Geita: Wassira na Mwema watimuliwa

Geita: Wassira na Mwema watimuliwa

Si kweli mi nipo Geita waliongea fresh tu il a mkuu wa mkoa ndiyo alifukuzwa msibani kwa mchungaji aliyechinjwa
 
Kuanzia leo sitosoma hili gazeti nilikuwa naliamini sana Tanzania Daima lakini kuanzia leo nimepoteza imani kabisa. Hii habari yote ni uongo kwa asilimia mia moja. Nimesikitika sana kwa kweli. Nilikuwapo Geita na Buseresere, kilichoandikwa ni iongo of the highest order. Mwema na Wassira wote hawakuwapo Geita, sababu za helikopta kutua shuleni na baadae kuondoka kwenda kutua Magereza si hizi zilizotajwa hapo. Masharti yote yaliyosemwa ni uongo mtupu. DC hakwenda msibani na wala hakupata shida yoyote. DC alikwenda msibani na Waziri Nchimbi na aliyeongea pale alikuwa ni RC Magalula na Nchimbi. Alitoa pole na kuwakumbusha wananchi wajibu wa kuepuka vurugu. Kwenye mazishi makaburini hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyekuwapo. Vyombo vya habari vinashabikia vurugu kwa kuandika uongo. Tuwe makini jamani hii chuki inayopandikizwa madhara yake yatatukumba sote hakuna atayepona. Poleni Watanzania wenzangu.
 
CCM ndio mwasisi wa udini chini .Hawakukumbuka kuwa Wakristo wamekuwa wavumulivu miaka yote, wakalianzisha. Sasa wataweza vipi kulizima? Walitumia uislam kama laverage ya kuingia Ikulu. Na ndio itakayokuwa lavarage ya kushuka na kufa moja kwa moja.

Umenena!... Ndiyo maana hivi sasa utaona baadhi ya waislamu wanashabikia CCM hata inapofanya madudu!... Hawakumbuki kuwa ni chama hiki kiki kilicho wadanganya kuwa kitaanzisha mahakama ya KADHI!... hivi sasa wanakana kama vile hawajawahi kusema hilo!
 
Kuanzia leo sitosoma hili gazeti nilikuwa naliamini sana Tanzania Daima lakini kuanzia leo nimepoteza imani kabisa. Hii habari yote ni uongo kwa asilimia mia moja. Nimesikitika sana kwa kweli. Nilikuwapo Geita na Buseresere, kilichoandikwa ni iongo of the highest order. Mwema na Wassira wote hawakuwapo Geita, sababu za helikopta kutua shuleni na baadae kuondoka kwenda kutua Magereza si hizi zilizotajwa hapo. Masharti yote yaliyosemwa ni uongo mtupu. DC hakwenda msibani na wala hakupata shida yoyote. DC alikwenda msibani na Waziri Nchimbi na aliyeongea pale alikuwa ni RC Magalula na Nchimbi. Alitoa pole na kuwakumbusha wananchi wajibu wa kuepuka vurugu. Kwenye mazishi makaburini hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyekuwapo. Vyombo vya habari vinashabikia vurugu kwa kuandika uongo. Tuwe makini jamani hii chuki inayopandikizwa madhara yake yatatukumba sote hakuna atayepona. Poleni Watanzania wenzangu.

Usipolisoma wengine tutalisoma!... Serikali inapandikiza udini mchana kweupe!... wameingia kwa udini 2010 na bado hiii ni sera ya CCM!....
 
Daaaaahhhh ningeshangaa sana tz daima isingetunga stori hii
 
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, wametimuliwa mkoani Geita, huku Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, akisulubiwa kwa masharti magumu.
Vigogo hao wa serikali walikumbwa na patashika hiyo, juzi mkoani humo walikoenda kusaka suluhu ya vurugu za kidini zilizosababisha mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila (45) wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God.

Habari za uhakika kutoka mkoani Geita zimesema kuwa mamia ya wananchi wa Geita walitishia kufanya lolote, ikiwa Wassira na Mwema wangeonekana wakati wa mazishi ya mchungaji huyo au sehemu yoyote mkoani humo.
Taarifa za uhakika zimesema kuwa viongozi wa wilaya na mkoa huo, baada ya kubaini kuwepo na hali ya hatari kwa viongozi hao, walilazimika kubadili eneo ambalo helkopta iliyowabeba mawaziri na IGP ingetua.

