Gazeti la Uhuru Vipi Tena?

Gazeti la Uhuru Vipi Tena?

mutua12

Member
Joined
Aug 20, 2008
Posts
39
Reaction score
2
Gazeti hili limetoa picha za majeruhi wa mabomu Mbagala ukurasa wa mbele wakiwa wamelazwa chini wawili wawili kwenye godoro moja.

Binafsi sijafurahishwa na picha hizo likiwa ni gazeti la chama tawala lisingeonyesha picha hizo.

Wengine mnasemaje?
 
hata mimi nimeshangaa leo. Nimepita kwenye mbao za wauza magazeti mipicha kibaaao sijui hata mantiki yake nini. Wangeweka picha hata za Makamba akiwa busanda
 
Sijakuelewa Mkuu! Nini hasa hakijakufurahisha? Kuonesha picha za majeruhi? Au kuonesha majeruhi wakiwa wamelazwa kwenye gororo moja?
 
wameonesha jinsi gani sera ya afya ya CCM inavyotekelezwa
 
Lol, huenda wanaanza kumchimba JK taratibu..2010 inakaribia.
 
Sijakuelewa Mkuu! Nini hasa hakijakufurahisha? Kuonesha picha za majeruhi? Au kuonesha majeruhi wakiwa wamelazwa kwenye gororo moja?

Hata mimi kidogo sijaelewa..Kama ni hiyo picha kutolewa mbele kwenye gazeti wakati tukio limepita au hao majeruhi kulala wawili wawili kwenye gorodo moja!

Tueleweshe vizuri mkuu!
 
Gazeti hili limetoa picha za majeruhi wa mabomu Mbagala ukurasa wa mbele wakiwa wamelazwa chini wawili wawili kwenye godoro moja.

Binafsi sijafurahishwa na picha hizo likiwa ni gazeti la chama tawala lisingeonyesha picha hizo.

Wengine mnasemaje?

wacha unafiki sasa wewe unataka ukweli ufichwe ?
 
watu wa mbagala wamechoshwa na mabomu, kuwaweka kwenye picha ndugu zao inawaongezea machungu,
 
wacha unafiki sasa wewe unataka ukweli ufichwe ?

Siyo kwamba ukweli ufichwe kwani nani hajui kuwa watu wengi wamedhurika, na si lazima utangazie watu wote hata wapita njia , zingewekwa basi hata ndani siyo front page!!!!!!!!
 
Acha Serikali ijianike yenyewe,na kuonyesha mapungufu yake hadharani,hizo picha hazina shida,tunachopaswa kuelewa hapo ni kwamba nchi iko mahali pabaya sana katika kila sekta.
 
Uhuru nao wanaanza kuamka. Hakuna tena kuficha mambo uvunguni.
 
Siyo kwamba ukweli ufichwe kwani nani hajui kuwa watu wengi wamedhurika, na si lazima utangazie watu wote hata wapita njia , zingewekwa basi hata ndani siyo front page!!!!!!!!

Kwani hao wapita njia ni raia wa wapi?hapo zilipowekwa kwenye front page ndo penyewe sasa,na ni vizuri kuelewa hali halisi ili unapopigana vita ya UFISADI ujue unapigana kweli ili kuondoa hizo kero,maana hiyo watu kulala wawili wawili ni matokeo ya UFISADI.
 
Ni vizuri hali halisi ionyeshwe wazi ili kesho na kesho kutwa vibaraka watakapopita mitaani kusema walitimiza ahadi ya 'maisha bora' kwa kila mtanzania muwapigie makofi mkijua nini mnafanya. Mpaka sasa hakuna aliyewajibishwa kwa hako katukio, wala hakuna mtu anayelishangaa hilo;ila tukio kuwekwa wazi kwenye gazeti watu wajue linashangaza.
 
gazeti hili limetoa picha za majeruhi wa mabomu mbagala ukurasa wa mbele wakiwa wamelazwa chini wawili wawili kwenye godoro moja.

Binafsi sijafurahishwa na picha hizo likiwa ni gazeti la chama tawala lisingeonyesha picha hizo.

Wengine mnasemaje?
kwani gazeti la chama ndio nini? Ule si ukweli?
 
Mhariri akificha ukweli hamtaki akiweka ukweli hamtaki,mnataka nini sasa? Nenda Amana Hospital, wagonjwa wanalala wangapi kitanda kimoja?
 
Mhariri akificha ukweli hamtaki akiweka ukweli hamtaki,mnataka nini sasa? Nenda Amana Hospital, wagonjwa wanalala wangapi kitanda kimoja?

Malil mbona huelewi? Anaye chukia kuwekwa picha hizo ni ambaye hataki haya mapungufu yaonekane. Soma kati kati ya mstari mkuu
 
Mkuu Malila

Nakuunga mkono mia kwa mia. Watu wengine kusema kwiiiiingi lakini porojo tu. Kila kitu kwao hakifai.
 
msondo wameimba 'mambo hadharani' hakuna kuficha tena maana kama wao wakificha basi magazeti mengine yataweka hadharani.
 
Siyo kwamba ukweli ufichwe kwani nani hajui kuwa watu wengi wamedhurika, na si lazima utangazie watu wote hata wapita njia , zingewekwa basi hata ndani siyo front page!!!!!!!!

Hata kurasa za ndani haitakiwi bila idhini yao.

Hii kawaida ya kuonyesha wagonjwa katika hali waliyonayo wamelala chini na vikanga havitoshi kuwasitiri kikamilifu ni kuwadhalilisha na kuvunja maadili ya siri za mgonjwa.
 
Dilunga,

Unajuaje kama wana ridhaa ya mgonjwa na mgonjwa anataka kuonekana hivyo, pengine katika kutaka kupata msaada zaidi?
 
Back
Top Bottom