Gerson Msigwa hakikisha leo Rais anaongea kilichosomwa na ulichomwandikia hapo JNIA vinginevyo...

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,568
108,911
Kwa tunaojua ' Saikolojia ' ya Mheshima Rais hapa pale pakiwa na jambo fulani linalomtatiza na lililoanzishwa na Wapinzani au Wapingaji huwa akipewa nafasi ya Kuongea hutoka kabisa nje ya ' Key ' na kuanza kuwa ' emotional ' au ( Kujaa Upepo ) hali ambayo huwa inamuharibia sana.

Ni vyema kwa Mhusika Mkuu hasa upande wa Mawasiliano hapa namaanisha Gerson Msigwa leo akahakikisha Rais anasoma kile tu alichomuandikia ili kuepusha kumwachia aongee tu mwenyewe na kupelekea muda wake mwingi kuutumia kupiga ' Vijembe ' badala ya kujadili mambo makubwa yenye tija na mafanikio zaidi.

Ajikite tu katika kutuambia malengo ya hizi Ndege na mafanikio yake kwa Tanzania lakini aepuke kuweka mambo mengi ' irrelevant ' katika Uhutubiaji wake kwani kwa sasa ' Saikolojia ' ya Wananchi haipo upande wake 100% hivyo kama akiweka ' Vijembe ' vyake kwa wale ' anaowachukia ' anaweza kujikuta ndiyo anaharibu zaidi.

Kazi yangu ni Kushauri tu na nimeshaifanya hapa.

Kila la kheri

Nawasilisha.
 
Leo maaskofu
Wapinzani wajiandae kupewa vidonge vyao


Leo anatoa dozi kavumilia wiki hizi kusemwa semwa

Subiri niandae bisi zangu

Na ndiyo maana nimetahadharisha mapema kwani siku hizi huhitaji kuwa na Certificate ( Astashahada ) au Diploma ( Shahada ) au Bachelor Degree ( Shahada ya Kwanza ) au Masters Degree ( Shahada ya Uzamili ) au Philosophy of Doctorate Degree ( Shahada ya Uzamivu ) kuweza kuijua ' Saikolojia ' ya Mheshimiwa Rais wetu kwamba ni mwepesi sana ' Kuhamanika / Kuhemka ' ( Watoto wa mjini tunaita Kujambishwa au Kujazwa Upepo ) kisha na Yeye akajaa na kuanza kuongea hata mambo mengine yasiyohitajika kwa ' hadhira ' ambayo muda mwingine pia yanamuharibia kama Kiongozi Mkuu wa nchi.
 
Sasa watamdhibiti vipi wakati akisoma. Labda useme wamsomee lakini alishasema yeye kusoma hotuba aliyoandikiwa huwa anaona siyo yeye anayeongea isipokuwa anasema maneno ya wengine ndio maana huwa hapendi kusoma za kuandikiwa.
Hata mimi nakubaliana na hoja hii. Kusoma zilizoandikwa ni sawa na una kiu ya maji halafu maji anapewa mwingine anywe huku wewe unamwangalia. He itakata kiu chako?
 
Back
Top Bottom