Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267

Kizaazaa kilitokea wakati wahudumu katika makaburi walitoa mwili katika jeneza na 'kuuteka nyara' kwasababu ya deni.
Kisa hicho cha kushtua kilitokea Accra, Ghana. Iliripotiwa kuwa familia ya marehemu walishindwa kuwalipa wahudumu hao wa chumba cha kuhifadhia maiti waliodai familia hiyo Sh3,000 za Ghana.
Kisa kilianza wakati wanaume wawili wamesimama juu ya jeneza huku mamia ya watu wakiwa wamesimama kutazama kisa hicho.
Wahudumu hao wenye ghadhabu waliwapigia kelele umati huo huku wakiendelea kuutoa mwili huo katika jeneza.
Muda mfupi baadaye, wanaume hao wanaonekana wakibeba mwili huo mabegani! Baadhi ya watazamaji wanajaribu kuongea na wanaume hao ambao kwa hasira wanatumia mwili huo kuwaashiria watu kuondoka.

Wanaume hao waliondoka nao kabisa bila kujutia hatua yao hiyo. Haikujulikana ikiwa marehemu alizikwa na hao wanaume au waliendelea kumshikilia kwa kutaka kulipwa.
Chanzo: TaifaLeo