George Marato awekwa chini ya ulinzi

George Marato awekwa chini ya ulinzi

MpiganiaUhuru

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Posts
777
Reaction score
912
Taarifa ambazo sijathibitisha zinasema kuwa mwandishi na ripota maarufu toka kanda ya Ziwa George Maratu amewekwa lockup baada ya kumkata kwa panga dereva taxi mmoja ambaye alimtuhumu kutembea na mkewe.

Inasemekana pia ameichakaza taxi aliyokuja nayo dereva huyo kwa mapanga kiasi cha kuiharibu vibaya!

Taarifa zaidi zinatonya kuwa kumekuwa na ugomvi kati yake na mkewe huyo kiasi kwamba leo mwanamke alimpigia simu dereva taxi anayetuhumiwa aje kumchukua na kumrudisha kwa wazazi wake ndipo yalipotokea masahibu hayo baada tu ya dereva taxi kufika kwa lengo la kumchukua mwanamke ambaye alisha-pack vyake!
View attachment 519251View attachment 519253

Kada wa CCM na mwandishi wa kituo cha ITV mkoani Mara anayetambulika kwa jina la George Marato anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kufanya fujo na kuvunja vioo vya gari kama inavyoonekana kwenye picha.
 
Siwezi kumlaumu George Marato.Na Hata kuuwa angeweza kuuwa kabisa.

Issue ya mahusiano ni ngumu si rahisi kama unavyoichukuliwa.

Tofauti ya mahusiano kati ya MTU na MTU ni jinsi ubongo wako ilivyoyapa uzito na kuyathamini.
 
nasubiri uthibitishe ndio nitarudi kucomment
 
duh! tuanzishe darasa la ushauri sass au makanisa na misikiti waongoze bidiiiii
 
Tatizo mapenzi mnayapa kipaumbele mno utafikiri sijui ni nini.....?!

Wa kuoa mwenyewe ulimtafuta kwa shida eti upate mrembo wakutambue, haya ndio mazara yake, nani kakwambia warembo ni wa kuwapa hifadhi kwa ndoa?
 
Ni udhaifu mkubwa kumpiga mtu anayekuibia mpenzi wako. Ukiona unaibiwa, mchawi ni mpenzi wako-sio anayekuibia.
Kwa kweli, mimi faster tu, aende zake ili awe huru na huyo jamaa, yaani wanawake wote hawa hadi wanafika hatua ya kutembea uchi barabarani ili tu watushawishi eti nije kumng'ang'ania mmoja tu! Akwende huko!
 
Back
Top Bottom