Geita: Serikali ya kijiji Nyankumbu yavuliwa uongozi

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,714
10,039
Kutoka gazeti la Nipashe

Serikali ya kijiji Nyankumbu yavuliwa uongozi

2007-10-13 08:37:59
Na Renatus Masuguliko, PST Geita

Uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Nyankumbu, Wilaya ya Geita akiwemo Mwenyekiti wake, John Lunyaba, wamevuliwa uongozi baada ya kukataliwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.

Viongozi hao walikataliwa mbele ya uongozi wa wilaya kwa tuhuma za kushindwa kuwajibika na ubadhirifu wa zaidi ya Shilingi milioni moja.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kalangalala, Bw. Hamadai Husein, alisema hatua hiyo ni halali kwa vile taratibu zote za kisheria zilizingatiwa na kuwa Mkutano Mkuu wa kijiji ambao uliwashirikisha zaidi ya wanakijiji 500, una mamlaka ya kutoa uamuzi kama huo.

Uamuzi wa kuivunja serikali ya kijiji, ulifikiwa baada ya kubainika kuwa, wajumbe wa serikali ya kijiji ambao ndio wenye mamlaka kisheria kusimamia utekelezaji wa kila siku na uendeshaji iikiwemo kusimamia na kulinda mali ya kijiji wamekuwa wanashirikiana naye na kumlinda badala ya kumwajibisha.

Aliongeza kuwa hatua hiyo ilifikiwa mbele ya Bw. Jackson Sombe, mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw. George Marco alisema ameridhia utaratibu uliotumika wa kuwang�oa madarakani viongozi hao.

Awali, katika mkutano huo uliokuwa umeitishwa rasmi kujadili matatizo ya muda mrefu kuhusu uongozi wa kijiji hicho, kumekuwepo na malalamiko dhidi ya serikli ya kijiji hicho kutowajibika.

Pia uongozi huo umedaiwa kushirikiana na Mwenyekiti wa kijiji na baadhi ya wajumbe kufuja fedha za kijiji.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi wa Halmashauri ya wilaya iliyothibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya, Bw. Dani Mollel, ilibainika kuwa, Mweyekiti wa kijiji anatuhumiwa kutafuna zaidi ya Shilingi milioni moja.

Fedha hizo ni pamoja na zilizotokana na malipo ya boma la kijiji, viingilio, na mradi wa uchomaji tofali.
 
Haya sasa mbona hizi ni TUHUMA na zimehalalishwa bila ushahidi, tena basi na hukumu imeshatolewa na viongozi wanaodai ushahidi ktk maswala ya Taifa.

Ni wakati gani haswa maamuzi ya wananchi huwekwa mbele ya uteuzi wa viongozi?
 
Haya sasa mbona hizi ni TUHUMA na zimehalalishwa bila ushahidi, tena basi na hukumu imeshatolewa na viongozi wanaodai ushahidi ktk maswala ya Taifa.
Ni wakati gani haswa maamuzi ya wananchi huwekwa mbele ya uteuzi wa viongozi?

Heshima kwako mkuu;

Ni zilikuwa tuhuma, zikapelekwa kwenye mamlaka husika (mkutano mkuu wa kijiji) na idadi ya wajumbe umeiona, nadhani watugtumiwa wakapewa muda wajitetee, kama katiba inavyotaka, wakasema hawawataki viongozi waliochaguliwa, Halmashauri ya Wilaya ikaweka baraka zake. In fact, mimi nimeona hawa jamaa ni matured sana kuliko hao akina. This is a good governance scenario. Kurusha mawe kwa namna yoyote ni uhuni tu!

Maoni yako nayaheshimu mkuu, maana mimi na wewe ni sawa sawa na kichuguu na mlima Kilimanjaro, uko juu mzee, lakini niruhusu sehemu chache chache niwe tofauti nawe.
 
Duh Tanzania Tanzania, inaliwa na wenye meno makali, kweli wanaipenda kwa moyo kutokana na kuneemeka bila jasho, kutegemea jasho la wengine. Sasa wavuja jasho wameshituka na wao wanataka malipo yao halali. Kazi ipo!
 
Baada ya kutimuliwa kazi ni wakati wa kuwafungulia mashitaka ya wizi na ubadhirifu. Ili waonje tamu ya chungu
 
In fact mimi nimeona hawa jamaa ni matured sana kuliko hao akina... This is good governance scenerio.... Kurusha mawe kwa namna yoyote ni uhuni tu!

Baada ya kutimuliwa kazi ni wakati wa kuwafungulia mashitaka ya wizi na ubadhirifu. Ili waonje tamu ya chungu
Today 06:14 PM

Heshima mbele mkuu Kilitime.

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100 kuwa hawa Watanzania wenzetu wametumia katiba na taratibu halali kuwavua uongozi watuhumiwa. Kweli wao ni mature, kwa maana ya kwamba jinsi walivyowaweka madarakani viongozi wao ndivyo hivyo walivyowatoa. Nasema ni watuhumiwa kwa sababu hakuna mahakama iliyokaa kuwahukumu viongozi wao. Wangengoja mahakama huenda kesi hii ingechukua hata miaka kuhukumiwa, kwa mazingira ya vyombo vyetu vya kutoa haki. Kama demokrasia hii itaendelea hadi ngazi za wilaya na mikoa nina uhakika tutafika mbali, kwani sisi ndio tunaowaajiri, kwa hiyo tuna mamlaka ya kuwaondoa katika ajira viongozi wasiowajibika.

Madilu, ni kweli kuwa sasa iwe ni wakati mwafaka kwa hawa watuhumiwa kupelekwa kunako mahakama ili wasafishwe ama wapatilizwe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom