Genge la Kihalifu la Sabaya, ni kweli Hayati Magufuli hakulijua? OCD Hai unafanya nini kazini mpaka muda huu?

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Ni maswali tata sana mbayo tungependa kumuuliza Shujaa. Ni kweli hakujua kuwa mteule wako anatuhumiwa na kufadhili genge la kihalifu?

-Kama alijua basi kuna haja ya wananchi Kufungua kesi dhidi ya Rais wa JMT aliyepita kwa kubariki kufanyika uhalifu dhidi ya binadamu kwa raia alioapa kuwalinda.

-Kama si kweli basi kuna haja ya watu wanaohusika na Intelijensia kwa viongozi ya usalama na vetting kuwajibika kuanzia TISS mpaka jeshi la polisi.

-Mpaka muda huu sidhani kama OCD wa hai anapaswa kuwa ofisini kwa hili suala la mkuu na swahiba wake.

-Tume ya maadili ya watumishi wa umma mmetukosea sana watanzania, KUWAJIBIKA NI MUHIMU SANA

2773304_FB_IMG_1620938613111.jpg
 
Ni maswali tata sana mbayo tungependa kumuuliza Shujaa. Ni kweli hakujua kuwa mteule wako anatuhumiwa na kufadhili genge la kihalifu?..
wote hao utakuwa unawaonea tu..

enzi hizo za mwendazake, yy ndiye sheria, yy ndiye katiba na vettung yy ndio anaifanya hata kama uliowataja walimwambia hafai

nao wanafamilia zinawasubiri, wapingane naye ile kwao?
hata ww ungeweza?
 
Jiwe alikuwa ni katiri na alitafuta makatiri wenzie waonee raia... Ukatiri wa Jiwe nadhani ni wa kutisha sana hawa kina Saba na Makondakta ni sehemu tu ya mifano ya ukatiri wa Jiwe... nilisikia Jiwe alishampasua mtu kwa risasi ya kichwa kikapasuka ndani ya white house... isije kuwa ndie saa 8 masikini... jiwe alitakiwa nae awe ndani pamoja na genge lake la kikatiri ikiwezekana mwili wake ufukuliwe upelekwe lock up
 
Ben Saanane alipotekwa na kupotezwa, wengi walipiga kelele na pia kukawepo watu wanaotuhumiwa. Kile kimya cha mwendazake, haswa kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, ndicho kilichopelekea muendelezo wa kina Sabaya na magenge ya uhalifu.
It was a copy cat. Wengi wakijitahidi kumuiga mkuu yule wa mkoa.
 
Mtu wa Hai anaenda kusomewa mashitaka Arusha ili iweje?
Hai hamna mahakama? Na mkoa wa Kilimanjaro je?
Wameogopa mafuriko ya watu mahakamani.

Mahakamani ni sehemu ya kutoa haki kwa hiyo ni vizuri amepelekwa huko ili sasa akina Mbowe wawe wanaenda mahakamani kutoa ushahidi juu ya madai yao.
Mbowe asipoenda kutoa ushahidi mahakamani tutajua ni unafiki tu

Hata Mbowe alikaa Segerea kwa miezi nne na madawa ya kulevya yakaisha mtaani
 
Rais wa nchi kwa mfumo wa nchi hii kila siku asubuhi anapewa taarifa za usalama wa taifa na tiss PDB , jibu alikuwa anajua kila kikichofanyika na yeye ndio aliekuwa anamtuma kupora pesa za wafanyabiashara na kumkingia kifua , hii ni kwa kifupi .
 
Jiwe alikuwa ni katiri na alitafuta makatiri wenzie waonee raia... Ukatiri wa Jiwe nadhani ni wa kutisha sana hawa kina Saba na Makondakta ni sehemu tu ya mifano ya ukatiri wa Jiwe... nilisikia Jiwe alishampasua mtu kwa risasi ya kichwa kikapasuka ndani ya white house... isije kuwa ndie saa 8 masikini... jiwe alitakiwa nae awe ndani pamoja na genge lake la kikatiri ikiwezekana mwili wake ufukuliwe upelekwe lock up
Kwa mujibu wa member mmoja humu, ilikuwa ni Saa 8
 
Mtu wa Hai anaenda kusomewa mashitaka Arusha ili iweje?
Hai hamna mahakama? Na mkoa wa Kilimanjaro je?
Wameogopa mafuriko ya watu mahakamani.

