Geita: Wassira na Mwema watimuliwa

Geita: Wassira na Mwema watimuliwa

Mauaji ya GEITA na kupigwa risasi padre zanzibar ni matokeo ya maelekezo ya Ustaadhi Ilunga Hassan kuwa waislam waue maaskofu, mapadre na wachungaji hadharani au kwa kujificha
 
Mauaji ya
mchungaji Geita

na Josephat Isango


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Mahusiano na Uratibu), Stephen
Wassira na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, wametimuliwa mkoani
Geita, huku Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, akisulubiwa kwa
masharti magumu.

Vigogo hao wa serikali walikumbwa na patashika hiyo, juzi mkoani humo
walikoenda kusaka suluhu ya vurugu za kidini zilizosababisha mauaji ya
Mchungaji Mathayo Kachila (45) wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God.

Habari za uhakika kutoka mkoani Geita zimesema kuwa mamia ya wananchi wa
Geita walitishia kufanya lolote, ikiwa Wassira na Mwema wangeonekana
wakati wa mazishi ya mchungaji huyo au sehemu yoyote mkoani humo.

Taarifa za uhakika zimesema kuwa viongozi wa wilaya na mkoa huo, baada
ya kubaini kuwepo na hali ya hatari kwa viongozi hao, walilazimika
kubadili eneo ambalo helkopta iliyowabeba mawaziri na IGP ingetua.

Uchunguzi umebaini kuwa, chopa hiyo, awali ilitua katika eneo la
Kalangalala, lakini baada ya kubainika kuwepo na hali ya hatari,
ililazimika kuruka na kwenda kutua katika eneo la Magereza mjini Geita.

Mawaziri hao waliandamana na Mwema, toka Dodoma kulikokuwa kunafanyika
kikao cha makamishna wa polisi, makamanda wa mikoa na Rais Jakaya
Kikwete.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa wakazi wengi wa mjini Geita, hususan
Wakristo, walipata taarifa ya ujio wa mawaziri hao, ndipo walipoamua
kuchukua hatua hizo, na kwamba wasingekuwa tayari kuonana na Wassira kwa
madai kuwa alitoa tamko lililochochea zaidi chuki baina ya waumini wa
dini ya Kikristo na Kiislamu, huku wakimshutumu IGP Mwema kwa kuzembea
kuchukua hatua kulinda usalama wa watu.

Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu Waziri Nchimbi kutumia juhudi kubwa
kuwashawishi wananchi wakubali kumsikiliza kwa nia ya kupata ufumbuzi wa
vurugu hizo.

Imedaiwa kwamba Nchimbi alikubaliwa kuonana na wananchi ambao walimpa
masharti mazito matano aliyolazimishwa kuyakubali, kama njia ya kupata
ufumbuzi.

Sharti la kwanza alilopewa, walimtaka akubali na kutamka hadharani kuwa
serikali haina dini, na hivyo sio lazima kwa Waislamu tu ndio wachinje
na Wakristo wasichinje.

Sharti la pili ambalo Nchimbi alipewa na kulitekeleza hapo hapo ni
kuwaachia wachungaji waliokuwa wamekamatwa kwa madai ya kuchinja, wakati
sharti la tatu lilimtaka athibitishe kuwa wachungaji na Wakristo
wengine wataacha kunyanyaswa na Waislamu.

Sharti la nne lilimtaka Nchimbi atamke kuwa serikali itagharamia matunzo
ya familia ya mchungaji aliyeuawa na mazishi yake kwa sababu kifo chake
kimetokana na uzembe wa serikali kutochukua hatua dhidi ya jambo hilo
pamoja na kulalamikiwa na kupewa taarifa na wachungaji kwa barua.

Hata hivyo, Nchimbi aliomba jambo hilo hususan matunzo ya familia
aliwasilishe kwa wakubwa wake wa kazi, hususan Waziri Mkuu ili waweze
kupata ufumbuzi wa pamoja.

Pamoja na juhudi hizo za Nchimbi, Mkuu wa Mkoa Saidi Magalula, na Mkuu
wa Wilaya Ludorick Mpogolo, walikataliwa kabisa na wananchi, kiasi cha
kushindwa kuhudhuria mazishi ya mchungaji huyo. Mashuhuda waliokuwepo
kwenye msiba huo, wanasema Mpogolo aliyekuja kwa niaba ya serikali
alizomewa hali iliyomsababisha atoe rambirambi haraka na kuondoka eneo
la tukio.

