham wamepata kona kuelekea goli la AC Milan, kwa kiingereza inatamkwa corner to Totenham (si corner from Totenham) au ikiwa wamepata faulo kuelekea goli la AC Milan, commentator atakuambia, this is foul to Totenham. Kwahiyo epuka kufanya tafsiri ya haraka na moja kwa moja.
   
 19. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,865
  Likes Received: 2,805
  Trophy Points: 280
  Mbona mifano yako sasa haiendani na hoja iliyokuwapo? Elewa hii ni bidhaa na mfano wako umelalia kwenye mpira! Hata kama utakuwa una Kiingereza cha Oxford hatukubaliani na wewe kwamba hiyo sentensi ilikuwa sahihi!! Maana kwenye bidahaa lazima tusema you are "importing from" and you are "exporting to"
   
 20. m

  majiyashingo Member

  #20
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau huu mchanganyuo si wa kawaida asante ila je ni kama mwagizaji ni mwanafunzi ambaye ndo kwanza tu ametoka kusoma kaja na hiyo gari je naye anapaswa kulipa hayo yote au ni kipi atapaswa kulipa kutoka kwa hivyo maana nasikia serikali iliahidi ushuru bure kwa wanafunzi waliokuwa nje
   
Loading...