13 October 2021
Chato, Geita
Tanzania
KITABU CHA NYERERE CHAFICHWA / MONGELA AFUNGUKA SABABU ZA KUFICHWA KITABU HICHO
Gertrude Mongella akemea siasa za ubaguzi zinazoendekezwa na jamii iwe kisiasa, kijamii, kijinsia, rika n.k
Ametoa hotuba moja ikigusia mfano kuwa mwanamke ni anasifa zote
Hivyo ubaguzi wa namna yoyote hautakiwi kwa kufuatana na sifa sita (6) za Binadamu hapo juu.
Mama Gertrude Mongella anakwenda zaidi na kusema mwanamke pia ana sifa ya ziada kwani binadamu tumeumbwa kwa dongo, lakini Mungu alipomuumba mtu-mume kwanza kwa kutumia udongo akamtazama kiumbe huyu akaona kuna kasoro/ mapungufu hivyo badala ya kuchukua udongo kufinganya kiumbe kingine akaona ni vizuri zaidi kuchomoa ubavu kutoka kwa mtu-mume na kutengeneza mtu-mke yaani katika hatua ya juu zaidi isiyo dongo lililofinyangwa hivyo kusahihisha yale aliyoyafikiria akifinyanga dongo.
Hivyo kuna kusudio kubwa la Mungu kumtengeneza mtu-mke katika hatua ya juu zaidi ili mtu-mke aweze kufanya majukumu mengi zaidi.
Hivyo mtu-mke asitiwe unyonge na jamii kuwa kuna masuala hawezi kuyatekeleza kwa manufaa ya jamii pana zaidi. Gertrude Mongella asema kuna njama za jamii na wala siyo za wanaume, ambazo zinatala kuzuia wanawake wasitambulike kama binadamu sawa au raia wenye haki sawa n.k
Mwaka 1944 Julius Nyerere akiwa mwanafunzi chuo kikuu cha Makerere Uganda, aliandika kitabu kuhusu wanawake ambacho kinafichwa fichwa ...
Mifumo hii ya kutenga baadhi ya wanaume kushiriki , wanawake kuwepo ktk nafasi za maamuzi , demokrasia kupewa wanachama wa chama fulani n.k mifumo hiyo ya kuwazuia baadhi ya raia katika jamii inatakiwa kubadilishwa...
Chanzo: Mwanahalisi TV

- Ni binadamu
- Raia wa nchi fulani
- Haki
- Ana akili
- Ana vipaji
- Mwanamke siyo malaika wala shetani