Gharama msingi vyumba vitatu

Gharama msingi vyumba vitatu

Ambrose Koller

Senior Member
Joined
Oct 13, 2024
Posts
109
Reaction score
102
Wakuu Naomba kuuliza msingi wa vyumba vitatu kimoja self, jiko sebule na public toilet kwa Dar unaweza kutumia cement mifuko mingapi?
 
uwe na mifuko 30 kwa uzoef wangu, hakikisha mkanda unashiba cement hapo ndo nyumba ilipo
Mifuko 30×60 =1800 je hizo tofali si zinakamilisha nyumba kabisa? Hesabu yako sio relevant
 
Mfuko mmoja unajenga tofali 60 mpaka 70, fundi kakuambia ununue tofali ngapi?
Wakuu Naomba kuuliza msingi wa vyumba vitatu kimoja self, jiko sebule na public toilet kwa Dar unaweza kutumia cement mifuko mingapi?
 
Mie niliona mtu alikua na mifuko 22, sasa sijui hapo.
Hpana hapo labda kuna factor nyingine ikiwemo kulaza tofali ngapi na ukubwa wa vyumba na sebule au muinuko. Lakini mifuko ya saruji inaletwa kulingana na wingi wa tofali. Mfuko mmoja tofali za kulaza 65. So mifuko 10 kwa tofali 650. Msingi wa hiki anacholisema hauwez kufika tofali 800 landa kuwe na factor nyingine. Mana msngi wa chumba kimoja ni around 220-260 kutegemea na ukubwa na urefu wa msingi
 
Oooh kumbe bas sawa.
 
Kama ni msingi wa kozi sita utachukua tofali 860 -1,000. Pia ukubwa wa vyumba hapo nimepiga vyumba vyote Sawa yaani futi 10.5 ×10.5. Kwa portion zote 5 yaani jiko,sebule na vyumba 3.Mifuko 20 ya cement na roli moja la mchanga lenye ujazo wa m 4 Sawa na debe 200.Hapo bila mkanda.
 
Oooh kumbe bas sawa.
Yan hapo asipate tabu mana fundi wake tofali alizomwambia ajue tu mfuko mmoja wa cement ni toroli 4, sawa na chepe 70 sawa zenye uwezo wa kujenga tofali 65. Hivyo atumie formula hii
 
Back
Top Bottom