Geita: Waziri Mkuu Majaliwa, afungua Ofisi za TRA Chato

So unataka kufananisha kwa Pesa mbili na Chato...aa bwana acha utani? Holili border inaingiza fedha zaidi ya Chato na huko Kwa Mramba kumeendelea kuliko hata Geita. Kuna ma-lodge ya kufa mtu ukiacha Tarakea inayopaswa kuwa mji. Mngekuwa na akili mngemsisitiza awajengee viwanda mpate kujikimu maana uwanja hamtaweza hata kumudu tiketi ya ndege.
Punguani wahedi. Huko shule huwa mnaenda kusomea Ujinga!? Umesoma vizuri nilichoandika au unafukunyuka tu!!??? Nimeongea enzi za Mramba kupeleka miradi ya Maendeleo miaka ya nyuma pengine hata ulikuwa haujazaliwa. Na huo upuuzi wote uliotaja kwa sasa miaka hiyo kulikuwa hakuna kitu. Chuki itawamaliza awamu hii. Vumilieni bado miaka Nane (8).
 
Wabantu wanaweza mambo matatu, kushibisha tumbo, kuridhisha maeneo yale ya kikolomije na kusema uongo basi. Mengine yote tuwaachie ngozi nyeupe. Huo ndio ukweli.
 
Mwacheni naye ana kwao, mbona waliopita nao walijenga makwao tatizo ni nini?
Aisee si kwa gharama ya kodi yetu kwa miradi tembo mweupe kama Chato International Airport. Ajenge hospitali na shule kwanza huko kwao kuondoa magonjwa na ujinga, umeona maoni ya watalii wanakuja Tanzania juu ya miundombinu yetu? Kumbuka utalii unaongoza kwa kuingiza fedha za kigeni.
 
Punguani wahedi. Huko shule huwa mnaenda kusomea Ujinga!? Umesoma vizuri nilichoandika au unafukunyuka tu!!??? Nimeongea enzi za Mramba kupeleka miradi ya Maendeleo miaka ya nyuma pengine hata ulikuwa haujazaliwa. Na huo upuuzi wote uliotaja kwa sasa miaka hiyo kulikuwa hakuna kitu. Chuki itawamaliza awamu hii. Vumilieni bado miaka Nane (8).
Barabara ya Pesambili ilijengwa kipindi cha Kikwete na pesa zilizotolewa na wahisani wa BADEA baada ya kupitia feasibility study na kuona umuhimu wake. Wakati uwanja wa Chato unajengwa kwa amri ya Magufuli nje ya Bunge chini ya 150 km toka Jiji la Mwanza kwenye mradi wa uwanja mwingine wa kimataifa. Huko Kwa Pesambili kuna Watalii kila siku wanapanda milimani ukiacha wakazi wa upande wa Kenya kuja kwa matibabu na kujipatia mahitaji yao upande wa Tanzania Holili na Tarakea. Msilazimishe mambo kwa uongo uongo..
 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa afungua ofisi za TRA, Wilaya ya Chato, mkoa wa Geita
View attachment 529002
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikata utepe kama ishara ya kufungua jengo jipya la ofisi ya TRA, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita katika ufunguzi uliofanyika leo mjini Chato.
View attachment 529001
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akihutubia wananchi wa Chato wakati wa ufunguzi wa jengo la TRA wilayani humo mkoani Geita leo.
View attachment 528999
Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere akitolea maelezo ya kina kwa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa namna jengo la ofisi ya TRA Chato litakavyoweza kuchochea ukusanyaji wa mapato katika Wilaya ya Chato.
View attachment 528998
Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa maagizo kwa watendaji wa TRA mara baada ya kupata maelezo ya jengo la ofisi ya TRA kutoka Meneja wa TRA wilaya ya Chato Abdallah Mtumwa
View attachment 528997
Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya TRA katika uzinduzi wa ofisi hiyo uliofanyika leo katika wilaya ya Chato, mkoa wa Geita

Katika Hotuba yake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutowatoza kodi ya majengo wazee walio na umri zaidi ya miaka 60.

====

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa,amesema kuwa kila mwananchi wa Tanzania anawajibika kulipa kodi kwaajili ya ujenzi wa Taifa na kwamba uchumi utajengwa na watanzania kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa kwani kufanya hivyo itawaza kusaidia upatikanaji mkubwa wa kodi.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa zinduzi wa Jengo la mamlaka ya mapato nchini(TRA)Wilayani Chato Mkoani Geita, ambalo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha Sh ,Bilioni 1.4.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa Kila mwananchi ambaye anastahili kulipa kodi la lazima alipe bila ya kushurutishwa kwani ni jambo la kawaidia na kwamba nchi ambazo zimeendelea ni kutokana na wananchi wake kujenga destuli ya ulipaji wa kodi

