GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,572
- 117,796
KENYA - Mahakama ya Rufaa imeagiza mwili wa Silas Igweta uhifadhiwe katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Umash jijini Nairobi kusubiri kesi iliyowasilishwa na mke wa pili wa marehemu, Sarah Kathambi.
Sarah Kathambi na mke mwenza Grace Rigiri wanapigania ni nani anafaa kuzika mabaki ya mume wao.
Igweta alifariki jijini Nairobi mnamo Februari 17 akiwa na umri wa miaka 100.
Alikuwa akiishi na mke wake wa pili Kathambi alipofariki.
Huku Kathambi na watoto wake Purity Kinya na Miriam Makena wakifanya mipango ya mazishi, mke wa kwanza Rigiri na mwanawe Mathew Kobia walihamia mahakamani wakitaka kuamuru mwili huo uachiliwe kwao kwa mazishi.
Wanawake hao wawili wana nyumba zao Kianjai (Rigiri) na Lairangi Mumui (Kathambi) ambazo zimetengana takriban kilomita 40 ndani ya Eneo bunge la Tigania Magharibi katika Kaunti ya Meru.
Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani G.M Gitonga mwezi Aprili aliamuru Igweta azikwe nyumbani kwa mkewe wa pili akisema familia ya pili ilikuwa na uhusiano wa karibu wa kifamilia na marehemu.
Hakimu pia aligundua kuwa ni wosia wa Igweta kwamba azikwe Lairangi Mumui.
Lakini Rigiri alihamia Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo.
Alishinda baada ya Hakimu Stephen Riechi katika hukumu yake ya Mei 21 kuagiza mwili wa Igweta uachiliwe kwa mke wake wa kwanza kwa mazishi huko Kianjai kwa mujibu wa mila na desturi za wameru.
Chanzo: habarileotz
==========
Mtu ameshaaga dunia na yawezekana hata kuaga Kwake dunia huko kumetokana na Upumbavu wenu halafu bado tena mnamtesa kwa Kumchelewesha kumhifadhi katika Nyumba yake ya milele.
Kuna muda huwa namuuliza kidogo Swali Mwenyezi Mungu ni kwanini aliniumba Mwafrika kwani kuna Matukio yanafanywa na Waafrika kadhaa Majuha kisha Waafrika wote tunaonekana Wapumbavu tukuka.
Na hapa unaweza kukuta wakati Marehemu labda anaugua yuko Kitandani walikuwa hata Wakitegeana kwenda Kumuona au Kumuuguza au hata Kumhudumia Kiupendo ila baada ya Kufariki ndiyo wanajifanya Kumpenda na kila Mtu kuvutia Kwake.
Na hapa ( katika huu Mzozo wa hawa Wake wawili ) ukiwa na Akili pana / kubwa utagundua kuwa kinachogambaniwa hasa si tu azikwe kwa Mke yupi bali ni azikwe na Mke yupi ili hata kwenye Mgao wa Utajiri wa Mali ( Fedha ) za Marehemu pia nyingi ziende kwa Mke yupi.
Ushauri kwa Wanaume ambao mnaoa / mmeoa Wake Wawili tafadhali jitahidini sana mkiwa bado Hai jengeni Upendo kwa hao Wake zenu na Vizazi vyako, gawa mapema Mali zako kwa Usawa ili hata Siku Israeli akibonyeza Kitufe chake cha Wewe kuandoka mazima Duniani basi usiache Mizozo ya Kishamba na Kipumbavu huku nyuma.