Gazeti la Uhuru: Tamati ya CHADEMA imefikia

Gazeti la Uhuru: Tamati ya CHADEMA imefikia

Ben kinachokufa kinajulikana kijana mwenzangu ni vema taratibu za misiba mkaziandaa chama cha kupigana kwenye vikao hakiwezi kudumu.

Kwenye Red nina mashaka makubwa kama wewe ni kijana. Kama ni kweli wewe ni kijana na hujitambui unatumiwa kwa kulipwa buku saba kwa siku kutetea majizi ya CCM huku wazazi wako wanateseka bila hata huduma za matibabu, ukizeeka lazima utakuwa mchawi...
 
Baada ya viongozi wa CHADEMA kumshushia kipigo aliekuwa Mwenyekiti wa CDM mkoani Arusha,SAMSON MWIGAMBA hali imezidi kuwa tete na viongozi waandamizi ndani ya chama hicho wamesema muda wa kusambaratika umewadia.

Pia wamesema Ubabe na Kunajisiwa kwa Katiba na Demokrasia ndani ya chama hicho kamwe hakuwezi kukinusuru zaidi ya kuongeza kasi ya kukitafuna.

Mwigamba ambae anatajwa kuwa "Muhimili"Mkubwa na "Muhimu" ndani ya Chama hicho mkoani Arusha,alishambuliwa na viongozi wenzake na walinzi wa Red Brigade kwa madai ya kuwa msaliti, huku kiongozi mmoja akidaiwa kumtolea BASTOLA!!

CHANZO;GAZETI LA UHURU.

Uhuru kwani nalo ni Gazeti au kipepperushi? Hacha kuchafua majina ya vitu vya msingi kwa kuita kipeperushi Gazeti bhana!
 
Moja kasumba zitakazoigharimu CDM siku zijazo ni hii tabia ya kudharau maoni na mawazo ya baadhi ya wanachama pale wanapokosoa chama chao na kudhani wanaofanya hivyo ni CCM. Kwa mfano, mleta uzi kwa kutumia uelewa wake mdogo wa kufikiri ameona eti kitendo cha kupigana kwenye mkutano kwa baadhi ya viongozi waandamizi na wanachama eti kumesababishwa na CCM.

Ifike sehemu utuachane na mawazo ya kipumbavu. Jaribuni kujibu hoja za wanachama. Msijichimbie kaburi
hivi wewe mkeo km anakojoa kitandani,utaenda kumtangaza sokoni au kijiweni?
 
chadema haiwezi kufa kwa kuwafukuza mamluki na mapandikizi ya maccm ndani ya chama.
chadema ni mashuhuri na ipo mioyon mwa watanzania kuliko kiongoz yeyote ndani ya chama.
kama utafanya ujinga tupa kuleeeeee bila kujali cheo chako ni bora kuwa na makomando wachache vitan kuliko kuwa na mgambo wengi.
 
Khaa!! Dont interrupt your enemy when he is doing some mistakes :A S 39:
 
Ben kinachokufa kinajulikana kijana mwenzangu ni vema taratibu za misiba mkaziandaa chama cha kupigana kwenye vikao hakiwezi kudumu.

Bhanji+2.jpg
 

Vurugu Chadema: Mwigamba apinga kusimamishwa,


mwigamba.jpg
Hizi tuhuma kuwa natumiwa na Zitto nimekuwa nikizisikia, lakini huo ni upofu, mimi si mtu wa kutumika nina elimu yangu nzuri ya shahada ya kwanza ya utawala wa biashara, najua ninachokifanya ni kwa masilahi ya chama. Samson Mwigamba
Na Mussa Juma, Mwananchi

Posted Jumatatu,Oktoba28 2013 saa 8:31 AM
Kwa ufupi

  • Mwigamba asema kikao kilichomsimamisha hakina mamlaka, adai chanzo ni kudaiwa kutumiwa na Zitto;



Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanaamini kuna uwezekano kuwa mgogoro katika chama hicho unatokana na vuguvugu la uchaguzi uliosogezwa mbele hadi mwakani.

Kuna wasiwasi huenda yakajirudia ya mwaka 2009 wakati Zitto alipojaribu kuwania nafasi ya Mwenyekiti dhidi ya Mbowe na kuzua mvutano mkubwa ndani ya chama hicho.

Hata hivyo, Zitto aliweka bayana kuwa hawezi kuzungumzia mambo hayo kwani hafahamu hata huo uchaguzi wa ndani utafanyika lini.