Pia ameendelea kueleza kuwa Kutokana na maelekezo ya Ilani,Katika Mwaka 2016/17 Kuanzia Mwezi Julai,2016 hadi kufikia mwezi Aprili ,2017 Serikali imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilion 20.7 Sawa na Asilimia 70.1 na kwa lengo la mwaka walijiwekea malengo ya kukusanya Sh,Trilion 29.5,Kati ya makusanyo hayo mapato ya ndani ya kodi yalikuwa ni Sh,Trilioni 11.6 Sawa na Asilimia 77.1 ya lengo la kukusanya Sh,Trilion 15.1

Aidha Waziri Mkuu ametoa Wito kwa Kila mwananchi kuakikisha anadai na kupewa Risiti ya manunuzi ya bidhaa alizonunua na kwamba TRA ihakikishe kila mfanyabishara anakuwa na mashine za kielektroniki.


Kamishina wa mamlaka ya mapato TRA Charles Kichere amesema kuwa Pamoja na kuboresha miundo mbinu ya majengo Mamlaka imeanzisha mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia za kielekitroniki ambazo zitaunganishwa na ofisi hiyo ili kutoa huduma kwa urahisi kama ilivyo kwenye ofisi zingine kote nchini.

"Baadhi ya huduma zitakazotolewa hapa ni kama; Utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), utoaji wa leseni za udereva, huduma za usajili wa magari, ukusanyaji wa kodi za majengo, na kodi zinginezo ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mujibu wa Sheria"Alisema Kichere.

"Haya yote yanafanyika kwa lengo la kuhakikisha kodi na tozo mbalimbali zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinakusanywa kikamilifu ili kufikia lengo la makusanyo yanayokusudiwa katika mwaka ujao wa Fedha na kuendelea"Aliseongeza Kichere.

Jengo hilo ambalo limefunguliwa leo lilianza kujengwa mnamo tarehe 13 Julai, 2016 na kumalizika tarehe 12 Juni, 2017 ambapo kazi ya ujenzi ilihusisha ujenzi wa jengo la ghorofa moja kama ambalo lina nafasi ya kutosha kutoa huduma zote za kodi pamoja na huduma za kibenki ili kuwapunguzia adha walipakodi kwa kupata huduma zote mahala pamoja.

Kampuni ambayo imejenga jengo hilo ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)na mjenzi ni kampuni ya Mayanga Constructions ambapo katika ujenzi huu zimetumika kiasi cha Takriban Shilingi Bilioni 1.4.

Credit kwa Mkuu Maduka

Majaliwa k Majaliwa Tafadhali sahihisha siyo Kassim Majaliwa Majaliwa
 
chato nimefika,hii yote ni upotevu wa hela na ulimbukeni ndugu zangu,chato kuna traffic lights inaweza kupita lisaa limoja hakuna hata gari lililopita taa zinacheza segere tu,wakati jiji la mwanza lina taa za kuongoza magari sehemu mbili tu,pale karibu na salam cone na kule buzuruga....Its so funny chatto wanategemea sijui uvuvi wa dagaa sasa hivi wanapelekewa madude ambayo yalitakiwa yawe kule geita makao makuu ya mkoa,hii ni white elephant kama kile kijiji alichojenga dikteta mobutu seseseko cha gdabolite,alivyoondoka madarakani mchezo ukaisha sababu economically hakukuwa na maana,kiongozi pendelea kwako lakini kuwe na manufaa basi ,kwa mfano ingekuwa sehemu kama iringa au sirari ningeelewa
 
Ni bora uyaambie maboya ya huko. Wanahitaji kutengenezewa ajira kabla ya vitu vya anasa kama uwanja wa ndege na traffic lights. Miaka 10 si mingi watakuja kufahamu tunachoongea jamaa aking'atuka

Geza Ulole

Heshima kwako mkuu!..... Natambua wanajua ukweli ila wametumwa kukitetea chama
 
So unataka kufananisha kwa Pesa mbili na Chato...aa bwana acha utani? Holili border inaingiza fedha zaidi ya Chato na huko Kwa Mramba kumeendelea kuliko hata Geita. Kuna ma-lodge ya kufa mtu ukiacha Tarakea inayopaswa kuwa mji. Mngekuwa na akili mngemsisitiza awajengee viwanda mpate kujikimu maana uwanja hamtaweza hata kumudu tiketi ya ndege.
Kwanza huyu Jamaa amedanganya..... Usangi kwa kina Msuya lami imeanza kupanda 2007 hivi wakati huo Msuya ameshatoka madarakani...


Kuhusu umeme kweli ulifika kwenye miaka ya 70's hivi


Rombo na Chato ni viwili tofauti.... Tarakea kumechanganya kushinda hata hiyo Geita achilia mbali Chato.
 