Taarifa zaidi zilizopatikana zinasema Waziri Mkuu Mizengo Pinda
anatarajiwa kufika Geita leo ili kutafuta suluhu ya madhehebu hayo.

Wakazi wa kata za Buseresere na Katoro katika wilaya za Chato na Geita
walilalamikia serikali kushindwa kutoa msimamo juu ya mgogoro huo na
kuufanya wa kisiasa zaidi jambo lililosababisha vurugu na mauaji ya
mchungaji na baadhi ya raia kujeruhiwa vibaya.

Katika vurugu hizo, mali za wananchi zimeharibiwa vibaya huku baadhi ya
maduka na bidhaa zikiteketezwa kwa moto.
Miongozi mwa wananchi walioharibiwa mali zao ni pamoja na Mwenyekiti wa
BAKWATA Wilaya ya Chato na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Buseresere, Yusuf
Idd Banana ambaye ametaja mali zilizoharibiwa kuwa na thamani ya sh
milioni 10.

Waziri Nchimbi hakupatikana kwa simu kuzungumzia hali hiyo kwa kuwa simu
yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.

Source: Tanzania Daima

Ah! Kumbe source na Chadema News paper! wala sishangai!
 
Kumbe tanzania daima gazeti la udaku, hapo hakuna ukweli wowote ule ni majungu tu.
 
Kumbe tanzania daima gazeti la udaku, hapo hakuna ukweli wowote ule ni majungu tu.
 
kwani wasira alienda tena kuwaambia waislam ndio wachinje,yan kufuga afuge mwingine,kuchinja achinje mwingine,nchi hii haina dini,kila mtu ana haki ya kuchinja ata ambaye hana dini
 
Acheni uongo na kuwadanganya watanzania wasioishi Geita.Mimi nipo Geita na jumatano nilikuwa Katoro na Nzera.Geita mjini hakuna mtu yeyote anayeongelea issue ya kuchinja wala hakuna tatizo lolote.Katoro ndio watu wanazungumzia hali hiyo haswa haswa wanasikitishwa na vurugu zilizosababisha kifo cha mchungaji na hakuna mtu anaetaka kujulikana alishiriki au alishawishi kila mtu yuko kimya akijifanya kusikitika pindi ukimuuliza.
 
Hatujajua bado mchuma janga hula na nduguze
 
Wasira ni janga la kitaifa! Ukisikia cheap popularity basi mzee huyu mwenye sura kama ya binadamu wa kale anapenda mno! Hata boss wake analijua kuwa hana hoja zaidi ya ukali na ukaidi, ndiyo maana akampa jina la Tyson


Ni tatizo la kumuinua mtu kutoka mavumbini hadi kwenye Uwaziri. Wasira alishakuwa mtu asiye na matumizi ktk taifa, ghafla eti anapewa uwaziri kama fadhila. Here we are!

Yeye ni kutafuta pesa tu ingawa mawaziri wote wa serikali hii ndo walivyo. Angalau basi awe na hekima! Hakuna!
 
Mauaji ya GEITA na kupigwa risasi padre zanzibar ni matokeo ya maelekezo ya Ustaadhi Ilunga Hassan kuwa waislam waue maaskofu, mapadre na wachungaji hadharani au kwa kujificha

Ni matokeo ya mkuu kuuchekea udini-kuwasapoti waislamu.
 
na bado!wanacheza na m2 aliyechoka!anaweza fanya lolote

hivi na wewe umeamini hizo porojo?eti mwema atimuliwa!!!!sifa za kijinga zitatupeleka pabaya jamani!!!!unaandika hivi watu wanasoma wanaamini kumbe inawezekana kesho wanajaribu kweli,wanauawa tunasahau kama tulivyowasahau waliokufa mtwara,arusha na kwingineko.
 
