Ndio maana naona katiba yetu ina mapungufu na inafaa iangaliwe upya,tabia ya siri siri ktk uwekezaji hapa Bongo inazidi kulitafuna taifa letu vibaya sana. Eeee Mungu tupe watanzania ujasiri wa kutambua na kuzuia mali ulizotupa tangu ulipoiumba dunia zisiendelee kuporwa na mabeberu wakishirikiana na watanzania wenzetu.
Najua kuapa ni dhambi lakini kwa hili naapa" HAIWEZEKANI RAISI WA MAREKANI AJE BONGO KWA ISSUE ZA CHARITY TU" eti chandarua, cancer nk nk!!!!!kumbukeni Marekani haina rafiki wa kudumu, wanachoangalia ni maslahi tu.