Gharama za kufunga Drip kwa ekari (70mx70m)

Gharama za kufunga Drip kwa ekari (70mx70m)

Jamani habarini wana JF.

Niko mbioni kufunga drip irrigation system shambani kwangu. Nimeona niachane na miradi mingine kwanza nikomae na hili. Nataka nilime vitunguu saumu kwa shamba lenye ukubwa wa mita 70 kwa 70).

Maji tayari ninayo nilichimba kwa mtambo (drilling), na kisima kiko hapo hapo shambani. Kwa sasa navuta maji kwa umeme wa Tanesco. Shamba liko tambarare safi. Maji yanapotoka underground yanapanda na kuingia kwenye reserve tank niliyojenga kwa cement.

Nimenunua pampu aina ya Pedrollo kwa ajili ya kutoa maji kwenye reserve tank na kuunga kwenye mfumo wa drip, ila hiyo pampu sijaifunga kwa sasa. Itafanyika wakati wa kufunga drip system. Kwa wazoefu wa kufunga drip, natamani kujua niandae sh ngapi kiuhalisia kwa ajili ya materials, na sh ngapi kwa ajili ya fundi.

Nimeambatanisha picha hapo chini ili kupata ramani halisi kichwani. Hii pampu ya kusukuma maji (Pedrollo) inlet na outlet zake ni upana 1 inch. Je bomba linalofaa kuungwa kwenye drip system ni inch ngapi? Natamani mtu mzoefu kabisa aje anipe details kuliko kusema tu makadirio ambayo yanaweza yasiwe halisi.
Hongera mkuu ila nina swali moja tu mbegu ya vitunguu swaumu unachukulia wapi wastani wa bei ukoje
 
Kama mambo ya mwajiri bado yanakukaba ni bora uka sort out hayo kwanza kabla hujaanza rasmi hii project yako.maana hiyo oroject inakuhitaji kwa karibu sana.yaani inahitaji muda wako mwingi maana naye ni kwijiri anayejitegemea.
Nakuelewa sana. Nifahandle fresh tuu,maana shamba lipo hapo mbele ya nyumba tu mkuu. Nikimaliza kufunga system naleta kijana wa kusimamia hapo, mimi nakuwa nafanya follow up kila siku nikitoka job au kabla ya kwenda, lakini pia familia ipo hapo kuwatch out every step. Siyo yale mashamba ya kulima kwa remote. Pia nature ya kazi yangu siyo ya kusimamiwa muda wa kuingia na kutoka. Isipokuwa kuna tight season na loose season. Kuna muda kazi itanifanya niwe bize na kuna muda nitakuwa free kiasi
 
Hongera mkuu ila nina swali moja tu mbegu ya vitunguu swaumu unachukulia wapi wastani wa bei ukoje
Mbegu ni kununua vitunguu alafu vile vidole ndo unapanda. Ila usichukue vitunguu vilivyotoka shambani fresh. Ukicheki na wakulima wanajua mbegu ni ile iliyokaa muda mrefu na imekomaa vizuri
 
Nakuelewa sana. Nifahandle fresh tuu,maana shamba lipo hapo mbele ya nyumba tu mkuu. Nikimaliza kufunga system naleta kijana wa kusimamia hapo, mimi nakuwa nafanya follow up kila siku nikitoka job au kabla ya kwenda, lakini pia familia ipo hapo kuwatch out every step. Siyo yale mashamba ya kulima kwa remote. Pia nature ya kazi yangu siyo ya kusimamiwa muda wa kuingia na kutoka. Isipokuwa kuna tight season na loose season. Kuna muda kazi itanifanya niwe bize na kuna muda nitakuwa free kiasi

Hapo sawa.maana huwezi wekeza hivyo halafu umtegemee shamba boy kwa zaidi ya asilimia 30%. Ila kama umeoa na mkeo yupo na muda na anapenda ishu za mashamba.Itabidi msaidiane kusimamia shoo.Ila siyo umuachie dogo sijui broo wako.Hao wote ni bora ya shamba boy.

Niliwahi kuwa na project ya ufugaji.Nikafeli vibaya sana kwa sababu muda wa kuangalia project yangu ulikuwa very limited.

Kila mtu anataka kukupiga kivyake,yaani daktari wa mifugo naye anakwambia leo niko busy nakuja kutibu kesho asubuhi wakati wewe kesho asubuhi utakuwa huna muda ila yeye ndiyo atakuwa na muda.

Haya mambo Bwana!
 
Kuweka tu rekodi sawa; acre ni sq.m. 4096 na sio 4900 regardless of the dimensions. Tukiiweka in square 🔲 shape itakuwa 64x64 na sio 70x70 kimazoea.
Watu wengi walipotoshwa na mambo ya miguu au hatua 70 Kwa 70 amszo zilikuwa kama conventional metric wakati hakuna vifaa.
 
Back
Top Bottom