lukubuzo Samsis
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 2,947
- 3,466
Kwanini urekodi?hujui km ikulu ni sehemu moja wapo usiyotakiwa kupiga picha kama hujapewa ruhusa?Naskia watu wanarushwa kichura kisa kushangaa sana ukuta...hivi wakikukuta unarekodi video ya jengo si unaweza kupewa uhaini kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
wewe ndo jesca?Kama unakuja njoo utanifahamu vizuri ukifika wala usihofie
Unamaanisha ile barabara ya kutokea wizara ya fedha kuelekea ferry imefungwa?Katiba inasemaje kwa raisi wa awamu ya tano ofisi zake zisiwe wazi? Ile Barabara aliyopewa Obama ndio basi tena imefungiwa
Nakumbuka kipindi cha kikwete kule Ikulu upande wa baharini tulikuwa tunaenda tunakaa hata siku nzima hadi wengine walikuwa wanaogelea nk...lakini siku ole wako ukutweIkulu zingine shughuli zingine zinaendelea mpk kupga picha selfie ikulu no problem...why here?
Ndio obama roadkwenye ile barabara si wanakataza kupita siku hizi.
[emoji23][emoji23][emoji23]Mimi nikifika maeneo yale hata kama ushuzi umenibana huwa najizuia mpaka niingie kwenye soko ndiyo naachia, unaweza kuambiwa una bomu la sumu ya anthrax
IkawajeHii umenikumbusha mwaka 2011 tulipita na jamaa yangu kule ufukweni kisha tukaona hakuna watu tukakojoa pembezoni mwa bahari! Aisee ile siku sitaisahau maishani mwangu.. Nikipindi cha utawala wa msoga daahh
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi sitaki hata kupitia mitaa hiyo...........Mimi nikipita pale hata kushangaa shangaa sana hua naogopa...hii nchi watu walivyo wababe unaweza kupewa kesi ya uhaini kirahisi rahisi.
Yaani nikipita pale mbele ya geti naangalia mara moja tu sigeuki tena tusije halibiana maisha
Sent using Jamii Forums mobile app
Juzi kati nimepata hakuna raia wanaobarizi kwenye ile miti kama zamani.Nakumbuka kipindi cha kikwete kule Ikulu upande wa baharini tulikuwa tunaenda tunakaa hata siku nzima hadi wengine walikuwa wanaogelea nk...lakini siku ole wako ukutwe
DuuuhNakumbuka siku moja niliingia matatani na jamaa wa suti nyeusi wale nakuaga kule nyuma ya ikulu beach kule wanao jifanyaga nao eti wanapanga upepo na hata mashati unaweza kuta wamevua.
Alikuja jamaa yangu kutoka mkoa hivyo nikaamua nimpeleke akaone bwana mkubwa wa wakati huo NKAPA anapoishi. Sasa kwa uzoefu wangu wa ule ukuta unaozunguka nyumba nyeupe kila baada ya mita tano au sita Kuna nguzo ya taa pamoja na vioo/camera ambavyo kazi yake wote twaijua.
Wakati tunapita kule upande wa beach nikawa namuelezea mgeni wangu juu ya hivyo vioo viliyo uzunguka ule ukuta wa nyumba nyeupe.katika hali isiyotarajiwa nilikuta mtu ananishika bega na kuanza nihoji vioo gani hivyo navyo zungumzia. Nilifikiria anatania tuu kumbe jamaa alikua kazini hasaaa.
Ashukuliwe mungu sikua na nia mbaya na Ile nyumba nyeupe, japo ilikua mbinde sana hadi kuwa huru.
Zama hizi za jiwe sio busara kabisa unapopita mitaa Ile kujaribu kukodolea macho eneo lile.
USOGA WI KUA KATI MWINA NSONGOO
Naamini wengi tulishawahi kupita maeneo ya magogoni pale, kwenye nyumba ya mkuu wa nchi ile ni ofisi kama zilivyo ofisi zingine za umma na huwa wanaacha wazi geti lao wazi 24 hours na wala hakuna aliye getini lakini kuna kakitambo kidogo kutoka getini mpaka kwenye ofisi za raisi zilipo...
Lakini cha kushangaza hakuna concentration ya watu eneo lile wala muonekano wa watu wakiingia na kutoka ikulu kupata huduma mbali mbali za umma kama zilivyo ofisi mbalimbali za umma sana sana ni magari tu ya kifahari yanaingia na kutoka na watu wenye suti suti tu na tinted na ving'ora.
Kwanini labda...?
Hebu nifungueni macho siku moja nilitaka niende nikamuone mkulu nikampe hata hai nikapige hata selfie kama zilivyo garden nyingine maana pale ikulu kuna garden safi sana.