Gazeti RAI laishambulia CHADEMA

Gazeti RAI laishambulia CHADEMA

Anasema chadema wanafuja fedha kwa kuzitumia kwenye oparesheni m4c huku kikishindwa vibaya kwenye uchaguzi wa madiwani.hajui kuwa ccm walishinda vizuri kwenye kata nyingi baada ya kufuja fedha kwa kuwahonga wapiga kura.je alitaka chadema nao wafuje hela nyingi kwa kuwahonga wapiga kura ili washinde vizuri?badala ya kutumia hizo fedha kuimarisha chama kupitia m4c ili uchaguzi ukifika chadema washinde kihalali kuliko ccm wanaoshinda vizuri kwa kuhonga.
 
Kutaka kuona sifa za CHADEMA kupitia gazeti la RAI aka ROSTAM AZIZ, ni sawa na kutaka kusikia Sifa na Ukuu wa Jina la Yesu kupitia RADIO IMANI.

Wala msipoteze muda hapa.
 
Gazeti la RAI limeshambulia vikali chama cha CDM kwa kile lilichodai kufuja pesa ovyo kwa operesheni M4C huku chama hicho kikishindwa vibaya kwenye uchaguzi wa madiwani.
Gazeti hilo limedai matokeo hayo ya Chadema hayaridhishi kabisa wananchi ikilinganishwa na nguvu kubwa iliyotumiwa na chama hicho.
Matokeo ya udiwani yanaonyesha mgawanyo wa viti ulikuwa CCM 22 CDM 5 TLP 1 CUF 1.Hata hivyo CDM ikifanikiwa kurejesha viti vyake 2 huku ikiinyanganya CCM viti 3.


My Take:
Gazeti la RAI miezi iliyopita lilikuwa limeanza kurudu katika ramani yake kwa kutoa habari bila upendeleo lakini tangu Prince Bagenda aajiriwe kama Mhariri Mkuu amekuwa na chuki kubwa dhidi ya chama cha CDM na habari za gazeti hilo kila wiki zimekuwa zikikishambulia vikali chama hicho.Pia tangu Bagenda aajiriwe kumekuwa na makala maalum kila wiki za kushambulia viongozi wa chama hicho hasa Mkiti Freeman Mbowe n Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.Hata hivyo soko la gazeti hilo kwa sasa tangu aajiriwe Bagenda limeporomoka vibaya sana.
Prince si wa kwanza kunena ufujaji wa Fedha M4C wapo pia Kama Nyimbo aliyekipa mgongo Chama hiki hivi karibuni. WanaJF tafadhari tajeni na wengine. Ila mimi naamini siku si Nyingi watashikana Mashati kugombea ulaji wa Fedha na hapo ndo Siri zaidi zitakapofumka. CDM ndo inakwenda hivyo ifikapo 2014 itakuwa hoi bini taabani
 
rai ni gazeti au toilet paper?halafu tokea lini kata 34 zika-determine mshindi 2015!!!!
 
Huyu jamaa alikuwa na jenerali ulimwengu ,salva rweyemamu, Padri privatus karugendo ,muhingo na wengine tu enzi za gazeti la rai .

Baada ya kuuzwa wananunuzi wakafikri na waandishi akili zao pia wamezinunua ,jamaa wakaachia gazeti wakaanzisha raia mwema vichwa vyote vikahama.

Isipokuwa Prince Bagenda aliyepewa jukumu la kuandika makombora enzi za mh.Kikwete baada ya ushindi Salva Rweyemam akapewa mwandishi wa rais,Bagenda ama misimamo yake ama hulka yake akaachwa,wenzie wote wakahamia gazeti la raia mwema.

Bagenda nampenda namheshimu ila ana udhaifu wake anatumiwa ana misimamo mikali akishika kalamu akakaa chini kama uko ofisini utatafuta pa kutokea ,kumbukeni enzi za gazeti la rai kipindi cha mkapa ,ila cha muhimu shujaa mmoja akipotea huzaliwa wengine .mwanahalisi ikazaliwa.

Wahaya ni kabila la kipekee na la ajabu. Ulimwengu is affiliated to them, ona timu yake aliyokuwa nayo Rai na itazame timu aliyonayo sasa Raiamwema
 
fmpiganaji, hili gazeti haliwezi hata siku moja kuiandika vizuri CDM kwa sababu ndio waliomfanya bosi wao ajiuzuru ubunge wa Igunga. Lakini pia 'Profesa' J. aliimba "ili nifanikiwe ninahitaji marafiki, ili nifanikiwe zaidi nahitaji maadui. Maadui wa CDM wamekuwa wakitoa mchango mkubwa sana (japo bila kulitambua hilo). M4C inatesa watu wengi sana, kwa kuona haraka unaweza kuona kuwa haijafanya kitu, ila kiukweli kuna kitu kikubwa sana kimefanyika, Vijana ambao bado wamenyimwa haki yao ya kupiga kura ni wangapi katika hizo kata, uandikishaji ulifanyika 2010. Siumizwi na wakala wa NYINYIEM (RAI) ila ni kuongeza umakini ktk M4C inayofuata.



Dah umenikumbusha kitu, hivi daftari lililotumika ni lilelile, ah aisee CHADEMA imeshinda maana najua for sure 80% ya kura mpya ni CHADEMA for 2015 election

Bravoo CHADEMA
 
Nimelinunua gazeti la Rai, na nimelisoma lote lakini sijaona sehemu yoyote limeishambulia Chadema. Rai limeandika Chadema wamepata viti 5 vya Udiwani, CCM wamepata viti 22 vya Udiwani...sasa hapo kuna kosa gani.
Mungu wangu kweli dunia haina haki hivi kweli kwenyeuteuzi wa wakuu wa mkoa amekusahahu,wa wilaya pia?jitahidi mwanangu akina nepi wanakusoma wanaweza wakakupendekeza
 
Kweli upenzi unawasumbua na utakiangamiza chama chenu huku mnakiona! Badala ya kujadili hoja mnajadili mtu. Hivi ni watu gani nyie ambao mnaamini kwamba mko perfect? There is only one perfect being.

ccm kwisha nambari wani eeeeeeeeee
 
Nimelinunua gazeti la Rai, na nimelisoma lote lakini sijaona sehemu yoyote limeishambulia Chadema. Rai limeandika Chadema wamepata viti 5 vya Udiwani, CCM wamepata viti 22 vya Udiwani...sasa hapo kuna kosa gani.

CCM Kata 22=kura 29 000
CHADEMA Kata 5=kura 28 800
 
Hivi CDM haipaswi kuhojiwa,kukosolewa au kushauriwa? Bila ya kukikosoa Chama kitajijengaje?

Kama tukiamini kwamba kila kinachofanywa na CDM ni sahihi tutakua hatukisaidii Chama kujijenga bali tutakuwa tunakiangamiza.

Au mnataka tuamini zile kauli za 'ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI WA CHAMA?"

TAFAKARI....
 
Ulitegemea Rostam aipende CDM ilhali akijua ikichukua nchi anaweza kuozea Keko akinyea debe kwa ujambazi wake?
 
Ukifungwa bao 22 nawe ukapata mabao 5 maana yake umeshuka daraja.

Kweli CDM ni wapiga debe profesional. Yaani kelele zote hizi mnaambulia viti 5 tu... Ama kweli Ikulu iko mbali nanyi. Hongera mwenyekiti wa CCM Mh Kikwete kwa kazi nzuri uliyoifanya.

Mama Angel Markel wa Ujerumani na chama chake Christian Democratic Party kitasusia kuwapa misaada, maana ile safari ya mwenyekiti wa vijana cdm ataonekana Tapeli kwa ile hutuba yake kule Ujerumani.

Sasa Utabiri wa CDM kufa upo karibu kuitika.
 
CCM Kata 22=kura 29 000
CHADEMA Kata 5=kura 28 800

Hamtamtambua Rais KWA matokeo haya. Au mtatoka Bungeni Spika atapohutubia.

Hebu muulizeni mh Slaa anamipango gani safari hii.

Naweza kuhisi tu, kuwa safari hii atajiuzulu.
 
fmpiganaji, hili gazeti haliwezi hata siku moja kuiandika vizuri CDM kwa sababu ndio waliomfanya bosi wao ajiuzuru ubunge wa Igunga. Lakini pia 'Profesa' J. aliimba "ili nifanikiwe ninahitaji marafiki, ili nifanikiwe zaidi nahitaji maadui. Maadui wa CDM wamekuwa wakitoa mchango mkubwa sana (japo bila kulitambua hilo). M4C inatesa watu wengi sana, kwa kuona haraka unaweza kuona kuwa haijafanya kitu, ila kiukweli kuna kitu kikubwa sana kimefanyika, Vijana ambao bado wamenyimwa haki yao ya kupiga kura ni wangapi katika hizo kata, uandikishaji ulifanyika 2010. Siumizwi na wakala wa NYINYIEM (RAI) ila ni kuongeza umakini ktk M4C inayofuata.

Wawaandike vizuri zaidi ya hivyo? au mnaona raha kufujiwa fedha na viongozi wenu, jiulizeni fedha ngapi zilizosemwa zimeelekezwa M4C hazikwenda huko. Nasikia Slaa kamjengea Josefina nyumba ya million 500.

Upo hapo ulipo?
 
Kweli upenzi unawasumbua na utakiangamiza chama chenu huku mnakiona! Badala ya kujadili hoja mnajadili mtu. Hivi ni watu gani nyie ambao mnaamini kwamba mko perfect? There is only one perfect being.

Now your talking,ebu twende katika mada,vuguvugu la mabadiliko lililenga uchaguzi wowote ukifanyika viti vyote viwe vya ubunge,udiwani,mitaa na urais,sasa hata nusu imeshindikana lakini hiyo haitoshi viongozi waandamizi wanaondoka bado tu mtasema wanatamaa na njaa,mnakazi kweli
 
Huyo Bagenda nilishamsikia Masilingi akimsema jinsi anavyo mpa shida ya Uongozi wake huko kwao Kagera.
 
Hii hoja ya udiwani tumeijadili weeeeeeee hapa mpalka wanazi waanza kuelewa, sasa kaamua kutoka nayo kwenye magazeiti yake ya udaku........maana simple logic... CCM na viti 22 wamepata kura 29,000.....ila CDM na Viti 5 tu, wamepata kura 20,000......haoni kuwa CDM ina supportes wengi zaidi kwa sasa
 
Back
Top Bottom