Uchunguzi umebaini kuwa, chopa hiyo, awali ilitua katika eneo la Kalangalala, lakini baada ya kubainika kuwepo na hali ya hatari, ililazimika kuruka na kwenda kutua katika eneo la Magereza mjini Geita.

Mawaziri hao waliandamana na Mwema, toka Dodoma kulikokuwa kunafanyika kikao cha makamishna wa polisi, makamanda wa mikoa na Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakazi wengi wa mjini Geita, hususan Wakristo, walipata taarifa ya ujio wa mawaziri hao, ndipo walipoamua kuchukua hatua hizo, na kwamba wasingekuwa tayari kuonana na Wassira kwa madai kuwa alitoa tamko lililochochea zaidi chuki baina ya waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu, huku wakimshutumu IGP Mwema kwa kuzembea kuchukua hatua kulinda usalama wa watu.

Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu Waziri Nchimbi kutumia juhudi kubwa kuwashawishi wananchi wakubali kumsikiliza kwa nia ya kupata ufumbuzi wa vurugu hizo.
Imedaiwa kwamba Nchimbi alikubaliwa kuonana na wananchi ambao walimpa masharti mazito matano aliyolazimishwa kuyakubali, kama njia ya kupata ufumbuzi.
Sharti la kwanza alilopewa, walimtaka akubali na kutamka hadharani kuwa serikali haina dini, na hivyo sio lazima kwa Waislamu tu ndio wachinje na Wakristo wasichinje.

Sharti la pili ambalo Nchimbi alipewa na kulitekeleza hapo hapo ni kuwaachia wachungaji waliokuwa wamekamatwa kwa madai ya kuchinja, wakati sharti la tatu lilimtaka athibitishe kuwa wachungaji na Wakristo wengine wataacha kunyanyaswa na Waislamu.

Sharti la nne lilimtaka Nchimbi atamke kuwa serikali itagharamia matunzo ya familia ya mchungaji aliyeuawa na mazishi yake kwa sababu kifo chake kimetokana na uzembe wa serikali kutochukua hatua dhidi ya jambo hilo pamoja na kulalamikiwa na kupewa taarifa na wachungaji kwa barua.

Hata hivyo, Nchimbi aliomba jambo hilo hususan matunzo ya familia aliwasilishe kwa wakubwa wake wa kazi, hususan Waziri Mkuu ili waweze kupata ufumbuzi wa pamoja.

Pamoja na juhudi hizo za Nchimbi, Mkuu wa Mkoa Saidi Magalula, na Mkuu wa Wilaya Ludorick Mpogolo, walikataliwa kabisa na wananchi, kiasi cha kushindwa kuhudhuria mazishi ya mchungaji huyo. Mashuhuda waliokuwepo kwenye msiba huo, wanasema Mpogolo aliyekuja kwa niaba ya serikali alizomewa hali iliyomsababisha atoe rambirambi haraka na kuondoka eneo la tukio.
Taarifa zaidi zilizopatikana zinasema Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kufika Geita leo ili kutafuta suluhu ya madhehebu hayo.

Wakazi wa kata za Buseresere na Katoro katika wilaya za Chato na Geita walilalamikia serikali kushindwa kutoa msimamo juu ya mgogoro huo na kuufanya wa kisiasa zaidi jambo lililosababisha vurugu na mauaji ya mchungaji na baadhi ya raia kujeruhiwa vibaya.

Katika vurugu hizo, mali za wananchi zimeharibiwa vibaya huku baadhi ya maduka na bidhaa zikiteketezwa kwa moto.

Miongozi mwa wananchi walioharibiwa mali zao ni pamoja na Mwenyekiti wa BAKWATA Wilaya ya Chato na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Buseresere, Yusuf Idd Banana ambaye ametaja mali zilizoharibiwa kuwa na thamani ya sh milioni 10.
Waziri Nchimbi hakupatikana kwa simu kuzungumzia hali hiyo kwa kuwa simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.



