Gazeti la UHURU nalo lifungiwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la UHURU nalo lifungiwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Oct 15, 2008.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Siku ya Jumatatu ya juzi Magazeti ya Bongo yalisheheni kwa habari za Matokeo ya Uchaguzi wa Tarime yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu na Watanzania.

  Nilifuatilia kupitia kipindi cha "Watanzania Tuzungumze Magazeti" cha RFA. Katika kipindi hicho Magazeti yote yalisema CHADEMA walikuwa wakiongoza kwa kura kwa mujibu wa kura kztika vituo vya Uchaguzi; Ni gazeti la UHURU tu ambalo ni la propaganda la CCM ndilo liliripoti tofauti na magazeti yote (likiwemo Habari Leo ambalo lilisema CHADEMA wanaongoza).

  UHURU walitoa taarifa kuwa CCM ilikuwa inaongoza katika vituo 11 kato ya 20 vya kupigia kura SIkubahatika kulisoma gazeti hilo lakini kwa udondozi ule wa RFA nilipata mawazo yafuatayo:-

  Moja, UHURU lilitoa ripoti ya Uongo ambayo kwa hali ya Tarime wakati ule taaifa ile ingeweza kuleta machafuko makubwa maana CHADEMA na wafuasi wao waliamini kuwa wameshindwa na habari ile ilitosha kuwapa picha wapiga kura kuwa CCM wameiba kura.

  Mbili, Kama kina cha habari kilikuwa hivyo, basi gazeti la UHURU liliudanganya umma wa WaTz.

  Tatu, Inaelekea kulikuwa na njama za kupora ushindi wa WanaTArime na habari hizo za UHURU ziliandaliwa mapema kulingana na njama hizo ili kuwaondoa mashaka WaTZ juu ya matokea ambayo CCM walikuwa wameandalwa kushinda.

  Naomba WanaJF waliopata gazeti hilo watubandikie hapa na ikithibitika kuwa kichwa cha habari walichokitumia kinaendana na maudhui ya habari hiyo basi namuomba Waziri Mkuchika alifungie Gazeti hilo kwa kutoa habari za uongo na za kuwagombanisha WaTZ na pia kuhatarihsa amani Tarime.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  hilo ni gazeti lake la propaganda la chama chake na yeye ni waziri wa Propaganda wa sisiemu sasa unadhani huo anaona ni uchochezi? kama lingekuwa gazeti jingine ndio limeandika ujinga huo nakwambia leo angeliitwa na waziri huyo wa propaganda wa sisiemu ili ajieleze kwa nini asifungiwe kwa kutoa habari za uongo wakati yeye si tume ya uchaguzi.
  Lakini kwa kuwa ni gazeti la chama kinachotawala kwa mabavu hawezi katu.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Soma vizuri bandiko lako usije ukawa wewe ndie muongo
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kuongoza sio kushinda!
   
Loading...