Gharama za kuezeka nyumba zipoje?

lee jack

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
1,033
1,817
Habari zenu ndugu zangu. Nimepewa nyumba na baba yangu mzazi, ni nyumba ambayo haijapauliwa sasa nikaona ni bora niweke pesa ili nije kuipaua sasa naomba maelezo kwenu juu ya gharama za kupaua nyumba.Ni nyumba iliyopo dar es salaam.

Ina vnyumba vitatu vya kulala, sebule, choo na Jiko. Hapa nilipo Nina tzs 2,000,000.

Je, kwa pesa hiyo inawezekana kupaua nyumba na ikaisha?

Naombeni mchanganuo kuanzia bati mafundi na mbao
 
habari zenu ndugu zangu. Nimepewa nyumba na baba yangu mzazi, ni nyumba ambayo haijapauliwa sasa nikaona ni bora niweke pesa ili nije kuipaua sasa naomba maelezo kwenu juu ya gharama za kupaua nyumba.
Ni nyumba iliyopo dar es salaam
Ina vnyumba vitatu vya kulala, sebule, choo na Jiko. Hapa nilipo Nina tzs 2000,000 je kwa pesa hiyo inawezekana kupaua nyumba na ikaisha?

Naombeni mchanganuo kuanzia bati mafundi na mbao
Too general, leta vipimo na sio idadi ya vyumba
 
inategemea aina ya bati na style ya upauaji ulivyo..

kwa mgongo wa tembo style na bati za bei rahis kabisa zile gauge 30 hiyo hela inaweza fanya nusu kazi so ukiwa na m4 hivi inatosha kabisa
mkuu mimi nataka tuu Bati za kawaida ila ziwe na rangi sitaki za migongo ni gharama. Je hizo za kawaida zenye rangi pesa hiyo itatosha?
 
Endelea kuvuta subira kuna wataalamu wazuri sana wako humu,ila hata mimi ningekushauri utaje vipimo vya hiyo nyumba,ugepata hata urefu na upana,angalau ingesaidia katika kupata makisio..
 
hapo kwenye kupima ndo sijui jinsi ya kupima ila ni nyumba ya wastani tuu
 
Hiyo pesa ya fundi tu m bona1.5m....mbao za hapo makadilio ya chini 2m...bati 3m..misumal na vitu zingine kama 200 elf...so kwa ufipi tu unatakiwa uwe na kama 6m kama unaezeka bati za rangi za kaida..maana bati zinaeza fika 130pcs.
 
fundi tuu ni 1.5 mbona ghali sana
 
Kukusidia ni kwamba tafuta fundi aje akupimie hyo nyumba na akuambie bati ngap zinatosha,,anza kununua bati uzihifdhi then utafute hela ya mbao na ufundi then ndio upaue. Itakusaidia zaid
 
Habari zenu ndugu zangu. Nimepewa nyumba na baba yangu mzazi, ni nyumba ambayo haijapauliwa sasa nikaona ni bora niweke pesa ili nije kuipaua sasa naomba maelezo kwenu juu ya gharama za kupaua nyumba.Ni nyumba iliyopo dar es salaam.

Ina vnyumba vitatu vya kulala, sebule, choo na Jiko. Hapa nilipo Nina tzs 2,000,000.

Je, kwa pesa hiyo inawezekana kupaua nyumba na ikaisha?

Naombeni mchanganuo kuanzia bati mafundi na mbao
Bila shaka UMRI WAKO bado bado kidogo nilidhani au sikuona maana ya kutamka kuwa umepewa na BABA YAKO. Nadhani jibu utalipata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
vipimo kivipi mkuu
Nina boma la 12m urefu na 10.6m upana , angle ya paa ni nyuzi 30 , dizaini ya paa ni kama hapo chini ,naomba makadilio ya bati na mbao.
 
Attachments

  • IMG_20200103_131335.jpg
    IMG_20200103_131335.jpg
    31.1 KB · Views: 82
Kama unapaua Kwa bati la kawaida Kwa wachina bei ni elfu 20,g30,kwa makadirio ya chini itaingia Bati 120,so ukizidisha utapata 240000 mbao umejibana sana 1.2M,mafundi wako wa bei nzuri tuu700-800k wanakupaulia.Ukipau mpauo ambao hauna mbwembwe bati 80,zitatosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu ndugu zangu. Nimepewa nyumba na baba yangu mzazi, ni nyumba ambayo haijapauliwa sasa nikaona ni bora niweke pesa ili nije kuipaua sasa naomba maelezo kwenu juu ya gharama za kupaua nyumba.Ni nyumba iliyopo dar es salaam.

Ina vnyumba vitatu vya kulala, sebule, choo na Jiko. Hapa nilipo Nina tzs 2,000,000.

Je, kwa pesa hiyo inawezekana kupaua nyumba na ikaisha?

Naombeni mchanganuo kuanzia bati mafundi na mbao
2M kuezeka nyumba hiyo haitoshi,kwa makadirio itakula bati 80 mpaka 90,sasa bati 90 zitakula sh ngapi?,bado mbao na hela ya ufundi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom