Gen. David Musuguri apewe fadhila yungali hai

L/cruiser LC 300 itaishi vizazi vingapi vijavyo kama alama ya kutambua mchango wake na uzalendo wake kwa nchi na jeshi? Kwa watendaji wenye matokeo makubwa ya kazi official car siyo motisha/motivation.

Majenerali/Makamanda wenzake wote alioongoza nao vita wametangulia mbele ya haki je, L/Cruisers walizopewa enzi za uhai wao zinaweza kuwatambua leo?!
Hivi unayajua maslahi ya mkuu wa majeshi mstaafu kweli?
 
Duh! Jana tu nimetoka kumsoma huyu jamaaa aliongoza vikosi vya TPDF dhidi ya Waganda, Walibya na Wapalestina.

Aloo anastahili recognition
Kuna Waganda fulani hivi kabila la Idi Amin la Kakwa nilifanya nao kazi, wanasimulia kwamba Amin aliwahi kusema akiwa Saudi Arabia ukimbizini kwamba Afrika hii askari mahiri pekee anayestahili kupewa kamisheni ya Field Marshal baada ya yeye ni Gen. David Musuguri.
 
Mji huo umekongoroka utadhani hajawahi kuishi pale CDF..... Kama familia haipawezi basi jeshi lipafanye pawe makumbusho...

Au GENTAMYCINE unasemaje kuhusu babu yako huyu?
Nina mengi ya Kumuongelea huyu Babu yangu ambaye alitupenda mno na Marehemu Dada yangu tokea tukiwa Wadogo huku tukipanda nae Ndege ya Jeshi kwenda nae Kutembea Mbugani Serengeti.

Kwa Heshima yangu Kubwa Kwake tafadhali naomba nisiseme yaliyopelekea nyie na Wengi wenu kuyaona hayo Mapungufu japo kwa Kiduchu tu niseme lawama zangu nyingi nazipeleka kwa Wanafamilia wake ( hasa Watoto ambao 55% wako JWTZ huku baadhi yao wakiwa hawatumii Jina la Musuguri ) na Wengine wakiwa System ( SSIT )

Pongezi nyingi sana kwa JWTZ kwa Kumpa kila Huduma, Upendo na Kumjali CDF Mstaafu Babu Jenerali David Bugozi Musuguri na hakika hawana Deni na Sisi Wazanaki na wana Mkoa wa Mara ( Musoma ) na kwa Niaba yao nasema Asante JWTZ na hasa CDF wa sasa Mweledi na Mpiganaji Aliyetukuka Jenerali John Mkunda.
 
Gen. David Bugozi Musuguri (103) rtd CDF amezawadiwa nini kwenye sherehe za miaka 62 ya uhuru? Miaka 44 ya vita ya Kagera? Miaka 46 ya utumishi jeshini (1942-1988)?

Vita alivyopigana:-

1. WW II 1942
-Battle of Madagascar

2. Uganda - Tanzania 1978-1979
-Battle of Simba Hills
-Battle of Masaka
-Battle of Lukaya
-Operation Dada Idi

NB.
Pana haja ya serikali kumpa alama ya kumbukumbu (souvenir) kufuatia pia kuwa ndiye Kamandaa pekee wa TPDF aliyepigana Kagera ambaye yungali hai na mwenye umri mkubwa kuliko muasisi wa taifa hili. Kiongozi huyu ni alama na fahari ya Tz, KAR na TPDF.

Ramani inaonyesha jinsi TPDF ilivyosambaza vita Uganda nzima na mishale kuonyesha njia za wapiganaji wa jeshi la adui la Uganda walipotorokea.

View attachment 2845166

Ramani kwa hisani ya Goran tek-en.
Kiwango chake cha juu kabisa cha elimu?
 
Kiwango chake cha juu kabisa cha elimu?
Kuna ngazi nyingine ya elimu-jeshi imebaki zaidi ya (kuliko) ujenerali?

Magufuli aliamua kuiingiza Tanzania Military Academy TCU, hivi sasa digrii inazotoa pale ikiwemo ya Military Science inatambuliwa na TCU.
 
Nina mengi ya Kumuongelea huyu Babu yangu ambaye alitupenda mno na Marehemu Dada yangu tokea tukiwa Wadogo huku tukipanda nae Ndege ya Jeshi kwenda nae Kutembea Mbugani Serengeti.

Kwa Heshima yangu Kubwa Kwake tafadhali naomba nisiseme yaliyopelekea nyie na Wengi wenu kuyaona hayo Mapungufu japo kwa Kiduchu tu niseme lawama zangu nyingi nazipeleka kwa Wanafamilia wake ( hasa Watoto ambao 55% wako JWTZ huku baadhi yao wakiwa hawatumii Jina la Musuguri ) na Wengine wakiwa System ( SSIT )

Pongezi nyingi sana kwa JWTZ kwa Kumpa kila Huduma, Upendo na Kumjali CDF Mstaafu Babu Jenerali David Bugozi Musuguri na hakika hawana Deni na Sisi Wazanaki na wana Mkoa wa Mara ( Musoma ) na kwa Niaba yao nasema Asante JWTZ na hasa CDF wa sasa Mweledi na Mpiganaji Aliyetukuka Jenerali John Mkunda.
Umeanza!!...

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Huyu CDF aliifanyia nini Tanzania mbona kila siku kelele za Musuguri tu. Wakati wa vita ya Kagera CDF wetu alikuwa Abdallah Twalipo sio huyo Pimbi.
 
..kambi mojawapo ya jeshi inatakiwa ipewe jina lake.

..kuna kambi ya jeshi pale Temeke imepewa jina Abdalah Twalipo kumuenzi Cdf wa pili wa Jwtz.

..huo ndio utaratibu unaotumiwa na majeshi mengi duniani kuwaenzi makamanda wao wa ngazi za juu.
 
Back
Top Bottom