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mwenezi wa Chadema, John Mnyika alifafanua kuwa kikao kilichomsimamisha Mwigamba kilikuwa halali.

Mnyika alisema, hata hivyo, ikiwa Mwigamba hajaridhishwa na hatua hiyo anapaswa kukata rufaa na siyo kulalamika kwenye magazeti.

Alisema kuwa Mwigamba anapaswa kusoma katiba ya chama hicho na kuelewa mambo ya chama yanamalizwa na kikao husika na siyo kwenye vyombo vya habari.

"Kikao kile kinaweza kumsimamisha ila kama hajaridhishwa na uamuzi ule basi aende kwenye ngazi inayofuata," alisema Mnyika.

Mnyika, hata hivyo, alisema kwa ngazi ya taifa wanasubiri taarifa ya kikao kilichomsimamisha kwani walikuwa hawajapokea na wala kutumiwa malalamiko yoyote na Mwigamba
 
Chanzo cha habari gazeti la uhuru???????=======++++++
Chombo cha habari na propaganda cha maccm????????========++++++
Kuna mtanzania anayesoma gazeti la uhuru?
Kazi ipo.
 
[h=1]Viongozi Chadema wazipiga kavukavu kwenye mkutano wa Mbowe[/h] nusura mbowe apigwe


Chadema+Mkong%2527oto+Clip.jpg
Mwasisi wa Chadema Edwin Mtei (mwenye kofia) akizungumza kwenye mkutano wa siku tatu wa Baraza la Kanda ya Kaskazini ya chama hicho jijini Arusha juzi. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kanda Mchungaji Israel Natse, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu wa Kanda, Amani Golugwa. PICHA | FILBERT RWEYEMAMU
Na Mussa Juma na Peter Saramba, Mwananchi

Posted Jumapili,Oktoba27 2013 saa 7:2 AM
Kwa ufupi

  • Mwigamba amekuwa mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha tangu mwaka 2009, akiwa pia Mjumbe wa Baraza la Uongozi Kanda ya Kaskazini, Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano Mkoa, Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chadema.




0
inSha​
Arusha. Mkutano wa Baraza la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini juzi uligeuka ukumbi wa ngumi, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kushushiwa kipigo.



Mwigamba alishushiwa kipigo hicho na baadhi ya viongozi wenzake wa chama kwa madai ya usaliti na tayari amesimamishwa uongozi kwa muda usiojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas jana alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na viongozi hao wa Chadema kufikishana polisi.

Alikutwa na zahama hiyo mbele ya viongozi wakuu wa Chadema Taifa, Mwenyekiti, Freeman Mbowe na mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei katika Hoteli ya Coridal Spring.

Viongozi hao wamekuwa wakifanya ziara za aina hiyo nchi nzima, kuimarisha chama na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na uchaguzi mkuu ujao wa Rais na wabunge mwaka 2015.

Habari kutoka ndani ya mkutano huo zinaeleza kuwa hatua hiyo ilifuatia tuhuma kwamba Mwigamba alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums, unaodaiwa kukichafua chama hicho.

Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati viongozi wote wa juu wa chama hicho, wakiongozwa na Mbowe walipokuwa wakijadili mustakabali wa chama hicho, mkutano ambao ulihudhuriwa na wabunge karibu wote wa Chadema wa kanda hiyo.

Hata hivyo, wakati mijadala ikiendelea baadhi ya viongozi wa chama hicho, akiwamo Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema walimtuhumu Mwigamba kutuma ujumbe kwenye mtandao huo, uliokuwa ukizungumzia ufisadi ndani ya chama hicho, wakidai alitaka Mwenyekiti Mbowe kukubali kuchunguzwa.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwigamba alisema kuwa baada ya Lema kutoa tuhuma hizo aliungwa mkono na viongozi wengine na vijana waliokuwa wameimarisha ulinzi, kumvamia na kuanza kumpiga pamoja na kumnyang'anya kwa nguvu kompyuta mpakato (Laptop), aliyokuwa nayo, kisha kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi, mjini Arusha.

"Wamenipiga sana na kuniweka ndani, ila nashukuru Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha (OCCID), alikuja na kunitoa saa 5:00 asubuhi," alisema Mwigamba.

Alisema kuwa leo katika mkutano wake na waandishi wa habari ataeleza yote yaliyotokea na hatua atakazochukua, kwa kuwa yeye ni kiongozi wa juu wa chama.

