DOKEZO Responded GEITA: Kuna Kijana ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Hifadhi ya Pori la Kigosi, TFS na Jeshi la Polisi mbona mpo kimya?

DOKEZO Responded GEITA: Kuna Kijana ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Hifadhi ya Pori la Kigosi, TFS na Jeshi la Polisi mbona mpo kimya?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Joined
Sep 23, 2024
Posts
73
Reaction score
73
Kuna tukio limetokea huku kwetu Kijiji cha Msonga Kata ya Runzewe, Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, kama tutaendelea kubaki kimya hakuna kitakachofanyika na hatua hazitachukuliwa.

Kuna kijana amepoteza maisha kwa kupigwa risasi na Askari wa Hifadhi ya Hifadhi ya Msitu Kigosi ambayo inasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), tukio limetokea jana saa kumi na mbili asubuhi, tarehe 13 Agosti 2025.

Vijana watani walikuwa ndani ya hifadhi hiyo wakikata miti kwa ajili ya mbao, ndipo wakatokea Askari hao wa hifadhi, vijana wakaamua kukimbia, mmoja wao aliyetambulika kwa jina la Eziboni ile anapiga hatua kukimbia askari hao wa hifadhi wakafyatua risasi ambayo ilimpiga kwa nyuma na kutokea kwenye kitovu.

Wakati wanakimbia ndugu wa Eziboni akaona tukio lote akaamua kugeuza na kwenda mwenyewe kwa hao askari na kuwaambia “Mmepiga ndugu yangu akiwa hana silaha wala madhara yoyote kwenu, niueni na mimi tu.”

Wale askari wakashangaa na kuanza kuogopa wakawa wanamgeuzageuza kijana aliyepigwa risasi baadaye wakambeba kumuweka kivulini, kisha wakamwambia yule ndugu yake kuwa aende akawaite ndugu zake wamchukue mwenzao kumpeleka hospitali kwa kuwa alikuwa bado hajakata kauli.

Wakati akigalagala pale chini Eziboni alikuwa akiwaambia wale Askari “Mnaniua ndugu zangu na sijawafanya lolote, mnaniua, mnaniua” huku akilia kwa uchungu.

Yule ndugu yake alivyoondoka kwenda kutoa taarifa nyumbani, waliporudi ili kumchukua mwenzao hawakuwakuta wale Askari na walikuta mwenzao ameshakata kauli.

Wakaubeba mwili hadi nyumbani kisha wakatoa taarifa Polisi ambapo walifika na kuuchukua mwili kuupeleka Hospitali.

Polisi wamewaambia ndugu wa marehemu kuwa wanaufanyia uchunguzi mwili kisha waende kuuchukua leo Tarehe 14, 2025, ndugu wamegoma kwa kuwa wanataka haki itendeke kwa waliohusika na mauaji ya ndugu yao.

Kijana huyo aliyefariki alikuwa na umri wa miaka 20+ kinachotokea wale askari wa Hifadhi wameingia mitini na hakuna mamlaka inayohusika kuchukua hatua kwa kuwa wanawaona ndugu wa marehemu hawajui chochote kuhusu masuala ya sheria.

Nimeandika kama raia mwema ambaye nimefika katika Kijiji hicho ili hatua zichukuliwe haraka, TFS nao watoe majibu na kuchukua hatua kuhusu tukio hilo.

================​

TFS WAULIZWA KUHUSU TUKIO HILO
Meneja Uhusiano wa Wakala wa Mistu Tanzania (TFS), Johary Kachwamba alipoulizwa kuhusu hoja hiyo ya Mwanachama wa JamiiForums.com amesema:

“Tumepata taarifa kuhusu tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inatarajiwa kuwa na kikao muda sio mrefu leo hii (Agosti 14, 2025) wanatarajiwa kujadili kuhusu hilo ili kubaini kama lina ukweli au la na pia kuna taratibu za ndani zinaenda, hivyo, kukiwa na taarifa zaidi tutatoa mrejesho.”

Tamko la Jeshi la Polisi ~ Geita: Askari wanne wa Jeshi la Uhifadhi wakamatwa kwa tuhuma za mauaji
 
Poleni, ila mjue uhalifu haulipi, hao vijana walijua wanafanya uhalifu ndiyo sababu walikwenda msituni kukiwa na giza ili wasionekane, hayo ndiyo malipo ya uhalifu.
 
Kama tunavyo jiepusha na ajali ,hata matatizo kama hayo tunapaswa kuyaepuka pia.
Anyway poleni kwa msiba.
 
Polisi, askari, wajeshi, hawa msitegemee sheria itawakiuka, inawalinda kivyovyote na popote.

Hawa dawa yao ni kuwapiga juju tyuuh, nimekumbuka kijijini kwetu walikuja mali asili, bas wakawa wanakataza watu kukata miti, pia kuwinda wanyama,

Ili hali wananchi walishazoea ukataji wa miti kwa mkaa na mbao pia kuni, na uwindaji wa nyama ili kupata kitoweo na mboga.

Bas kuna siku hao mali asili, walikuta vijana msituni wanawinda, wakawakuta wanamchuna mbalapi tena amenona, wasianze kuwatesa wale vijana, pigisha kwata, mazoezi, yaan waliwahenyesha, na nyama wakawa pora, sasa ktk wale vijana m1 wapo alikua ana matatizo yake tangu kuzaliwa, kwa mateso Yale, alipata hitilafu na akapelekwa hospital akafia huko.

Wenzie wakaenda kwa mtendaji wa kata kueleza tukio lilivyo, yule mtendaji akawa upande wa wale mali asili, kuwa vijana wana makosa, sasa kwann nyama waliporwa si wangeachiwa? Blaah blaah.

Team ya mafekeche ikaingia kazini, mali asili m1 km utanii akadanja, zubaaa zubaa, wa 2 nae chaliii, ndani ya mwez 1 huo, wale wengine wakastuka huu mchezo, wasirudi kuomba radhi, walilipa hela.

Hawa dawa yao ni kuwapiga kipapai pyuuh, wanatia adabu, sisi kwetu hatucheki na yoyote, tunamalizana nao namna tunayoweza wenyewe.
 
Back
Top Bottom