Baljurashi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 2,236
- 3,703
Mohamed alikua na maneno machafu na mdomo mchafu sana, alimdhalilisha sana Joe Frazier kwa kumuita nyani, yeye akawa anajifananisha na wazungu kisa kua light skin ama kua na light complexion na kusema Joe Frazier ni Nyani kisa yeye ana weusi zaidi kuliko yeye.
Mohamed Ali kwa ujumla alikua mtu wa hovyo. Mohamed Ali na Michael Jackson ni watu ambao jamii ya weusi tunapaswa kuwalaani na kuwakana kwenye jamii yetu. Ni watu wa hovyo kabisa.
Mbona husemi kuwa Muhammad Ali alimuomba radhi Joe Frazier kwa zile "trash talks"? Au hujui kwamba aliwahi ku regret na kuomba radhi?
Halafu eti jamii ya watu weusi wamlaani Ali!!? Wewe unaweza kufanya harakati za kutetea weusi hata kidogo kama za Ali? Wewe una mchango gani kwa watu weusi kumfikia Ali?
Mtu aliyepata misukosuko na hata ku risk career yake kwa sababu ya kukataa kujiunga na Jeshi kwenda kupigana Vietnam.
Siupendi mchezo wa masumbwi wala siuungi mkono ila acha chuki binafsi dhidi ya Muhammad Ali.
Allah Amsamehe madhambi yake na Amrehemu.