GF wangu anakatishwa tamaa na watu

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,978
5,025
Nampenda na yeye ananipenda. Kinachoniumiza kuna watu wanaonifahamu wanamfeed mambo yangu ambayo hayamvutii. Kuna wengine wanamtajia wasichana niliowahi kuwa nao. Mwingine alifika mbali zaidi na kumwambia mimi nimeoa na kuacha mke. Huwa ananiulizia majina ya hao wasichana na tulikuwa na uhusiano gani! Nilishamwambia kuwa nilikuwa na mahusiano huko nyuma na nimeacha lakini sikumtajia majina yao. Hivi haniamini? Nifanyeje? Naona kama itavunja uhusiano, maana kuna muda huwa nakasirika ila najishusha.
 
Kama unampenda kwa dhati then umwambie vitu vinavyokuhusu ambavyo unahisi akiambiwa na mtu mwingine itakuwa disaster....ni bora asikie kutoka kwako kuliko kutoka mdomoni mwa mwingine..niamini mimi,lazima uaminifu upungue especially wakati akikuuliza unaanza kubabaika...ndo kabisa atakuona una vitu vyako vya kijinga unavificha...Funguka bro!!
 
Na si unajua mdomo haulipiwi kodi...mtu akiamua kuliongelea lako likitiwa chumvi hilo...haliliki hata kwa ndimu lazima GF wako akasirike,so kama una vijimambo vyako bora umwambie..
 
Komaa ! Ng'ang'ana na Mususu wako hao wavimbamacho hua wapo kila eneo hakuna masika yakakosa Mbu!
 
Kama unampenda kwa dhati then umwambie vitu vinavyokuhusu ambavyo unahisi akiambiwa na mtu mwingine itakuwa disaster....ni bora asikie kutoka kwako kuliko kutoka mdomoni mwa mwingine..niamini mimi,lazima uaminifu upungue especially wakati akikuuliza unaanza kubabaika...ndo kabisa atakuona una vitu vyako vya kijinga unavificha...Funguka bro!!

nashukuru kwa ushauri. In short sikupenda kuanza kuzungumzia nilikuwa na nani au yeye alikuwa na nani before. Nilichomwambia ni tunaanza safari yetu wawili tuachane na waliotusindikiza nyuma. Ila akiniuliza huwa nafunguka ukweli na kuukana uongo. Kinachonikera ni ile kunikumbushia watu ambao wengine nilishawasahau.
 
Na si unajua mdomo haulipiwi kodi...mtu akiamua kuliongelea lako likitiwa chumvi hilo...haliliki hata kwa ndimu lazima GF wako akasirike,so kama una vijimambo vyako bora umwambie..

nilishamwambia kuhusu kuwa na uhusiano huko nyuma kabla yake na nimetengana nao.
 
mwanawane hapa wewe itabidi uwe muwazi. pamoja na kuwa honest inabidi ukubali kuwa kunauwezekano kuwa mwenzio asipendelee historia yako na hivyo kujenga mistrust kwako. sasa swali lakijiuliza ni je upo tayari kukubali kuwa kwenye uhusiano ambao wewe kwa muda mrefu utakuwa unajitahidi kumthibitishia kuwa u r trustworthy?....kama haupo ready basi jua kuwa hapa ni muda wakusepa.
 
kwa nini usimwambie past yako yote huyo mdada?

unajua hata ungekuwa wewe nikikuambia nimepitia wasichana 15 mfano,ungeweka uoga wa kutoniamini kwa sababu utahisi mi ni virulent sana. Lakini nikishasema kuna wasichana nilishakuwa nao inatosha.
 
Achana nao wanachuki binafsi hao.Zidisha upendo kwa huyo Gf wako,na mwambie ukweli.Past is past.na yeye ndo present,aache kusikiliza wanafki.
 
kuna faida gani kuanza kupekenyuana? Ni ajabu sana. Mmependana kama mnavyoonana. Kasoro za nje wala za ndani hazionekani na hazina athari katika mahusiano yenu kwani mmeamua kuacha ya kale na kuwa wapya. Sasa inakuwaje maneno toka kwa watu yaanze kubadili mentality ya mtu? Wakati mwingine huu ni ulimbukeni. Anachokonoa ya zamani ili muachane? Mkaripie huyo na wala usimbembeleze kwani anatapatapa. Kwa maneno yako mwambie aache ujinga na hakuna faida ya historia yako wala yake.
 
je anayoambiwa na watu yana ukweli? kama ni ya kweli kwa nini usiwe wazi kwake toka mapema mpaka aambiwe na watu? hakuna kuaminiana kati yenu?
 
Nadhani hapo hata huyo Mpnz wako anasikiliza sana watu,
Kwann anawapa watu nafasi ya kuongelea mpnz wake mpaka wamwambie mamabo yako ya zaman?
Km anakupenda kweli nawe umekua muwazi kwake,onesha msimamo bwana,
Mapnz ni yenu wawili hao wambea asiwasikilize na asiwe na muda wakuongea nao na kuwapa nafasi ya kukuharibia.
 
inavyoonekana huyo mpnz wako hana msimamo au bado ana akili za kitoto! mambo ya kufatilia kuwa ulikuwa na demu gani hapo nyuma hayana maana, cha muhimu alipaswa ajue msimamo wako wa sasa na ni jinsi gani we unamfeel na kujali, kaa naye ongea naye,
anapaswa aelewe kuwa kabla yake we hukuwa h*n*s.
 
hehehehe hapo chacha kuna watu wana msururu wa totoz kiasi akianza kutoa historia huyo demu mwenyewe anaweza kuanza kuwazia kusepa .
 
Funguka mkuu kwa demu wako kwa kumuambia ukweli past relationship yako,
pia jaribu kumuonyesha mapenzi ya dhati na uwe naye karibu.
Pia kama bado una uhusiano na hao wadada wa zamani, kata mawasiliano nao haraka sana.

Inawezekana bado ana wasiwasi nawe sababu hujawa muwazi kwake kitu ambacho kinamkosesha raha kabisa na ni mbaya sana ktk uhusiano wowote.
 
Huyo mpenzi wako nae asijifanye anakupenda mpaka anakerwa na mambo yako yalio pita inamaana yeye hakua na bwana kabla yako au alikutajia majina ya wote? yeye asitake kujua alikua nani na nani sababu hamtafika mbali na wewe ndio ulomjulisha kwa hao marafiki sasa iweje awasikilize hao kuliko wewe? mwambia wenzie walipo acha yeye aendeleze na mweleze kero zake ndio zitafanya ukawarudie au ukachukue mwengine,yeye kazi yake nikujishughulisha na mapenzi na kukujali ili usiwakumbuke wale walopita kwa RAHA zake kama atakua na mjanja,mwambie Ujanja kupata sio kuwahi sasa kama anataka uibiwe kwenye mikono yake kazi kwake...
 
hehehehe hapo chacha kuna watu wana msururu wa totoz kiasi akianza kutoa historia huyo demu mwenyewe anaweza kuanza kuwazia kusepa .

ndo hapo! Hata mi naogopa kumtajia msururu asije nikimbia. Nampenda sana na wengine woote,nilishawaacha.
 
Back
Top Bottom