Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 54,137
- 43,225
Unaionaje M4C?
M4C nimeiona inavyofanya kazi mikoani mpaka ulaya matunda yake tumeyaona imezaa kata 3.
Unaionaje M4C?
CDM kamwe haiwezi kutoa taarifa kujibu gazeti la udaku kama Rai
Udaku gani Rai wameandika? Hivi kuandika Chadema wamepata viti 5 ndio udaku?
M4C nimeiona inavyofanya kazi mikoani mpaka ulaya matunda yake tumeyaona imezaa kata 3.
Udaku gani Rai wameandika? Hivi kuandika Chadema wamepata viti 5 ndio udaku?
Nimelinunua gazeti la Rai, na nimelisoma lote lakini sijaona sehemu yoyote limeishambulia Chadema. Rai limeandika Chadema wamepata viti 5 vya Udiwani, CCM wamepata viti 22 vya Udiwani...sasa hapo kuna kosa gani.
Gazeti la RAI limeshambulia vikali chama cha CDM kwa kile lilichodai kufuja pesa ovyo kwa operesheni M4C huku chama hicho kikishindwa vibaya kwenye uchaguzi wa madiwani.
Gazeti hilo limedai matokeo hayo ya Chadema hayaridhishi kabisa wananchi ikilinganishwa na nguvu kubwa iliyotumiwa na chama hicho.
Matokeo ya udiwani yanaonyesha mgawanyo wa viti ulikuwa CCM 22 CDM 5 TLP 1 CUF 1.Hata hivyo CDM ikifanikiwa kurejesha viti vyake 2 huku ikiinyanganya CCM viti 3.

My Take:
Gazeti la RAI miezi iliyopita lilikuwa limeanza kurudu katika ramani yake kwa kutoa habari bila upendeleo lakini tangu Prince Bagenda aajiriwe kama Mhariri Mkuu amekuwa na chuki kubwa dhidi ya chama cha CDM na habari za gazeti hilo kila wiki zimekuwa zikikishambulia vikali chama hicho.Pia tangu Bagenda aajiriwe kumekuwa na makala maalum kila wiki za kushambulia viongozi wa chama hicho hasa Mkiti Freeman Mbowe n Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.Hata hivyo soko la gazeti hilo kwa sasa tangu aajiriwe Bagenda limeporomoka vibaya sana.
![]()
Hata mimi si mnunuzi wa gazeti hili toka limemilikiwa na Rostam Aziz kutoka mikononi mwa Jenerali Ulimwengu & Co.
Lakini ni lazima twende mbele na turudi nyuma kidogo. Si kila kinachozungumzwa negative kuhusu CDM ni kibaya kweli. Negativity nyingine ni sehemu ya kujenga. Huwezi kuwa na taasisi Malaika isiyokosea au kuhitaji kukosolewa. Hii habari haiwezi kuwa shambulio.
Tunaweza tukabeza habari hii ya gazeti la RAI lakini principally unapoendesha project lazima uzingatie uwiano wa input na output. Kilichofanywa na gazeti la RAI ni kupima mambo hayo. Sasa kinachotakiwa kufanywa na CDM ni kukanusha kwa kuegemea mizania hiyohiyo ya INPUT na OUTPUT. Sasa suala linahojiwa na RAI ni Je Input ya CDM kwenye chaguzi hizo za udiwani inaona na output? Hapo ndipo pa kuanzia kujadili na kupatolea ufafanuzi.
Tukianza kushambulia gazeti bila kuona mantiki ya kilichoandikwa tutakuwa tunakosea sana na huko si kukisaidia chama.
fmpiganaji, hili gazeti haliwezi hata siku moja kuiandika vizuri CDM kwa sababu ndio waliomfanya bosi wao ajiuzuru ubunge wa Igunga. Lakini pia 'Profesa' J. aliimba "ili nifanikiwe ninahitaji marafiki, ili nifanikiwe zaidi nahitaji maadui. Maadui wa CDM wamekuwa wakitoa mchango mkubwa sana (japo bila kulitambua hilo). M4C inatesa watu wengi sana, kwa kuona haraka unaweza kuona kuwa haijafanya kitu, ila kiukweli kuna kitu kikubwa sana kimefanyika, Vijana ambao bado wamenyimwa haki yao ya kupiga kura ni wangapi katika hizo kata, uandikishaji ulifanyika 2010. Siumizwi na wakala wa NYINYIEM (RAI) ila ni kuongeza umakini ktk M4C inayofuata.