JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Mtandaoni kuna maoni hasi dhidi ya Serikali au Viongozi wa Serikali, hamuoni kuna kiwango fulani Wananchi hawapendezwi na kinachoendelea?
Gerson Msigwa: Mengi yanayozungumzwa hayana ushahidi, tatizo hili siyo Tanzania tu, mitandao imekuwa ikitumika vibaya katika Nchi nyingi, sasa hivi kuna AI, kuna watu wanatumia nafasi hiyo kupotosha umma na kuchafua viongozi.
Huu ni wakati wa Uchaguzi watu hao wenye nia hasi wanaona ni wakati sahihi wa kugombanisha Wananchi na Serikali.
Kuna mtu kajificha nje ya nchi anapotosha Watanzania, niwaambie Watanzania msidanganywe na wanaojificha nje ya Nchi na kuandika taarifa potofu, fuatilieni kwenye tovuti rasmi za Serikali kuna taarifa sahihi.
Mtu asizungumze kama ndiye mamlaka, atawapotosha.
Hayo ni mahojiano ya Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alipozungumza na Kituo cha UTV, leo Jumatatu Oktoba 13, 2025.
MSIGWA: WANATUMIA AKAUNTI ZANGU KUPATA FOLLOWERS
Katika ukurasa wako umekuwa ukifunga comments kwa nini?
Msigwa: Nilifanya utafiti nikagundua kurasa zangu zina wafuatiliaji wengi, nikukusanya zote ni takribani milioni 3 hivi, pia nafuatiliwa na watu wengi makini, wakati huohuo kuna wengine wanatumia ukurasa wangu kufanya siasa.
Kuna watu wengi wanaanzisha akaunti ambazo hazina followers, hivyo wanatumia kurasa zangu ili waongeze followers.
Ukiona nimepost na kuacha ujue nipo na muda wa kufuatilia kinachowekwa kwenye comments , nikiwa sina muda ninafunga koment.
Hata kama kuna uhuru wa maoni, siwezi kuacha watu watukane na watoe ujumbe wa vitisho kwenye pages zangu.