Gerald Hando muombe msamaha Dr. Ulimboka

Gerald Hando muombe msamaha Dr. Ulimboka

frozen

Senior Member
Joined
Aug 12, 2010
Posts
135
Reaction score
32
hamna shaka kwa namna moja au nyingine kupigwa na kutekwa kwa dokta ulimboka kunatokana maneno ya kuhamsha na kuchochea hasira kwa dkt ulimboka yaliyofanywa na kituo cha radio cha clouds fm ktk kipindi cha power breakfast,segment ya jicho la ngombe majuzi,bwana gerald hando kwa makusudi au kwa kutokujua impact ya radio kwenye kurusha maneno ya chuki na kumkosoa mtu tena kwa kumuita jina lake moja kwa moja bila kufikiria reactions na response za watu kwa mtu husika. bwana hando alimsema sana bwana dkt ulimboka kwamba anapenda sifa, umaarufu,anatakuwa shujua ili sanamu lake liwekwe muhimbili..na maneno mengi ya ajabu ajabu, ambayo mtu yeyote ambaye ameguswa na mgomo wa madaktari angeweza fanya kitu chochote kumdhuru dkt ulimboka. Gerald hando na watangazaji wa radio clouds fm kuweni makini na lugha zenu, acheni unafiki, kumbukeni hata kama mnadhani hakuna watu wanaoweza kuwachukulieni hatua , hasira za watu na malalamiko yao kwenu personaly si jambo jema, wote tunajua mambo ya hovyo yanayofanywa na serikali, na hata serikali kama inashindwa tatua maombi ya madaktari kwa wakati mmoja. waonyeshe tu commitment ya dhati ya kutatua kero za madaktari tusingekuwa na migomo hii, plz gerald hando , angalia maneno yako brother , radio ni very powerful too , inaweza kuwa very destructive isipotumiwa kwa weredi
 
Nilimsikiliza kwa uzuri sana Gerald Hando kwenye kile kipindi,Hando kama Hando alikuwa anatumia haki yake ya kikatiba kama Mtanzania yeyote wa kawaida isitoshe kilichosemwa na Hando kinaweza kuwakilisha mitazamo ya watu wengi sana including I, myself, ni kwa vile tu hatuna pa kusemea tukasikika na wengi kama Hando,ni lazima tukubali watu wameathirika sana kutokana na hii migomo ya madaktari,kama haukukugusa wewe ksbb una uwezo wa kwenda Hospital kubwa za Private ukafikiri kila mtanzania ana uwezo huo...anyway nisimsemee ngoja aamue mwenyewe kama anafikiri analazimika kuomba radhi kwa maoni yale.
 
Nimekupata mkuu. "what goes around comes around". Ukimtenda ubaya mwenzio leo, ipo siku nawe utandewa ubaya pengine wa kiasi kikubwa kuliko kile ulichomtendea mwenzio. Hata kama Ulimboka anatafuta sifa, kwani hando ni msemaji wa serikali au wizara ya afya na ustawi wa jamii? Kwa msomi aliyepewa dhamani ya kutangaza kwenye chombo cha habari kama clouds, naamini ana uwezo mzuri wa kuchambua mambo hasa yanahusiana na matumizi yasiyokuwa ya lazima yanayofanywa na serikali yetu, pesa ambayo ingeweza kutumika kufanya mabadiriko makubwa katika utoaji wa huduma katika hospitali za umma. Sikusikiliza kipindi, kama kweli hando alitamka hayo, nashawishika kusema kuwa alitumiwa!!!
 
Nilimsikiliza kwa uzuri sana Gerald Hando kwenye kile kipindi,Hando kama Hando alikuwa anatumia haki yake ya kikatiba kama Mtanzania yeyote wa kawaida isitoshe kilichosemwa na Hando kinaweza kuwakilisha mitazamo ya watu wengi sana including I, myself, ni kwa vile tu hatuna pa kusemea tukasikika na wengi kama Hando,ni lazima tukubali watu wameathirika sana kutokana na hii migomo ya madaktari,kama haukukugusa wewe ksbb una uwezo wa kwenda Hospital kubwa za Private ukafikiri kila mtanzania ana uwezo huo...anyway nisimsemee ngoja aamue mwenyewe kama anafikiri analazimika kuomba radhi kwa maoni yale.

Kwa hiyo wewe nawe unawalaumu madaktari badala ya serikali? Ulitaka wafanye kazi kwa masilahi duni na mazingira magumu ya kazi? Wewe upone tu wao waumie? THINK AGAIN!
 
Anatafuta ukuu wa wilaya huyo.clds inasikilizwa na wengi,hata wakuu.lakini anasahau kuwa tv ya clouds imeonesha picha halisi ya nani aliyehusika na tukio hili maana wameirusha kwa mda mrefu sana na mambo mengi ambayo hayajaelezwa na tv zingine, clouds wameyaeleza tena kwa uwazi na picha za matukio zote zumeonekana.
Achaneni naye ya jeri muro yatamkuta.chezea magamba.
 
hando alisema ''this is personal btn u n me ulimbokal'
 
Labda Hando anaamini.....

vasco_da_gama_is_my_homeboy_mousepad-p144926090055241514trak_400.jpg
 
Hando ana msimamo ila njaa inamtoa kwenye msimamo,,adui yako mwombee njaa!
 
Anakemea mgomo,???hata yeye anafanya kazi kwenye mazingira magumu,anahofia kugoma maana hajiamini,,,,,mwenzie masoud Kipanya na Phina hawakuridhika wakagoma,,,,,kwanza wamekufa na njaa????kama wewe una taaluma na vitendea kazi vya taaluma hupati ufanisi wa kazi utatokea wapi????
Labda huyo Mr PB aseme hapa kwanini walitaka kugoma baada ya kupata shida ya kumhoji baloz wa US???KWANINI WALIAZIMIA KUGOMA????
 
Hando hajakosea na aliyempa kichapo hando hakufanya makosa, unajuwa ni maelfu mangapi ya wagonjwa wanaoteseka kwa fitna zake. Akipona tumuone aendelee na ufataani wake.
 
Nahisi yalikuwa sio maneno ya Hando bali inawezekana alitumwa au kusukumwa NA njaa!!
 
Shetani ni yule anaehamasisha wenzake wagome na kuwatesa wagonjwa wetu, huyo alikuwa hafai hata kuishi.
Hizi akili za kuunganishaunganisha taabu kweli. Hivi hata madaktari waki vunja mgomo wao na kurudi kazini hatafu hakuna dawa, vifaa vya kutibia hakuna,wagonjwa wanalala mzungu wa nne na kuambukizana magonjwa ina faida gani?
 
Back
Top Bottom