Wananchi wa Geita kiwalacho ki nguoni mwenu, hizo dini munazojifanya nyinyi ndo waanzilishi mmezitoa wapi?
Hiyo misimamo ya kuchinjana badala ya kuchinja wanyama kwa kitoweo hamuoni ni misimamo ya watu wasiyokuwa na akili? Inakuja mijitu yenye uroho wa mali inawadanganya kwamba matatizo yenu ni dini na nyie munakubali? Kwa mtaji huu nashindwa kujua taifa lina watu wa aina gani? Hata mkiwakataa hakina wassira na mwema haisaidii kitu kama mumekwishauana kwa kisingizio cha dini. Hizo imani zinazowafanya kuuana ni imani za kishetani wala hazitoki kwa Mungu achana nazo. Babu zenu wamewafundisheni hayo? Na nyie waislamu nani kawaambia muna hati milki ya kumchinjia kila mtu?
Kama muna hati milki ya kuchinja basi anzeni na nguruwe. Watu waliamua kuchinja kwa ajili ya wao wenyewe nyinyi kiliwawasha kitu gani hadi mwende kuwavamia? Watu walikuwa na haki ya kuwasusa Wassira na Mwema kwa sababu mchokozi anajulikana kwa nini munataka kumung'unya maneno. Tunaweza kumaliza tatizo kwa kuangalia nani alikuwa mchokozi kati ya waislamu na wakikristu. Hao ng'ombe au bucha iliyotumika ilikuwa ya nani? Je waliiuza nyama kimya kimya au walitangaza? kama walitangaza kwamba aliyechinja ni mkristu basi waislamu walitakiwa kutangaziana ili wasiende kununua kwenye bucha hizo/hiyo ya nini kuvamia na mapanga? Hapo si ndo kuna kesi ya mauaji kwa hao waliovamia? Ni wakati gani mtu anafunguliwa kesi ya mauaji kama si ndo wakati kama huo?

Ili kuzuia tatizo hilo lisitokee tena ni vyema kuuleza umma kinaga ubaga juu ya sheria inayotuongoza katika swala zima la kuchinja wanyama wote akiwemo nguruwe. Pia kila muumini aelezwe mipaka ya imani yake anapokuwa katika jamii nje ya msikitini, kanisani au chini ya mbuyu mkubwa. Imani yake isimfanye kuingilia uhuru wa watu wengine
 
Hivi inawezekana vipi mtu anoe panga, kisha aende kumchinja binadamu mwingine kama kuku? Huyo mtu anakuwa na roho ya namna gani? Biblia inasema mwivi, yaani, Shetani haji ila, aibe, achinje na aharibu. Je, mtu wa namna hii tunaweza kumfananisha na Shetani? (Yohana 10:10a) :confused2:
 
Madhara ya akili kidogo kung'ang'ania madaraka,mpaka ma sokwe yanaaminiwa eti kuiwakilisha serikali.
 
Wasira anajua nini zaidi ya kutumika? 2005 salm ahmed si mtanzani,si ukabila huo? 2010 slaa katumwa na kanisa, uchaguzi mdogo igunga, cdm wamvua mkuu wa wilaya baibui badala ya kilemba, si udini huo? Kikwete hakuyajua hayo? Na je, alisema nini? Sisi si wajinga hata kidogo! Naomba watanzania tujiandikishe kupiga kura 2015.


hapo kwenye BOLD muhimu sana!!
 
Halafu mjinga mmoja anasema Tanzania kuna amani. Huu ni utulivu tu.
 
haya ndio madhara ya viongizi wetu kutoa kauli nyepesi katika mambo mazito yanayohusu nchi.kukataliwa kwa.wasira.na igp mwema.iwe fundisho kwa viongozi kuwa makini kutatua mambo yanayo jitokeza katika nchi leo madhara haya yasingetokea kama serikali ingekuwa makini kutafuta suluhu.geita waswahili wana msemo wao unasema ukificha moto moshi utakuumbua.sasa haya ni madhara ya kuficha moto moshi unawa umbua.

Majibu mepesi na ya ovyo ovyo kwenye mambo muhimu haya ndio matokeo yake.Kule Mbagala tulitegemea kauli nzito tukaishia kusikia tuvumiliane,Zanzibar hivyo hivyo huyu mtu atavumilia mpaka afanywe nini?Kama maamuzi hatuna ebu tuige ya mzee Mwinyi mbona hayakujirudia tena?Kama viongozi wataweka uzani kwa kuonyesha pande zote zinahusika mwisho wa siku yatatokea makubwa zaidi ya haya ale yule anayetakiwa kuvumilia atakapochoka.Uongozi ni kutoa suluhisho bana
 
Back
Top Bottom