Hata hivyo, alieleza kwamba bado anashauriana na wanasheria wake kuona kama anaweza kuwachukulia hatua waliompinga.
 
chadema is real dying, im happy of that

Ha haa haa kwi kwi kwi Munaomba CHADEMA ife ili mbaki munagombea na vivuli kama enzi zilee.CHADEMA haifi ina mungu mtakufa wenyewe na shetani wenu CHADEMA hiyooo mpaka magogoni tiii.
 
CCM inachota fedha nyingi sana za walipakodi, na inaongezewa fedha za kununua mamluki toka kwa watu wanaofanya biashara fulani fulani.

Hata hivyo, hawataweza kuiangamiza CHADEMA.

Walitumia mabomu ya machozi na vitu vyenye ncha kali wakashindwa, wakatengeneza video ya ujangili wakashindwa, wakarusha magruneti wakashindwa, na sasa wameamua kutumia mamluki wao. Watashindwa pia.

Watanzania wa leo wanaikataa ccm na mambo yake yote.

Kazeni buti makanda. Tuko nyuma yenu, na hatudanganyiki. Ukiondoa wachumia tumbo wachache, hakuna Mtanzania anayetaka hii hali ya sasa iendelee. Na kuikubali ccm ni kutaka tubaki kama tulivyo!
 
Kinachonifurahisha kwa CHADEMA ni kufanya kazi kama king'amuzi kinavyoweza ku-detect hata vilivyojificha ndani ya tumbo!

Tutawang'amua mmoja hadi mwingine hadi wabaki wale wenye dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya tunayoyaota!

Mamluki wengine ni kama majoka ya kibisa tu,hayana athari...Tutaendelea kuwalisha unga hadi 2015 then tuyatelekeze!

SHIBUDAAAA...Kama nakuona vile!
 
Huoni aibu kutetea uongo na uovu unaofanywa na mbowe na slaa au na wewe ni mnufaika wa huo uozo ushindwe na ulegee.
Kwa kweli kutetea uovu ndani ya chama, ili kumainrain status quo na makosa sawa sawa na kukisaliti chama. Kosa la mwigamba ni kushindwa kustrike balance. Makundi yanaibomoa CCM; makundi yatakibomoa CHADEMA.
Tuendelee kuadibishana huku tukifanyia kazi mapungufu yaliyomo ndani.
 
Wa Tanzania wenzangu siasa za fitina zitatuangusha na kutukandamiza,hasa katika nyanja za maendeleo.CCM wamejikita kuihujumu CDM badala ya kuletea Watanzania maendeleo baada ya miaka 50 ya uhuru.
Watanzania wanapima na hawadanganyiki kama ambavyo wengi wanafikiri,CDM watoweni wasaliti wote mubakiwe na wazalendo wa kweli na sio waliopo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi,ili kuikomboa nchi hii kutokana na umaskini uliokithiri kwa wananchi walio wengi kwa kipindi kirefu sasa.
Hao wachumia tumbo hawatufikishi kokote zaidi ya kutuingiza kwenye mabalaa na migogoro isiyoisha na kutuondoa kwenye agenda ya msingi ya kutuondoa kwenye umaskini baada ya miaka hamsini ya uhuru licha ya rasilimali nyingi tulizonazo na rasilimali watu na kutaka kudhoofisha upinzani kwa mikakati yao dhaifu yenye kuwashusha hadhi.

Ushauri kwa CCM: Bado hawajachelewa kurekebisha makosa yao kama wana nia ya dhati ya kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo ya kweli na si kudhoofisha upinzani ili waendelee kuwepo madarakani bila tija.Watakuwa wanajidanganya kufanya propaganda ambazo zinawapaisha wapinzani na bila kujijua,muda ambao ungetumika kukijenga Chama cha Mapinduzi
 
hivi na wewe mtoa mada ilikuwaje hadi kupoteza resources zako kwa gazeti la uhuru
 
CDM tutatoa kichapo kwa kila msaliti hata kuvunja bandama kama ilivyo vitani kamanda akionekana kurudi nyuma na wakati wenzio wanapambana kusonga mbele ukihurumiwa utavunjwa mguu lakini vinginevyo unatakiwa hata kuuawa kwa sababu umekuwa mwoga na unaweza hata kusaliti ukawatosa wenzio

Kwahiyo kwa vile hii ni vita CDM tuwe fit kuwamaliza wasaliti kabla hawajatumaliza sisi ..PEEEEOOOPLEEEEEE'S!
 
Back
Top Bottom