[TD="bgcolor: #ffffff"]
Wassira, Mwema watimuliwa
• Mauaji ya mchungaji Geita

na Josephat Isango


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
amka2.gif
[/TD]
 
Ufafanuzi wa Ikulu wa habari ya TanzaniaDaima - "Wassira, Mwema watimuliwa Geita"


Gazeti la Tanzania Daima la leo, Jumamosi, Februari 16, mwaka huu wa 2013 lilichapisha habari nzito kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti hilo zenye kichwa cha habari, "Wassira, Mwema watimuliwa Geita".


Katika habari hiyo, Gazeti hilo limedai kama ifuatavyo: "Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema wametimuliwa mkoani Geita…Vigogo hao wa Serikali walikumbwa na patashika hiyo juzi (Alhamisi, Februari 14, 2013) mkoani humo walikoenda kusaka suluhu ya vurugu za kidini…"


Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (DPC), Ikulu, inapenda kuwaarifu wananchi kuwa habari hii siyo ya kweli. Ni habari ya kutunga. Ni habari ya uzushi. Na kwa sababu habari hiyo ni ya uongo, ni ya uzushi na ni ya kutunga, ni dhahiri kuwa ina lengo la kuwapotosha wananchi na kudhalilisha maofisa waandamizi wa Serikali.


DPC inapenda kufafanua kama ifuatavyo:


Kwanza Mheshimiwa Stephen Wassira siyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu. Mhe. Wassira ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu.
Pili, Mhe. Rais hakwenda Geita juzi, Alhamisi, Februari 14, 2013 kama inavyodaiwa na Gazeti la Tanzania Daima. Kwa siku tatu zilizopita, Mhe. Wassira amekuwa anaandamana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika ziara ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Juzi, Alhamisi, siku ambayo inadaiwa kuwa "alitimuliwa Geita" Mheshimiwa Wassira aliandamana na Mhe. Rais katika mazishi ya Askofu Mstahivu( Bishop Emeritus) wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Baba Askofu Amedeus Peter Msarikie yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Kristo Mfalme mjini Moshi.
Jana, Ijumaa, Februari 15, 2013, Mhe. Wassira aliandamana na Rais Kikwete kumzika aliyekuwa Askofu wa Dayosisis ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Kaskazini Kati, Baba Askofu Dkt. Thomas Olmorijoi Milia Lazier yaliyofanyika Kanisa Kuu ya KKKT Dayosisi ya Arusha, mjini Arusha.
Leo, Jumamosi, Februari 16, 2013, Mhe. Wassira akiambatana na Mhe.Rais Kikwete amerejea Dar es Salaam na kwenda moja kwa moja nyumbani kwake Masaki kushiriki shughuli za msiba wa kaka yake. Na hata leo hakwenda Geita.


DPC inapenda kuvikumbusha vyombo vya habari nchini kuhusu msimamo thabiti na usionyumba wa Serikali ya Mheshimiwa Kikwete wa kuhimiza, kulea na kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari na uhuru mwingine wowote nchini. Hakuna wakati wowote katika historia ya nchi yetu, Uhuru huo umejengeka, ukaimarika na ukashamiri kama ilivyo kipindi cha sasa cha Uongozi wa Awamu ya Nne ya Rais Kikwete.


Lakini ili uhuru huo uzidi kushamiri zaidi ni wajibu wa vyombo vyetu vya habari nchini kutenda kazi zao kwa kuongozwa na misingi mikuu ya uandishi wa habari ambayo ni kuandika habari za kweli na kwa misingi ya haki.


Habari hii ya Tanzania Daima leo ni mfano mwingine wa uvunjaji wa misingi hiyo kwa sababu siyo tu kwamba habari yenyewe ni ya uongo bali Mhariri wa Gazeti hilo hata hakujali kumtafuta na kuzungumza na Mhe. Wassira mwenyewe ambaye angesaidia kumpa ukweli wa hakika wa "habari zake za uhakika"

via wavuti.com
 
Lakin Waislam Mbona mnakuwa na mambo ya ajabu kiasi hiki?kwa nini hamuogopi hata nafsi zenu?mmepata faida gan kumuua mchungaji na Hisia zenu za kipuuzi?nyinyi mnaweza kumpigania mungu kweli?ila tambuen moto mkishauwasha msiokuwa na kazi nao kuuzima mtajuta wacha tuone ila mwenyezi mungu yupo na marehem huyu mliyemuua kinyama na Damu Yake itawaumbua,sina uhakika Kama mtume wenu anafundisha haya mambo yenu mnayoyafanya sasa ila muda utasema
 
"MASHARTI MAZITO MATANO" Huu ndiyo mtazamo wa mwandishi na taaluma yake.

