Muuza viatu
JF-Expert Member
- May 14, 2020
- 3,839
- 7,924
Kama ilivyotokea kipindi cha Obama pale 2006 alipoahidi kulifunga gereza la Guantanamo hatimaye Biden nae ameahidi kulifunga ndani ya hiki kipindi chake cha uongozi. Obama baada ya kuahidi kulifunga akachukua hatua kadha wa kadha ikiwemo kuwahamisha baadhi ya wafungwa lakini alikwama baada ya kukosa kuungwa mkono na bunge ambalo kwa kiwango kikubwa lilidhibitiwa na Republican.
Gereza la Guantanamo linapatikana katika visiwa vya Cuba katika eneo ambalo wamarekani walipewa na Cuba kama zawadi baada ya Cuba kushinda vita kati yake na uhispania iliyotokea mwaka 1903 ambapo Marekani alitoa msaada mkubwa kwa Cuba.
Hili gereza limekuwa likilalamikiwa na jamii ya kimataifa kwa kukiuka haki za kibinaadamu kwa kipindi kirefu labda hatimaye linaweza fungwa.