Mahakamani ni sehemu ya kutoa haki kwa hiyo ni vizuri amepelekwa huko ili sasa akina Mbowe wawe wanaenda mahakamani kutoa ushahidi juu ya madai yao.
Mbowe asipoenda kutoa ushahidi mahakamani tutajua ni unafiki tu

Hata Mbowe alikaa Segerea kwa miezi nne na madawa ya kulevya yakaisha mtaani
Una akili za kitoto. Sasa ni kitu gani umeandika?
 
Mtu wa Hai anaenda kusomewa mashitaka Arusha ili iweje?
Hai hamna mahakama? Na mkoa wa Kilimanjaro je?
Wameogopa mafuriko ya watu mahakamani.

Mahakamani ni sehemu ya kutoa haki kwa hiyo ni vizuri amepelekwa huko ili sasa akina Mbowe wawe wanaenda mahakamani kutoa ushahidi juu ya madai yao.
Mbowe asipoenda kutoa ushahidi mahakamani tutajua ni unafiki tu

Hata Mbowe alikaa Segerea kwa miezi nne na madawa ya kulevya yakaisha mtaani
Makosa mengi alifanya Arusha.Nini tatizo?
 
wewe unasikia sabaya alikuwa anateka watu alafu unauliza kama magufuri hakuwa anajua.
Magufuri ndio muanzilishi wa ushenzi wa namna hii hapa nchini.

watu walikuwa wanatekwa nyakati za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, lakini basi walikuwa wanapiga japo mikwara mbuzi, lile bwege lenyewe lilikuwa linashangilia kabisa
 
Ushahidi wote RC Anna anao ila NI dharau tu kwakuwa alitokea upinzani.Kwani aliwaonya sana OCD NA DC

Huyo mama nae alipokuwa RC pale Kilimajaro alikuwa very weak ndio maana hakuwa na impact; hasa kwa Wilaya ya Hai, alipelekewa malalamiko mengi dhidi ya afisa Ardhi wa Hai kuwa corrupt lakini alishindwa kumchukulia hatua ingawa alikuwa anajua ukweli wa mashitaka hayo!
 
Kwa mwendazake, Sabaya alikuwa juu ya mama. Nashangaa hilo umeshindwa kuliona.
 
Kwa hili nawaza sana kuhusu Hayati JPM, aliwezaje kuona na kujua kwamba chanjo za COVID, BARAKOA ni hatari kwa Watanzania ila asijue uhalifu wa huyu Jambazi, JPM alikuwa anaipeleka hii Nchi kubaya sana, nina uhakika Mungu wa mbinguni aliona hili akaamua kutuepusha na shari mapema.
 
Hakuna Rais aliekua akifuatilia "A - Z" mienendo ya wateule wake kama Magufuli, hata Nyerere hamfikii. Magufuli ilifikia hatua alikiri mbele ya vyombo vya habari kwamba anawafuatilia mpaka maongezi yao kwenye simu.

For that case, alikua anajua yote Ole Sabaaya aliokua akiyapanga kufanya, hata kabla hajayafanya.

Chini ya kapeti:

Ole Sabaaya aliwahi kumuibia kwa nguvu mfanyabiashara wa Arusha Million 300, mwezi September 2020, ishue ilifika Chamwino na akaitwa kujieleza kwa mtukufu.

Alichosema ni kwamba "Kweli mzee nimechukua kiasi hicho, ila ni kwaajili ya kujiandaa na uchaguzi mkuu huu unaokuja 2020, nimefanya hivyo kukisaidia Chama ili kisitumie hela nyingi kanda ya kaskazini, na nakuahidi Mbowe namuangusha uchaguzi huu. Harudi bungeni. Hizi hela nimechukua kutoka kwa mfanyabiashara anaempa Mbowe jeuri ya kampeni ili nimuangushe Mbowe".
 
Ni maswali tata sana mbayo tungependa kumuuliza Shujaa. Ni kweli hakujua kuwa mteule wako anatuhumiwa na kufadhili genge la kihalifu?
Kuna kina Sabaya kibao humu nchini, enzi za hayati hapakuwa na utawala wa kisheria, kuwalaumu waliopaswa kuchukua hatua ni kuwaonea. Yote yaliyo fanywa na akina 'Sabaya' yalikuwa na full backings ya marehemu.

Tabora alipo elezwa mabaya yaliyo fanywa na akina Sabaya wa mkoa huo aliwaita wenyeji wa Tabora ni wenye majungu. Kauli ya mh SSH ya 'tuanze upya' ina maana kubwa.
 
Back
Top Bottom