Utayasemaje masharti 'mazito' wakati hayo ni mambo ya msingi kabisa ambayo serikali inatakiwa iyafanye kwa Raia wake. Sharti gumu hapo ni hili la serikali kuihudumia familia ya marehemu. Maamuzi kwa hili yanahitaji busara za hali ya juu kwa sababu serikali kuruhusu kufanya hivi, ni kufungua mlango kwa madai mengine na ishara kuonyesha kuwa serikali ndiyo GUILT kwa mauwaji ya mchungaji (CASE TO ANSWER). watu wengine wanaweza wakaleta pia madai kama hayo, kwa mfano, yaliyotokea Mtwara, Iringa, Morogoro n.k

Kweli kwa sasa magazeti yamepata waandishi.
 
WATANJANIA chijui nicheme nini!!!Mh!Yaani tunachubili jipya kutoka kwa nchema uongo?Kwani chi wanachema alichema uongo kwa palayament???Tukachikia alipotoka hapa home akaludia tena kudanganya kwa media na kwa palayament?CHACHA HAPA TUNATEGEMEA JIPYA LIPI?¿!CHI ALICHACHEMA LIWALO NA LIWE?Mhh!!!tuchubili tuone ichije ikawa chikio la kufa.
 
Lakin Waislam Mbona mnakuwa na mambo ya ajabu kiasi hiki?kwa nini hamuogopi hata nafsi zenu?mmepata faida gan kumuua mchungaji na Hisia zenu za kipuuzi?nyinyi mnaweza kumpigania mungu kweli?ila tambuen moto mkishauwasha msiokuwa na kazi nao kuuzima mtajuta wacha tuone ila mwenyezi mungu yupo na marehem huyu mliyemuua kinyama na Damu Yake itawaumbua,sina uhakika Kama mtume wenu anafundisha haya mambo yenu mnayoyafanya sasa ila muda utasema
Sio kosa lao ni kosa la kuchapika hadi akili zinayumba KUNAKOSABABISHWA NA JANGA KUU CCM,hata wakristo kwa asilimia kubwa wameathirika na gonjwa hili hatari.USIOMBE KUPATA VIRUS VYA GONJWA HILI KWANI NI HATARI KULIKO UNAVYOFIKIRI.~KOSA KUU HAPO NI KUUA,jiulize kama ni jambo geni masikioni mwako???Kila siku unasikia watoto wachanga wanaokotwa,unujua ni wangapi wanaoliwa na mbwa??Kila siku vibaka wanachomwa kwa ushirikiano wa watu wa imani hizi mbili tunazotaka kuzigombania??KWA NINI YOTE HAYA?ANS IS ccmonia,ni virus hatari vyenye kuambukiza magonjwa elfulela ulela.UJUMBE WANGU KWA WATU WA MATHEHEBU YOTE"PAMBANA NA CCM KULIKO UNAVYOPAMBANA NA MALARIA KWANI WAYO NDIO CHANZO CHA MADHILA YOTE YALIYOTUSIBU,YANAYOTUSIBU NA WAMESHATUTENGENEZA MENGI YATAKAYOTUSIBU TUSIPOKUWA MAKINI TUTAANGAMIA.
 
tatizo ni kwamba kuna kundi ambalo wanajiona kuwa dini yao ni bora zaidi ya kundi lingine na wanahaki zaidi ya wengine so ili kutatua tatizo hili lazima elimu ya kuheshimiana kiimani itolewe na kila dini ina ibada ambayo hukubaliwa kwa mungu kama wenzao. So nao pia wanastahili kuheshimiwa pia na sio kuwatungia majina ya ajabu, sijui makafiri nakadharika.
 
Back
Top Bottom