Geita: Wananchi wagombea nyama ya fisi kwa madai kuwa ni dili kwa waganga wa kienyeji

Katika hali ya kawaida watu wanaweza kugombea nyama ya Ng'ombe, Mbuzi, hata Kondoo, lakini hali hiyo ni tofauti kwa wananchi wa kijiji cha Bukungu wilayani Nyang'hwahe mkoani Geita wao wamegombea nyama ya fisi.

Hatua hiyo imekuja baada ya mnyama huyo aliyeingia kwenye zizi la Mbuzi na Kondoo linalomilikiwa na Bwana Mpuya Ganganyi, saa 10 alfajiri kukumbana na kifo kutoka kwa majirani wa mfugaji huyo baada ya kupata kibali cha kumuua.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Azam Tv Geita, aliyeshuhudia tukio hilo la kugombea nyama hiyo amesema, ilikuwa kama sinema baada ya mnyama huyo kuuawa na watu kuamua kugawana nyama yake kwa madai kuwa ni dili kwa waganga wa kienyeji.View attachment 842455View attachment 842456View attachment 842457

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona Wengi ni wanaccm wakiwa katika uniform na huo ndio mtaji mkuu
 
huku niliko fisi aligongwa na gari asubuhi kabisa alfajiri kufika saa tano mchana hakukuwa na kiliachobaki nasikia walianza na kukata pua kasha mkia wasukuma wanaamini ushirikina sana
 
Kweli njaa ni kali sana kwa Wabongo wengi. Wanagombea nyama ya fisi? 😳😳😳😳

Back
Top Bottom