Gharama za kufunga Drip kwa ekari (70mx70m)

GIAN JUNIOR

Member
Joined
Mar 9, 2011
Posts
49
Reaction score
53
Jamani habarini wana JF.

Niko mbioni kufunga drip irrigation system shambani kwangu. Nimeona niachane na miradi mingine kwanza nikomae na hili. Nataka nilime vitunguu saumu kwa shamba lenye ukubwa wa mita 70 kwa 70).

Maji tayari ninayo nilichimba kwa mtambo (drilling), na kisima kiko hapo hapo shambani. Kwa sasa navuta maji kwa umeme wa Tanesco. Shamba liko tambarare safi. Maji yanapotoka underground yanapanda na kuingia kwenye reserve tank niliyojenga kwa cement.

Nimenunua pampu aina ya Pedrollo kwa ajili ya kutoa maji kwenye reserve tank na kuunga kwenye mfumo wa drip, ila hiyo pampu sijaifunga kwa sasa. Itafanyika wakati wa kufunga drip system. Kwa wazoefu wa kufunga drip, natamani kujua niandae sh ngapi kiuhalisia kwa ajili ya materials, na sh ngapi kwa ajili ya fundi.

Nimeambatanisha picha hapo chini ili kupata ramani halisi kichwani. Hii pampu ya kusukuma maji (Pedrollo) inlet na outlet zake ni upana 1 inch. Je bomba linalofaa kuungwa kwenye drip system ni inch ngapi? Natamani mtu mzoefu kabisa aje anipe details kuliko kusema tu makadirio ambayo yanaweza yasiwe halisi.
 
Attachments

  • SHAMBA .jpg
    SHAMBA .jpg
    121 KB · Views: 51
Hongera sana kwa hatua uliyofikia. Pengine ungeweka wazi pump inayotoa maji underground kwenda kwenye store ni ya ukubwa gani (hp ngapi). Maana kiuhalisia huna haja ya kuvuta maji underground kwenda kwenye tank, halafu uvute kutoka kwenye tank kwenda kwenye drip system. Badala yake ipo namna maji yanatoka underground moja kwa moja kwenda kwenye mfumo wa drip shambani.
 
Namna gani hyo kiongozi!?
 
Spacing ya zao lako ikoje!!? Lazima ujue hilo ili ujue drip utanunua ya spacing ipi!???

Kisha ujue utapanda miche mingapi, hapo ndo utajua jumla ya urefu wa drip system.

Baada ya hapo ndio tutakuja kwenye mahesabu ya ukubwa wa kiwanja ili ujue utaitandaza vip hyo system.!!

Usiogope kufuatilia/kujifunza namna inavyotengenezwa kwani sio sayansi ya kurusha roketi.
 
Namna gani hyo kiongozi!?
Kama pump inapandisha maji bila shida mpaka juu ya ardhi, unaweza kuingiza moja kwa moja kwenye mfumo wa drip. Kikubwa ujue tu kuligawa shamba lako vizuri kwa kuzingatia pressure ya maji. Kiuhalisia, hakuna haja ya tank kwaajili ya mfumo wa drip. Mara nyingi tunaingizwa katika gharama za mfumo wa tank kutokana na influence ya wafanyabiashara wa mifumo ya umwagiliaji ambao huweka biashara mbele kuliko uhalisia
Jamani habarini wana JF.

Niko mbioni kufunga drip irrigation system shambani kwangu. Nimeona niachane na miradi mingine kwanza nikomae na hili. Nataka nilime vitunguu saumu kwa shamba lenye ukubwa wa mita 70 kwa 70).

Maji tayari ninayo nilichimba kwa mtambo (drilling), na kisima kiko hapo hapo shambani. Kwa sasa navuta maji kwa umeme wa Tanesco. Shamba liko tambarare safi. Maji yanapotoka underground yanapanda na kuingia kwenye reserve tank niliyojenga kwa cement.

Nimenunua pampu aina ya Pedrollo kwa ajili ya kutoa maji kwenye reserve tank na kuunga kwenye mfumo wa drip, ila hiyo pampu sijaifunga kwa sasa. Itafanyika wakati wa kufunga drip system. Kwa wazoefu wa kufunga drip, natamani kujua niandae sh ngapi kiuhalisia kwa ajili ya materials, na sh ngapi kwa ajili ya fundi.

Nimeambatanisha picha hapo chini ili kupata ramani halisi kichwani. Hii pampu ya kusukuma maji (Pedrollo) inlet na outlet zake ni upana 1 inch. Je bomba linalofaa kuungwa kwenye drip system ni inch ngapi? Natamani mtu mzoefu kabisa aje anipe details kuliko kusema tu makadirio ambayo yanaweza yasiwe halisi.
Pia ukubwa wa shamba lako kwa kupanda kitunguu uyahitaji wastani wa roller 10-12 hivi za mita 1000 kwa maana yae kuwa na matuta ya vitunguu yenye line 4-6@.
 
Kama pump inapandisha maji bila shida mpaka juu ya ardhi, unaweza kuingiza moja kwa moja kwenye mfumo wa drip. Kikubwa ujue tu kuligawa shamba lako vizuri kwa kuzingatia pressure ya maji. Kiuhalisia, hakuna haja ya tank kwaajili ya mfumo wa drip. Mara nyingi tunaingizwa katika gharama za mfumo wa tank kutokana na influence ya wafanyabiashara wa mifumo ya umwagiliaji ambao huweka biashara mbele kuliko uhalisia

Pia ukubwa wa shamba lako kwa kupanda kitunguu uyahitaji wastani wa roller 10-12 hivi za mita 1000 kwa maana yae kuwa na matuta ya vitunguu yenye line 4-6@.
Pampu inatoa maji kutoka chini ya ardhi ni 2HP, Submersible, umbali wa bore hole ni 100m. Sema sasa nimeshajenga tank la cement kama reserve ambayo ndo inakusanya maji, na pia nina tank ya plastiki (Polytank)
 
Hongera sana kwa hatua uliyofikia. Pengine ungeweka wazi pump inayotoa maji underground kwenda kwenye store ni ya ukubwa gani (hp ngapi). Maana kiuhalisia huna haja ya kuvuta maji underground kwenda kwenye tank, halafu uvute kutoka kwenye tank kwenda kwenye drip system. Badala yake ipo namna maji yanatoka underground moja kwa moja kwenda kwenye mfumo wa drip shambani.
mie nadhani ameweka tank la reserve kutokana na matatizo ya umeme, si unajua umeme wetu hasa huko mikoani ni shida
 
Kama ni kwa hoja hiyo sawa.
Hata hivyo "reserve" iwe reserve kweli. Siyo tank la lita 10000 kwa shamba la vitunguu.....
 
Kuna kipindi mambo ya mwajiri yananikaba hadi nakwama kuingia humu mara kwa mara
Kama mambo ya mwajiri bado yanakukaba ni bora uka sort out hayo kwanza kabla hujaanza rasmi hii project yako.maana hiyo oroject inakuhitaji kwa karibu sana.yaani inahitaji muda wako mwingi maana naye ni kwijiri anayejitegemea.
 
Umechimba kisima halafu unalima acre moja? Changamka wewe, weka acre 20 hapo kilimo sio hobby
 
Back
Top Bottom