Geita: Wananchi wagombea nyama ya fisi kwa madai kuwa ni dili kwa waganga wa kienyeji

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Katika hali ya kawaida watu wanaweza kugombea nyama ya Ng'ombe, Mbuzi, hata Kondoo, lakini hali hiyo ni tofauti kwa wananchi wa kijiji cha Bukungu wilayani Nyang'hwahe mkoani Geita wao wamegombea nyama ya fisi.

Hatua hiyo imekuja baada ya mnyama huyo aliyeingia kwenye zizi la Mbuzi na Kondoo linalomilikiwa na Bwana Mpuya Ganganyi, saa 10 alfajiri kukumbana na kifo kutoka kwa majirani wa mfugaji huyo baada ya kupata kibali cha kumuua.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Azam Tv Geita, aliyeshuhudia tukio hilo la kugombea nyama hiyo amesema, ilikuwa kama sinema baada ya mnyama huyo kuuawa na watu kuamua kugawana nyama yake kwa madai kuwa ni dili kwa waganga wa kienyeji.
FB_IMG_15347716115179540.jpg
FB_IMG_15347716006736273.jpg
FB_IMG_15347715832193541.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je walipata kibali toka mali asili na utalii? Hizo ni nyara za serikali.
 
Hahahaha naoana ccm wanagombea fisiem kumbe kweli ni haya majamaa yanapenda uchawi sana!
Cc Mshanajr
 

Attachments

  • tapatalk_1534774963317.jpeg
    tapatalk_1534774963317.jpeg
    36.7 KB · Views: 19
Back
Top Bottom