Gharama ya ziara ya Prof Muhongo Mkoani Mara ni kufuru

Gharama ya ziara ya Prof Muhongo Mkoani Mara ni kufuru

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,018
Reaction score
20,489
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi katika ziara ya dalali wa wezi nchini Prof Muhongo kumebainika ufujaji mkubwa katika wizara hiyo kwa ziara ya waziri huyu katika sherehe za krismasi na mwaka mpya.

Kwa upande wa taarifa zilizonaswa ndani ya jeshi la Polisi mkoani Mara nikuwa katika kibali cha tarehe 24 Dec gate pass number 1776857, Muhongo aliomba ulinzi toka jeshi la polisi kisha akaambiwa jeshi halina mafuta ya mchezo mchafu, kuona hivyo Muhongo akaamua kugharimia mafuta na matengenezo ya magari ya polisi na kuwalipa polisi wote atakaoambatana nao katika ziara yake.

Nyaraka zinaonyesha jeshi la polisi lilikabidiwa mafuta ya dizeli lita mia tisa (900) kwaajili ya magari mawili yaliyokuwa yakiongoza msafara huo, Matairi manne mapya kwa ajili ya gari aina ya Toyota Land cruiser, T 381 BQP, Blue ya Polisi.

Malipo hayo yamefanyoka Central store ya Musoma power station, Gate keeper anaitwa Musa anakiri kupitisha, maana ni order ya wizara, Escort ya magari mawili na askari kumi walilipwa posho zao laki tano kwa siku kila mmoja. Pia Waandishi wa habari Kasoro wa IPP media, walilipwa laki Tatu kwa kila Mwandishi wa siku kwa kila story nzuri iliyotoka, Blogger pia walialikwa.

Kula na kulala kwa wote ilikuwa juu ya wizara(Muhongo.

Musoma walikaa Penisula hotel, Tarime walikaa Goldland Hotel, Serengeti walikaa Giraffe hotel, Butiama na Bunda walienda na kurudi.

Hoja ya msingi nikuwa gharama hizi zinatoka katika bajeti ipi pale wizarani??
 
Kwamjibu wa taarifa za kiuchunguzi katika ziara ya dalali wa wezi nchini Prof Mhongo kumebainika ufujaji mkubwa katika wizara hiyo kwa ziara ya waziri huyu katika sherehe za krismasi na mwaka mpya.

Kwa upande wa taarifa zilizonaswa ndani ya jeshi la Polisi mkoani Mara nikuwa katika kibali cha tarehe 24 Dec gate pass number 1776857, Mhongo aliomba ulinzi toka jeshi la polisi kisha akaambiwa jeshi halina mafuta ya mchezo mchafu, kuona hivyo Mhongo akaamua kugharimia mafuta na matengenezo ya magari ya polisi na kuwalipa polisi wote atakaoambatana nao katika ziara yake.

Nyaraka zinaonyesha jeshi la polisi lilikabidiwa mafuta ya dizeli lita mia tisa (900) kwaajili ya magari mawili yaliyokuwa yakiongoza msafara huo, Matairi manne mapya kwa ajili ya gari aina ya Toyota Land cruiser, T 381 BQP, Blue ya Polisi,

Malipo hayo yamefanyoka Central store ya Musoma power station, Gate keeper anaitwa Musa anakiri kupitisha, maana ni order ya wizara, Escort ya magari mawili na askari kumi walilipwa posho zao laki tano kila mmoja. Pia Waandishi wa habari Kasoro wa ipp media, walilipwa laki Tatu kwa kila Mwandishi kwa kila story nzuri iliyotoka, Blogger pia walialikwa,

Kula na kulala kwa wote ilikuwa juu ya wizara(Mhongo.

Musoma walikaa Penisula hotel, Tarime walikaa Goldland Hotel, Serengeti walikaa Giraffe hotel, Butiama na Bunda walienda na kurudi.

Hoja yamsingi nikuwa gharama hizi zinatoka katika bajeti ipi pale wizarani??


yericko tupia viambatanisho hapa
 
Pesa za umma hazimuumi,angekuwa anazitoa mfukoni mwake asingefanya hivyo.

Issue sio kumuuma, muhimu ni ukweli kuwa hatakiwi kuwa ofisini. Anafanya safari za kujijenga binafsi kwa kutumia pesa za umma.
 
We tapeli wa laki mbili lete ushahidi ili tuamini hii hadithi yako
 
!!!!
huyu profesa ndio alikataa kupande ndege hadi akae first class???
!!!!!
 
Mara nyingi ukiona mtu anatoa story kama hizi ujue na yeye kuna dili alikuwa amelilenga la kumpa ulaji kwenye hiyo ziara likampita pembeni, kama siyo yeye basi anatumiwa na mtu aliyelenga kunufaika na yeye kapigwa chini. Na inaonekana kuna watu walikuwa wanagombania ulaji kwenye hiyo ziara wakazidiana kete sasa waliokosa wanaamua kuharibu.

Hebu, tusaidie pia ndugu yangu Yericko, lengo la hiyo ziara ilikuwa ni nini? Alilenga kwenda/ alienda wapi na wapi? ni yapi matokeo ya hiyo ziara (matokeo yaliyopatikana au yanayotarajiwa) kwa maendeleo ya taifa letu?
 
Mkuu Yericko Nyerere kama umeweza kujua matumizi hayo umeshindwaje kujua zimetoka wapi?
 
Last edited by a moderator:
Hata kama Muhongo angekuwa tajiri , HAYA NI MATUMIZI YA KISHAMBA SANA ! asante mkuu yericko kwa kufichua ubadhilifu wa kishamba sana kama huu .
 
Back
Top Bottom