Punguani wahedi. Huko shule huwa mnaenda kusomea Ujinga!? Umesoma vizuri nilichoandika au unafukunyuka tu!!??? Nimeongea enzi za Mramba kupeleka miradi ya Maendeleo miaka ya nyuma pengine hata ulikuwa haujazaliwa. Na huo upuuzi wote uliotaja kwa sasa miaka hiyo kulikuwa hakuna kitu. Chuki itawamaliza awamu hii. Vumilieni bado miaka Nane (8).
Hebu taja hiyo miradi aliyopeleka ..


Maana hata Lami imeenda miaka ya 2008... Mwanzoni barabara ya Tarakea ilikuwa ni vumbi tu
 
Itajilipa tu huko mbeleni vumilieni mkuu.
Mh. Kikwete alipojenga kiwanda cha kisasa Chalinze cha kutengeneza dawa za kutokomeza mbu mlibeza na kulia sanaaa. Leo hii wote tunaona faida yake. Vumilieni mkuu huwezi jua unaweza kuhitaji huduma ya TRA Chato siku za mbeleni. Karibu Uji wa iliki yakhe.
Chalinze mji..mkongwe hata bila Jakaya unabebeka
 
Hivi hii ofisi ingejengwa Arusha au Kilimanjaro tungefanya hizi kebehi na lawama? Hivi kwa nini kuna Watu wanaamini kwamba wao ndo wenye haki ya kula mema ya nchi hii peke Yao? Ukweli in kwamba hata ingejengwa kibondo au namtumbo I don't care. Kote wanaishi watanzania. Kwamba hakuna economic activities kujustify hiyo investment, possibly yes, lakini ni fursa Kama hizo ndo zitaleta maendeleo. Tukubaliane kuna Mikoa na wilaya imetengwa sana nchi hii as if wao siyo wananchi WA taifa hili. Wengine mkijengewa airports, hotel na kumbi za kimataifa.....it's all good. Kwa sababu mmeendelea na mnastahili. As if maendeleo mlizaliwa nayo...yet hata nyinyi fursa nyingi mlizipata kwa sababu ya viongozi WA taifa hili waliokuwa wana divert miradi. Very unfair kutuaminisha kwamba wananchi WA Chato hawastahili hii ofisi. Next wakajenge Kasulu na Kakonko.
Sio mikoa yote imepata viongozi wa juu wa kitaifa sema...Geographical locations na sababu za kibiashara kihistoria....
Mikoa kama.Mwanza...Mbeya ..Arusha..Dar,Tanga,Kimanjaro inajibeba kibiashara

Ukiniambia Mkoa..ambao ulisahaulika pamoja...na..potentials nitakutajia Kigoma na Mtwara

Ukiniambia mkoa ambao...kihistoria ulikua maarufu kibiashara ukaanguka nitakuambia ni Lindi
Kilwa masoko na kilwa...kivinje tunesoma...kwenye historia toka...karne ya 13 kulikua na miji wakati Wareno...wanapita lakini walipokuja..wajerumani umaarufu wa kilwa kama..mji mkubwa ukafa ikaja Bagamoyo ambayo baadaye ikawa Dar
Mji wa Tanga ulikuwa Manispaaa kabla ya Dar na bandari ya Tanga ilikuwa busy kuliko ya Dar kutokana na kusafirisha Mkonge,chai na kahawa hadi baada kidogo ya uhuru ndio Dar ikainuka

Miaka inavyoenda...kuna...maeneo...yanaibuka mengine yanarudi nyuma na mengine stagnant
 
Akina Msuya, Mrema, Sumaye, etc. walitengeneza lami mpaka vijijini migombani huko, walisambaza umeme wa uhakika mpaka vichochoroni wakati huohuo mikoa mingine ilikuwa haifikiki kutokana na barabara mbovu, umeme na maji shida. Ilifikia kipindi wakademand kujengewa mpaka International Airport (KIA). Lakini leo amepatikana kiongozi anayejitahidi kuendeleza maeneo mengine (including eneo lake) ambayo yapo nyuma sana kimaendeleo wanamuona mbaya. How selfish are they.
KIA kajenga Mwalimu Nyerere mwaka 1967 hii pia ilichagizwa na ushauri wa world bank kwa.kuwa asilimia...kubwa ya mapato ya utalii nchii hii ambako...sasa yanakimbilia dola bilioni 2 kwa mwaka yanatokana na...wapanda...Mlima
Kwa hiyo baada ya uhuru hatua...ya kwanza ..ilikuwa kujinusuru na...watalii kupitia Nairobi ili waje kupanda mlima.

Mkitaka kujua wenzetu majirani bado wanavizia wageni wapanda mlima...wapite kwao...bado ..wanampango wa kujenga uwanja Taveta ambapo...ni kilometa...30 toka njia ya mlima...ya Marangu jambo ambalo...kuna wakati lilizaaa mgogoro mkubwa kwenye jumuia kwani ni wazi wanataka kutunyima maapato
 
Back
Top Bottom