Gerson Msigwa: Chanjo za COVID-19 kuanza kutolewa kuanzia Agosti 2, 2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Zoezi la chanjo litaanza kutolewa kesho kuna vituo kama 550 vilivyoandaliwa, chanjo hazijaleta madhara kwa waliotumia kama tulivyokuwa tunasikia. Chanjo zitaendelea kuletwa baada ya zile dozi milioni 1 kuna nyingine zitaendelea kuletwa

Vilevile Msigwa amesema Madiwani wa Halmashauri ambazo mapato yake si makubwa na zipo Daraja A wameanza kulipwa mishahara

Gerson Msigwa amesema madiwani wanalipwa moja kwa moja kutoka hazina

Madiwani wanalipwa Tsh. 300,000 huku mwenyekiti wao akilipwa Tsh. 400,000
 
Madiwani wa halmashauri ambazo mapato yake si makubwa na zipo Daraja A wameanza kulipwa mishahara

Gerson Msigwa amesema madiwani wanalipwa moja kwa moja kutoka hazina

Madiwani wanalipwa Tsh. 300,000 huku mwenyekiti wao akilipwa Tsh. 400,000
Madiwani wa Chama gani?
 
Walipane hata milioni 100 kwa mwezi hao madiwani wote ni MATAGA wanapeana wenyewe kwa wenyewe!
 
Mama aache uonevu jamani, sh 300,000 tu? Si angewapa angalau nusu ya anacholipwa mbunge?

Sisi wananchi tupo, aendelee kutukamua, akimaliza damu, aendelee mpaka ahakikishe maji maji yametoka, hatuna shida sisi!

Kamua mama, kamua mama....by J.Nature
 
''Zoezi la chanjo litaanza kutolewa kesho kuna vituo kama 550 vilivyoandaliwa, chanjo hazijaleta madhara kwa waliotumia kama tulivyokuwa tunasikia. Chanjo zitaendelea kuletwa baada ya zile dozi milioni 1 kuna nyingine zitaendelea kuletwa''- @MsigwaGerson

#MsemajiWaSerikaliPress
Waanze na Baba Askofu Mkuu Mbeba Maono Dr. Mhe.
 
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Zoezi la chanjo litaanza kutolewa kesho kuna vituo kama 550 vilivyoandaliwa, chanjo hazijaleta madhara kwa waliotumia kama tulivyokuwa tunasikia. Chanjo zitaendelea kuletwa baada ya zile dozi milioni 1 kuna nyingine zitaendelea kuletwa

Vilevile Msigwa amesema Madiwani wa Halmashauri ambazo mapato yake si makubwa na zipo Daraja A wameanza kulipwa mishahara

Gerson Msigwa amesema madiwani wanalipwa moja kwa moja kutoka hazina

Madiwani wanalipwa Tsh. 300,000 huku mwenyekiti wao akilipwa Tsh. 400,000
Mbona anarukaruka, mara chanjo mara madiwani, inaonekana hana cha kuandika, mishahara ya madiwani inatusaidia nini sisi? Huduma za maji, umeme na barabara hakuna yeye anaona mishahara ndiyo jambo muhimu kuandika
 
HUYU GERSON MSIGWA WAKATI WA HAYATI MAGUFURI ALIKUWA ANASEMA CHANJO SIO SALAMA
Wanafiki hawajifichi, wanatambulika, tazama mdomo wa Msigwa, tazama macho yake, ukiwa makini utajua ni mchumia tumbo
 
Back
Top Bottom