Geita: Ahukumiwa kwenda jela miaka 3 au kulipa faini ya tsh milioni 2 kwa kula rushwa ya Tsh. milioni 75

Hasara aliyosababisha milioni 75,hukumu anatakiwa kulipa milioni 2?!! Hizi milioni 73 za Jamhuri nani anazifidia?

Katiba mpya muhimu sana
Jamani muwe mnasoma na kuelewa kabla ya kujionesha mlivokuwa namna gani vichwani.....hebu Rudia tena kusoma mpaka paragraph ya mwisho,usipoelewa njoo PM nikufundishe tuition
 
Hasara aliyosababisha milioni 75,hukumu anatakiwa kulipa milioni 2?!! Hizi milioni 73 za Jamhuri nani anazifidia?

Katiba mpya muhimu sana
Kuna yule Dada wa Songwe Mbeya huko aliyepigwa miaka 30 kwa kosa la million sijui tatu...mahakama zinachekesha sana
 
Hasara aliyosababisha milioni 75,hukumu anatakiwa kulipa milioni 2?!! Hizi milioni 73 za Jamhuri nani anazifidia?

Katiba mpya muhimu sana
Lazima ujue kwamba katiba haiwezi kubeba kila kitu mkuu. Msiweke matumaini makubwa kwenye katiba as if huo ndiyo muarobaini wa matatizo yetu.
Yakupasa ujue kama hatutakuwa na utashi wa kisiasa, katiba haiwezi kutibu changamoto zetu.
 
Kuna yule Dada wa Songwe Mbeya huko aliyepigwa miaka 30 kwa kosa la million sijui tatu...mahakama zinachekesha sana
 
Kwa aina hii ya sheria, kupunguza vitendo vya rushwa na ufisadi nchini (achilia mbali kuvimaliza kabisa!) hakika itabakia kuwa historia tu.
 
Daktari kapata karushwa ka ngono kutoka kwa denti mzoefu, tena kwa makubaliano ya me kubembelezwa eti ''nifanye kidogo tu hapahapa pichu sina, wala sita sema'' ........ likibumburuka ni miaka 30 jela!!.......jamani Dunia hii??
 
MAHAKAMA ya Wilaya ya Geita imemhukumu Kaimu Mkuu wa Idara ya Maji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mhandisi Rael Buliba (38), kutumikia kifungo cha miaka 3 jela au kulipa faini ya Sh. milioni 2 kwa makosa mawili ya kupokea rushwa ya Sh. milioni 75.

Alipatikana na hatia ya kupokea rushwa hiyo kupitia kwenye akaunti ya mzazi mwenzake, Edes Joseph, kutoka kwa mkandarasi Francis Nyenge ili apate kuongezewa muda wa mkataba wa kusambaza mabomba ya maji katika mradi huo.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Samuel Maweda, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha makosa yote mawili pasipokuacha shaka yoyote.

Hakimu Maweda alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili liwe fundisho kwake na kwa watumishi wengine wenye tabia ya kupokea rushwa.

Alisema upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Kiongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita, Kelvin Murusuri, alipeleka hapo mahakamani mashahidi 5 na vielelezo 6, ambavyo vilithibitisha kuwa mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo.

Aidha, Hakimu Maweda alisema amelipitia ushahidi wa pande zote mbili na kugundua kuwa upande wa mashtaka umethibitisha makosa yote mawili pasipo kuacha shaka yoyote, hivyo mahakama inamtia hatiani mshtakiwa kwa makosa yote mawili.

Mshtakiwa huyo alipopewa nafasi ya kujitetea, aliiomba aachiwe huru kwa sababu ana familia inayomtegemea.
Hakimu Maweda alitupilia mbali utetezi huo na kusema kuwa makosa ya namna hii ya kuhujumu serikali yamezidi sana, kwa sababu mshtakiwa huyu ni mtumishi wa serikali, na kwamba chakushangaza anaihujumu serikali iliyomwajiri.

Aidha, Hakimu Maweda alisema mahakama inakuhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh. milioni moja na kosa la pili mshtakiwa utakwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh. milioni moja.

Mshtakiwa huyo alilipa faini ya Sh. milioni mbili kwa makosa yote mawili na kuachiwa huru.
Mshtakiwa huyo alikuwa akitetewa na Wakili wa Kujitegemea, Penina Mashimba na upande wa Jamhuri ulikuwa ukiongozwa na Wakili Kiongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita, Kelvin Murusuri pamoja na Wakili wa Serikali, Daniel Masambu.

Mshtakiwa huyo na wengine wawili walikuwa wakikabiliwa na makosa tisa ya uhujumu uchumi na rushwa ya Sh. milioni 75 za mradi wa maji wa vijiji viwili ambavyo ni Chikobe na Nyamtukuza.

Awali washtakiwa Edes Joseph na Frasinci Nyenge walikiri makosa yao yote na kuhukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini ya Sh. milioni 75 na kwa pamoja walilipa faini na kuachiwa huru.

Katika hati ya mashtaka, ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo na wenzake wawili walitenda makosa hayo Machi na Oktoba mwaka 2014, kwa kupokea rushwa ya Sh. milioni 75 kupitia kwenye akaunti ya mzazi mwenzake, Edes Joseph kutoka kwa mkandarasi, Frasinci Nyenge ili apate kuongezewa muda wa mkataba wa kusambaza mabomba ya maji katika mradi huo.

NIPASHE
Sasa hizo milioni 75 atazitumia wapi?
 
Back
Top Bottom